Engine oil gani ni nzuri kwa Gari aina ya IST?

Engine oil gani ni nzuri kwa Gari aina ya IST?

Mi niwekewa ya 20w50 kwnye ist, matumiz yake ni kwenda ofisini na kurudi nyumbani nipo dar,je ni sawa au ndio wananiulia gari?
Siyo sahihi mkuu..na isitoshe matumizi ni ofisini, nyumbani...Fanya kama walivyosshauri wengine
 
Kama engine bado ina hali nzuri <18,000km Tumia mult grade full synthetic 5w-30 ukiikosa chukua 10w-30 achana na SAE 40 hizo ni monograde zina himili joto kali tu, alafu ni nzito hivyo usambaaji wake sio nzuri kwenye ingini hasa pale unapowasha gari hivyo ingine kuwa nzito na kusagika kwa vyuma. Hiyo ni nzuri kwa gari zinazopiga kazi mda mrefu ka daladala au yale ambayo yalishachoka tayari ili kuhimili joto kubwa la ingini na kuzuia friction
 
Nimewekewa engine oil ya total 20w50 kwenye ist, engine 1nz cc 1500 gari imetembea km 190,000.. tafadhali naomba maarifa je ni engine oil sahihi?
 
Hukupaswa kutumia 20w 50 kwa gari ndogo ka iyo ..hizi oil ni kwa heavy duty or load cars au yale ya diesel
 
Hukupaswa kutumia 20w 50 kwa gari ndogo ka iyo ..hizi oil ni kwa heavy duty or load cars au yale ya diesel
Shukran ndugu, naomba ushauri je engine oil sahihi kabisa kwa hiyo "bibi kizee wangu" ni ipi
 
Hizi namba kila moja ina tafsiri yake.
Unapokuta mfano 5W 30. Namba ya kwanza kabla ya W inawakilisha uzito wa oil. Kadri namba inavyozidi kuwa ndogo, ndivyo oil inavyozidi kuwa thin hivyo kuwezesha better performance at the cold start.

W simply inawakilisha winter wengine wanasema Weight wengine wanasema Watt...lakini inawakilisha Winter..

30 inawakilisha viscosity ( ile hali ya oil kuwa kama ina nata nata fulani hivi.)
Hii ina maana kwamba injini inpopata joto lake la juu ambalo linatakiwa ili ifanye kazi vizuri, viscosity ya oil hii bado itabaki katika kipimo hicho cha 30 ambacho kimewekwa na watengenezaji, hali kadhalika kwa oil namba 40 au 50

Kwa mantic hii oil 5w 30 ni nyepesi kuliko 10w 30.

Oil hizi zenye namba mbili yaani 5w 30 kwa lugha nyingine zinaitwa multi grade oils....ni oil ambayo imetengenezwa kufanya kazi katika mazingira ya baridi sana na joto sana.

Lakini hizi SAE 40 za kawaida ni mono garde....hizi ni maalumu kwa mazingira ya joto tu...na ndiyo maana kwa siai tulioko huku Arusha ikifika lile baridi la mwezi wa saba, kama gari ni ndogo na umeweka SAE 40, ukiliwasha asubuhi utasikia injini inavuma sana kwa muda mrefu...injini ikishafikia joto kiasi fulani ndiyo unaona inatulia...wakati unasubiri injini ipate moto, unakuwa unasaga vyuma..

Ukifuatilia zamani nchi zenye baridi kama huko Ulaya, walikuwa na oil za aina mbili..nzito kwa ajili ya msimj wa joto na nyepesi kwa ajili ya msimu wa baridi....watu walilazimika kumwaga oil msimu wa bari na kuweka oil nyepesi ya kukabiliana na baridi...hali kadhalika msimu wa joto, walimwaga oil nyepesi na kuweka nzito.

Kuepuka purikushani hizo, ndiyo Society of Automobiles Engineers (SAE) wakaja na oil ambayo ni mult grade mfano 5w30, 10w 30,10w40 n.k....oil hii ukishaiweka haichagui baridi wala joto wewe ni kuangalia tu muda wa service ukifika unaimwaga.

