Mikhail Tal
JF-Expert Member
- May 12, 2016
- 421
- 778
Wakuu kuna hii gari nimeagiza sasa natafakari ni namna gani ntapata chaguo sahihi la oil ya engine.
Nimejaribu ku google maana mi ist yangu engine yake ni 2NZ sasa majibu ya google yanakuja kama hivi. 5W-30 na 10W-30 kwamba ndo recommended fuel engine kwa engine ya namna hiyo.
Ila katika kupeleleza zaidi kati ya 5W-30 na 10W-30 nikakuta kwamba 5W-10 inatumika kwenye majira ya baridi of which inaweza isiwe chaguo zuri kwangu kwakuwa bongo baridi sio kivile.
Hiyo 10W-30 ndo imekuwa indicated kwamba inatumika zaidi kwenye majira ya joto of which naona kama itaendana na mazingira ya bongo.
NOTE: Kuna hii oil ya 15w40 ambayo nimeona wanaisema kwamba inatumika sana kwenye nchi za tropical ila naiogopa kidogo maana wanasema ipo thicker sana angali mimi cc ya gari yangu ni 1.3l sasa naogopa hiyo oil inaweza isisupport hizo cc.
Hapo hapo nikakuta hizi fuel engine kuna wanaziita synthetic na mineral. Ikionekana synthetic iko reliable kuliko hiyo mineral.
Sasa hapa nlikuwa nauliza itakuwa sahihi kutumia kwenye hii IST fuel yenye hizi specification 10W-30 Synthetic? Na je ni brand gani nzuri kutumia? maana leo nimeenda shell wakanionesha brand ya castrol oil.. Sasa ndugu wazoefu itakuwa sahihi kwa gari langu.
Au nyie wenye IST wengine huwa mnatumia engine fuel ya aina gani?
Ntashukuru kwa majibu.
Sasa hapa najiuliza
BAADHI YA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU
---Mkuu tumia oil kulingana na recommendations ya watengenezaji na oil nzuri kwa gari ambayo haijafikisha km 180000 unashauriwa kutumia 5w30 au umekoswa sana tumia 10w30 basi na kuhusu kampuni hata Toyota wao wana oli zao zilizotengenezwa kwa ajili ya magari yao unaweza kuzipata madukani mfano wa hilo duka ni JO GENUINE SPARE PARTS AND ACCESSORIES lipo Kinondoni.
Vijana barabara ya mwananyamala karibu na meridian hotel fika hapo utashauriwa oil nzuri ila angalizo oil hizo zinakuaga na bei ya juu sana kuliko oil nyingine ile pia kuhusu synthetic na mineral ni aina mbili za oil tofauti na zimetengenezwa kwa material tofauti pia na kuhusu 15w40 Mara nyingi oil hii ni nzito hivyo inashauriwa itumiwe na magari yanayotumia diesel.
---Elimu ya bure..
Kwa gari lako na kwa mazingira ya Tanzania tumia 5w 30,
Ukikosa nenda 10w 30.....
.Anayekuambia hizi oil ni za nchi za baridi amekariri bila kusoma...
Iko hivi..
5w 30 ina uwezo wa kuhimili baridi kali kuanzia -30°C bila kupoteza viscosity yake...pia oil hii ina uwezo wa kuhimili kiwango cha juu cha joto ambacho ni +40 °C bila kupoteza viscosity yake..
Hiki kiwango cha joto nilichotaja ni joto la mazingira unayoishi (outside temperature)
10w 30 ina iwezo wa kufanya vizuri kuanzia joto la -20°C mpaka joto la +40°C...
Hii ina maana kwamba oil 5w30 na 10w 30 zina uwezo wa kusambaa haraka sehemu za injini hata kama gari limewashwa kwenye mazingira ya baridi sana kibongo bongo tunasema Arusha, Iringa, Mbeya na maeneo mengine yenye baridi.
Pia inahimili joto kali kama la Dar, Zanzibar nk.
Kwa hiyo hizi oil zinamudu mazingira yote na ndiyo maana car manufacturers wa siku hizi wana recommend oil hizi zaidi siyo Nissan, Toyota,Honda, Subaru,Mazda n.k...
Ukinunua nunua full synthetic ukikosa ndiyo ununue hizi mineral oil ambazo usivushe 3000 km.
Synthetic unaweza ukaenda km 5000 na zaidi kama umefunga oil filler genuine ndiyo ufanye service nyingine..
Full synthetic inahimili dhoruba ngumu kama milima, matope, joto, baridi, racing bila kupoyeza viscosity yake....na bei yake imesimamia kucha.
Agalia fundi wa mwembeni asikushauri uweke SAE 40 ya kawaida...hii oil ni nzito sana na utakuwa unalitesa gari bila wewe kujua...
Oil ndiyo DAMU ya engine.....zingatia if you love your car.
---Hizi namba kila moja ina tafsiri yake.
Unapokuta mfano 5W 30. Namba ya kwanza kabla ya W inawakilisha uzito wa oil. Kadri namba inavyozidi kuwa ndogo, ndivyo oil inavyozidi kuwa thin hivyo kuwezesha better performance at the cold start.
