Engine oil gani ni nzuri kwa Gari aina ya IST?

Elimu ya bure..
Kwa gari lako na kwa mazingira ya Tanzania tumia 5w 30,
Ukikosa nenda 10w 30.....
.Anayekuambia hizi oil ni za nchi za baridi amekariri bila kusoma...

Iko hivi..
5w 30 ina uwezo wa kuhimili baridi kali kuanzia -30°C bila kupoteza viscosity yake...pia oil hii ina uwezo wa kuhimili kiwango cha juu cha joto ambacho ni +40 °C bila kupoteza viscosity yake..
Hiki kiwango cha joto nilichotaja ni joto la mazingira unayoishi (outside temperature)

10w 30 ina iwezo wa kufanya vizuri kuanzia joto la -20°C mpaka joto la +40°C...

Hii ina maana kwamba oil 5w30 na 10w 30 zina uwezo wa kusambaa haraka sehemu za injini hata kama gari limewashwa kwenye mazingira ya baridi sana kibongo bongo tunasema Arusha, Iringa, Mbeya na maeneo mengine yenye baridi.
Pia inahimili joto kali kama la Dar, Zanzibar nk.

Kwa hiyo hizi oil zinamudu mazingira yote na ndiyo maana car manufacturers wa siku hizi wana recommend oil hizi zaidi siyo Nissan, Toyota,Honda, Subaru,Mazda n.k...

Ukinunua nunua full synthetic ukikosa ndiyo ununue hizi mineral oil ambazo usivushe 3000 km.

Synthetic unaweza ukaenda km 5000 na zaidi kama umefunga oil filler genuine ndiyo ufanye service nyingine..

Full synthetic inahimili dhoruba ngumu kama milima, matope, joto, baridi, racing bila kupoyeza viscosity yake....na bei yake imesimamia kucha.

Agalia fundi wa mwembeni asikushauri uweke SAE 40 ya kawaida...hii oil ni nzito sana na utakuwa unalitesa gari bila wewe kujua...

Oil ndiyo DAMU ya engine.....zingatia if you love your car.
Vipi kuhusu 20w50
 
Wadau nina ist ya 2006, juzi niliipiga sehemu radiator ikapinda ikagusa fan na kuzuia fan kuzunguka... Kulikopelekea motor kuungua.

Baada ya motor kuungua fan ikashndwa kuzunguka na mashine ikaanza kuheat.

Shida yangu ni kuwa nishaweka motor zingine kama 2 hivi na bado injini inaheat kwa kilometer chache tu hata 30 hazifiki na maji yanaisha kabisa.

Nb.
Rejeta haivuji, sasa hapa solution ipo vipi.
Je kuna aina ya moto special kwa hizi gari, au fan special,. Na ni wapi naweza nikaipata na kwa gharama gani maaana nateseka saana na nina safari. Ya kwenda bukoba week ijayo.
Unagongaje gari kizembe hivyo? Huwa unachati wakati unaendesha gari mzee ama ni vurugu zenu zile tulizowazoea nazo
 
Na kwa kuongezea tu oil filter genuine bei yake haipungui 20000 ukikuta unauziwa chini ya hapo hiyo sio genuine na mafundi wengi wanawashauri wateja kutumia sae 40 kwa sababu bei yake ipo chini sana na wengi wa mafundi wa uswahilini hawana elimu ya kutosha kuhusu hii oil
Very true
 
Oil filter huwa n 10k zaid ya hapo fundi anakupiga
 
Wakuu kuna hii gari nimeagiza sasa natafakari ni namna gani ntapata chaguo sahihi la oil ya engine.

Nimejaribu ku google maana mi ist yangu engine yake ni 2NZ sasa majibu ya google yanakuja kama hivi. 5W-30 na 10W-30 kwamba ndo recommended fuel engine kwa engine ya namna hiyo.

Ila katika kupeleleza zaidi kati ya 5W-30 na 10W-30 nikakuta kwamba 5W-10 inatumika kwenye majira ya baridi of which inaweza isiwe chaguo zuri kwangu kwakuwa bongo baridi sio kivile.

Hiyo 10W-30 ndo imekuwa indicated kwamba inatumika zaidi kwenye majira ya joto of which naona kama itaendana na mazingira ya bongo.