Hatari ya SAE 40 kwa garo dogo, haijalishi unaishi Dar au Arusha.... ukiwasha gari asubuhi wakati injini imepoa, oil hii kitaalam huchelewa kufika sehemu za juu za injini kutokana na uzito wake...pale inapichelewa, vyuma vinaendelea kusagana na unaendelea kuua injini yako taratibu...

SAE 40 ukitumia kwa magari makuu kuu sana haina shida...mfano madaladala au gari ambalo mileage imeenda juu sana pengine zaidi ya 180000km..
Hongera sana, maana nilpoona tu Society of Automobiles Engineers (SAE). Nikajua utakachoshauri ni sahihi, kwa kuwa umesawasoma hao wataalamu
 
Wakuu kuna hii gari nimeagiza sasa natafakari ni namna gani ntapata chaguo sahihi la oil ya engine.

Nimejaribu ku google maana mi ist yangu engine yake ni 2NZ sasa majibu ya google yanakuja kama hivi. 5W-30 na 10W-30 kwamba ndo recommended fuel engine kwa engine ya namna hiyo.

Ila katika kupeleleza zaidi kati ya 5W-30 na 10W-30 nikakuta kwamba 5W-10 inatumika kwenye majira ya baridi of which inaweza isiwe chaguo zuri kwangu kwakuwa bongo baridi sio kivile.

Hiyo 10W-30 ndo imekuwa indicated kwamba inatumika zaidi kwenye majira ya joto of which naona kama itaendana na mazingira ya bongo.

NOTE: Kuna hii oil ya 15w40 ambayo nimeona wanaisema kwamba inatumika sana kwenye nchi za tropical ila naiogopa kidogo maana wanasema ipo thicker sana angali mimi cc ya gari yangu ni 1.3l sasa naogopa hiyo oil inaweza isisupport hizo cc.

Hapo hapo nikakuta hizi fuel engine kuna wanaziita synthetic na mineral. Ikionekana synthetic iko reliable kuliko hiyo mineral.

Sasa hapa nlikuwa nauliza itakuwa sahihi kutumia kwenye hii IST fuel yenye hizi specification 10W-30 Synthetic? Na je ni brand gani nzuri kutumia? maana leo nimeenda shell wakanionesha brand ya castrol oil.. Sasa ndugu wazoefu itakuwa sahihi kwa gari langu.

Au nyie wenye IST wengine huwa mnatumia engine fuel ya aina gani?

Ntashukuru kwa majibu.

Sasa hapa najiuliza

BAADHI YA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU

---

---

---

---
Kwanza hio gari haina engine hio ...
 
Niliimwaga nikaweka total 5w40 ..
Angalau.

Mimi uwa ninaweka 5W30 Fully Synthetic ya Castrol.

A5455964-removebg-preview.png

download.jpeg
 
Mkuu oil ya gearbox kwenye cami ni ipi
Hizi namba kila moja ina tafsiri yake.
Unapokuta mfano 5W 30. Namba ya kwanza kabla ya W inawakilisha uzito wa oil. Kadri namba inavyozidi kuwa ndogo, ndivyo oil inavyozidi kuwa thin hivyo kuwezesha better performance at the cold start.

W simply inawakilisha winter wengine wanasema Weight wengine wanasema Watt...lakini inawakilisha Winter..

30 inawakilisha viscosity ( ile hali ya oil kuwa kama ina nata nata fulani hivi.)
Hii ina maana kwamba injini inpopata joto lake la juu ambalo linatakiwa ili ifanye kazi vizuri, viscosity ya oil hii bado itabaki katika kipimo hicho cha 30 ambacho kimewekwa na watengenezaji, hali kadhalika kwa oil namba 40 au 50

Kwa mantic hii oil 5w 30 ni nyepesi kuliko 10w 30.

Oil hizi zenye namba mbili yaani 5w 30 kwa lugha nyingine zinaitwa multi grade oils....ni oil ambayo imetengenezwa kufanya kazi katika mazingira ya baridi sana na joto sana.