W simply inawakilisha winter wengine wanasema Weight wengine wanasema Watt...lakini inawakilisha Winter..
30 inawakilisha viscosity ( ile hali ya oil kuwa kama ina nata nata fulani hivi.)
Hii ina maana kwamba injini inpopata joto lake la juu ambalo linatakiwa ili ifanye kazi vizuri, viscosity ya oil hii bado itabaki katika kipimo hicho cha 30 ambacho kimewekwa na watengenezaji, hali kadhalika kwa oil namba 40 au 50
Kwa mantic hii oil 5w 30 ni nyepesi kuliko 10w 30.
Oil hizi zenye namba mbili yaani 5w 30 kwa lugha nyingine zinaitwa multi grade oils....ni oil ambayo imetengenezwa kufanya kazi katika mazingira ya baridi sana na joto sana.
Lakini hizi SAE 40 za kawaida ni mono garde....hizi ni maalumu kwa mazingira ya joto tu...na ndiyo maana kwa siai tulioko huku Arusha ikifika lile baridi la mwezi wa saba, kama gari ni ndogo na umeweka SAE 40, ukiliwasha asubuhi utasikia injini inavuma sana kwa muda mrefu...injini ikishafikia joto kiasi fulani ndiyo unaona inatulia...wakati unasubiri injini ipate moto, unakuwa unasaga vyuma..
Ukifuatilia zamani nchi zenye baridi kama huko Ulaya, walikuwa na oil za aina mbili..nzito kwa ajili ya msimj wa joto na nyepesi kwa ajili ya msimu wa baridi....watu walilazimika kumwaga oil msimu wa bari na kuweka oil nyepesi ya kukabiliana na baridi...hali kadhalika msimu wa joto, walimwaga oil nyepesi na kuweka nzito.
Kuepuka purikushani hizo, ndiyo Society of Automobiles Engineers (SAE) wakaja na oil ambayo ni mult grade mfano 5w30, 10w 30,10w40 n.k....oil hii ukishaiweka haichagui baridi wala joto wewe ni kuangalia tu muda wa service ukifika unaimwaga.
Hatari ya SAE 40 kwa garo dogo, haijalishi unaishi Dar au Arusha.... ukiwasha gari asubuhi wakati injini imepoa, oil hii kitaalam huchelewa kufika sehemu za juu za injini kutokana na uzito wake...pale inapichelewa, vyuma vinaendelea kusagana na unaendelea kuua injini yako taratibu...
SAE 40 ukitumia kwa magari makuu kuu sana haina shida...mfano madaladala au gari ambalo mileage imeenda juu sana pengine zaidi ya 180000km..
---Nenda maduka yanayoeleweka wanayouza spea genuine...
Ukiwapa tu Aina ya gari, model, mwaka na chasis number wanakupa...
Kwa mfano huwa ninafanya hivi
Oil filter-Nissan Note 2005 DBA E-11....
Ukishatoa details kama hizi, utaletewa spea genuine au nyingine ambayo ni compatible lakini imependekezwa na muundaji wa gari...
Pia huwa zina nembo ya kampuni husika mfano Toyota, Nissan n.k..
Feki nyingi hazina majina ya Kampuni ya gari.
Maduka ya makanjanja ukiwapa hizo details, watabaki wanakushangaa kisha watakuambia hatuna au nenda ulete sample ya spare...
Lakini kama ni mzoefu hata bei inaongea...
Genuine kwa hizi gari ndogo ndogo inaazia 15000/ npaka 20000/
Kanjanja atakupa ile ya elfu 4 anakuambia ni genuine...
Fundi haruhusiwi kukuambia kuhusu oil yeye kazi yake ni kumwaga oil na kukukabidh gari yako na tambua engine ya gari ndio gari yenyewe tusiwasingizie mafundi hata sisi wahusika ndio chanzo oil ya sae40 ni oil cheap sana kuliko oil zozote zile sasa wewe ukifika dukani ukiambiwa 5w30 au 5w40 na 10w30 au 10w40 ni 65-80 kwa dumu la Lita 4/5 unaona kuwa unapigwa wakati sae 40 inauzwa 40 unaona y nisumbuke na cha garama wakati cheap ipo lkn kumbuka hivyo unaiua engine yako taratibu taratibu ushauri wangu kwa wenye magari mpendelee kusoma manual za magari yenu kuhusiana na aina ya oil
Pia mpende kupokea ushauri kwa sisi wauza oil kuna baadhi ya vitu tunafundishwa kuhusu kumpa mteja oil sahihi kulingana na oil sahihi na ukifika dukani kwangu kitu cha kwanza nakuuliza gari inaitwaje na imetengenezwa mwaka gani ili nikupe oil iliyo sahihi na yenye API inayoendana na mwaka wa gari mwisho karibuni sana JO GENUINE SPARE PARTS AND ACCESSORIES tupo Kinondoni vijana karibu na meridian hotel upate oil sahihi kwa gari yako +255762263074/+255719263074