NOTE: Kuna hii oil ya 15w40 ambayo nimeona wanaisema kwamba inatumika sana kwenye nchi za tropical ila naiogopa kidogo maana wanasema ipo thicker sana angali mimi cc ya gari yangu ni 1.3l sasa naogopa hiyo oil inaweza isisupport hizo cc.

Hapo hapo nikakuta hizi fuel engine kuna wanaziita synthetic na mineral. Ikionekana synthetic iko reliable kuliko hiyo mineral.

Sasa hapa nlikuwa nauliza itakuwa sahihi kutumia kwenye hii IST fuel yenye hizi specification 10W-30 Synthetic? Na je ni brand gani nzuri kutumia? maana leo nimeenda shell wakanionesha brand ya castrol oil.. Sasa ndugu wazoefu itakuwa sahihi kwa gari langu.

Au nyie wenye IST wengine huwa mnatumia engine fuel ya aina gani?

Ntashukuru kwa majibu.

Sasa hapa najiuliza

BAADHI YA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU

---

---

---

---
sasa mi naona unajua kila kitu afu unauliza tena, unajua mpaka recomeended oil ni 10w30 au 530 unatakaje sasa
 
Unagongaje gari kizembe hivyo? Huwa unachati wakati unaendesha gari mzee ama ni vurugu zenu zile tulizowazoea nazo
Haikuwa kizeembe Man. Ni saa 8 usiku kwenye u turn bubu road inayotengenezwa (kilwa road).. upande mmoja upo flat wa pili kukawa na shimo ndani ya shimo kukawa na jiwe afu kuna maji. Ni ajali ambayo humkuta hadi mwenye tahadhari.

Sikuombei mabaya ila natamani ikupate maana wahenga walinena.
"INABIDI UONE VIFO VINGI ILI UJUE THAMANI YA UHAI"
 
Ki

Kizuri ni kwamba sitembelei gari sahizi
 
Elimu ya bure..
Kwa gari lako na kwa mazingira ya Tanzania tumia 5w 30,
Ukikosa nenda 10w 30.....
.Anayekuambia hizi oil ni za nchi za baridi amekariri bila kusoma...

Iko hivi..
5w 30 ina uwezo wa kuhimili baridi kali kuanzia -30°C bila kupoteza viscosity yake...pia oil hii ina uwezo wa kuhimili kiwango cha juu cha joto ambacho ni +40 °C bila kupoteza viscosity yake..
Hiki kiwango cha joto nilichotaja ni joto la mazingira unayoishi (outside temperature)

10w 30 ina iwezo wa kufanya vizuri kuanzia joto la -20°C mpaka joto la +40°C...

Hii ina maana kwamba oil 5w30 na 10w 30 zina uwezo wa kusambaa haraka sehemu za injini hata kama gari limewashwa kwenye mazingira ya baridi sana kibongo bongo tunasema Arusha, Iringa, Mbeya na maeneo mengine yenye baridi.
Pia inahimili joto kali kama la Dar, Zanzibar nk.

Kwa hiyo hizi oil zinamudu mazingira yote na ndiyo maana car manufacturers wa siku hizi wana recommend oil hizi zaidi siyo Nissan, Toyota,Honda, Subaru,Mazda n.k...

Ukinunua nunua full synthetic ukikosa ndiyo ununue hizi mineral oil ambazo usivushe 3000 km.

Synthetic unaweza ukaenda km 5000 na zaidi kama umefunga oil filler genuine ndiyo ufanye service nyingine..

Full synthetic inahimili dhoruba ngumu kama milima, matope, joto, baridi, racing bila kupoyeza viscosity yake....na bei yake imesimamia kucha.

Agalia fundi wa mwembeni asikushauri uweke SAE 40 ya kawaida...hii oil ni nzito sana na utakuwa unalitesa gari bila wewe kujua...

Oil ndiyo DAMU ya engine.....zingatia if you love your car.
Mi niwekewa ya 20w50 kwnye ist, matumiz yake ni kwenda ofisini na kurudi nyumbani nipo dar,je ni sawa au ndio wananiulia gari?
 
Back
Top Bottom