Lakini hizi SAE 40 za kawaida ni mono garde....hizi ni maalumu kwa mazingira ya joto tu...na ndiyo maana kwa siai tulioko huku Arusha ikifika lile baridi la mwezi wa saba, kama gari ni ndogo na umeweka SAE 40, ukiliwasha asubuhi utasikia injini inavuma sana kwa muda mrefu...injini ikishafikia joto kiasi fulani ndiyo unaona inatulia...wakati unasubiri injini ipate moto, unakuwa unasaga vyuma..

Ukifuatilia zamani nchi zenye baridi kama huko Ulaya, walikuwa na oil za aina mbili..nzito kwa ajili ya msimj wa joto na nyepesi kwa ajili ya msimu wa baridi....watu walilazimika kumwaga oil msimu wa bari na kuweka oil nyepesi ya kukabiliana na baridi...hali kadhalika msimu wa joto, walimwaga oil nyepesi na kuweka nzito.

Kuepuka purikushani hizo, ndiyo Society of Automobiles Engineers (SAE) wakaja na oil ambayo ni mult grade mfano 5w30, 10w 30,10w40 n.k....oil hii ukishaiweka haichagui baridi wala joto wewe ni kuangalia tu muda wa service ukifika unaimwaga.

Hatari ya SAE 40 kwa garo dogo, haijalishi unaishi Dar au Arusha.... ukiwasha gari asubuhi wakati injini imepoa, oil hii kitaalam huchelewa kufika sehemu za juu za injini kutokana na uzito wake...pale inapichelewa, vyuma vinaendelea kusagana na unaendelea kuua injini yako taratibu...

SAE 40 ukitumia kwa magari makuu kuu sana haina shida...mfano madaladala au gari ambalo mileage imeenda juu sana pengine zaidi ya 180000km..
 
Elimu ya bure..
Kwa gari lako na kwa mazingira ya Tanzania tumia 5w 30,
Ukikosa nenda 10w 30.....
.Anayekuambia hizi oil ni za nchi za baridi amekariri bila kusoma...

Iko hivi..
5w 30 ina uwezo wa kuhimili baridi kali kuanzia -30°C bila kupoteza viscosity yake...pia oil hii ina uwezo wa kuhimili kiwango cha juu cha joto ambacho ni +40 °C bila kupoteza viscosity yake..
Hiki kiwango cha joto nilichotaja ni joto la mazingira unayoishi (outside temperature)

10w 30 ina iwezo wa kufanya vizuri kuanzia joto la -20°C mpaka joto la +40°C...

Hii ina maana kwamba oil 5w30 na 10w 30 zina uwezo wa kusambaa haraka sehemu za injini hata kama gari limewashwa kwenye mazingira ya baridi sana kibongo bongo tunasema Arusha, Iringa, Mbeya na maeneo mengine yenye baridi.
Pia inahimili joto kali kama la Dar, Zanzibar nk.

Kwa hiyo hizi oil zinamudu mazingira yote na ndiyo maana car manufacturers wa siku hizi wana recommend oil hizi zaidi siyo Nissan, Toyota,Honda, Subaru,Mazda n.k...

Ukinunua nunua full synthetic ukikosa ndiyo ununue hizi mineral oil ambazo usivushe 3000 km.

Synthetic unaweza ukaenda km 5000 na zaidi kama umefunga oil filler genuine ndiyo ufanye service nyingine..

Full synthetic inahimili dhoruba ngumu kama milima, matope, joto, baridi, racing bila kupoyeza viscosity yake....na bei yake imesimamia kucha.

Agalia fundi wa mwembeni asikushauri uweke SAE 40 ya kawaida...hii oil ni nzito sana na utakuwa unalitesa gari bila wewe kujua...

Oil ndiyo DAMU ya engine.....zingatia if you love your car.

Akipuuza huu ushauri wako huyu jamaa hakuna sehem atasaidiwa. Bro umeeleza kwa ufasaha kabisa with facts, safi.
 
Back
Top Bottom