Enyi Manabii wa kizazi kipya ni kweli mmepewa nguvu na Mwenyezi Mungu, au ni ushirikina tu?

Vitabu hutungwa na kuandikwa na watu, kwaio uwepo wa stori za kwenye vitabu si uthibitisho mungu yupo, hizo ni stori kama stori zingine za kufikirika.Mbaya zaidi vitabu vyenyewe havipo consistency ni full contradiction. Mkuu mungu angekuwepo hata hizi thread za kumjadili zisingewezekana kuwepo kwa namna yoyote.
 
Mtu anabinywa tumbo kama anakanda chapati..utaacha kutapika dagaa kweli?.ila kwny screen wanaonyesha kono kono...hahahah

😄😀😀, hao ni manabii walio vaa ngozi ya kondoo. Lakini wanatumia mazingaombwe.
 
Mungu angekuwepo, kila mtu angemjua bila utata.

Ukishaona Mungu anaanza kuelezewa, kuhubiriwa, kutangazwa, ujue hizo ni siasa na hadithi za watu tu.
 
Moderators badilisheni kichwa cha habari kiwe :

Enyi Manabii wa kizazi kipya ni kweli mmepewa nguvu na Mnyaazi Mungu, au ni ushirikina tu?​

 
Kumuaminisha mtu kuwa kuna Mungu halafu yeye na misingi yake hairuhusu kuamini kuhusu Mungu ni jambo gumu sana tena sana ....ni Bora ubaki na unacho kiamini kaka
Siongelei imani tu hapa, naongelea ukweli unaoweza kupimwa kimantiki.

Wewe unaelewa hata tofauti kati ya viwili hivyo?
 
Hao matapeli kwa kivuli cha unabii wakikutapeli huna tofauti na wanaotapeliwa na Yahoo boys.
 
Wakiristo jamani JITOKEZENI kuchangia Mwl. Francis Ndacha kumuwezeshe ahudhurie Mdahalo na Waislam hapa Dar tarehe 16 na 17 December 2023 katika ukumbi wa PTA SABA SABA. Mchango wako wa fedha upeleke kwa Bw Jaffari Massawe muwakilishi wake hapa Tanzania kwa namba +255757722557


View: https://www.youtube.com/live/xg7IQgi2W-E?si=SypOSE5vlRzCHWEV
 
akainama

Nani akainama? Binadamu? Embu soma hiyo sentensi vzuri, nalimngoja bwana kwa saburi; akainama.
Zaburi 40:1, maneno "akainama" yanarejelea Mungu. Hapa, "Nalimngoja Bwana kwa saburi; akainama, akaisikia kilio changu" inamaanisha kwamba mwombaji (mwenye kusali) amekuwa akimngojea Mungu kwa uvumilivu na subira, na Mungu, kwa fadhili na huruma, anajitokeza kusikiliza kilio chake. Hii inaonyesha uhusiano wa karibu kati ya mwombaji na Mungu, ambapo sala inajibiwa kwa huruma na upendo wa Mungu.,,,.. Kidogo utakua umenielewa hapo.
 
Kwa hiyo mkuu, imani yako inasema mungu hayupo, je kama hayupo umeangalia nini ukaona mungu hayupo?? 🤔🤔.
 
Moderators badilisheni kichwa cha habari kiwe :

Enyi Manabii wa kizazi kipya ni kweli mmepewa nguvu na Mnyaazi Mungu, au ni ushirikina tu?​

Mnyaazi inamaana gani mkuu??
 
Hapo ndo nilipopata,
Mungu aliniinama kutoka wapi?
 
😄😄, Tupe stori kidogo kuhusu yahoo Boys, ina maana gani.
Ni matapeli wa kimtandao wengi wakiwa ni raia wa Nigeria.

Walikuwa wanatumia account fake za yahoo zenye majina mbali mbali kutapeli watu kwa mtandao huo.
 
Hapo ndo nilipopata,
Mungu aliniinama kutoka wapi?
• Jamii ya Waebrania katika Agano la Kale. Zaburi zina utajiri wa hisia, sala, sifa, na maombi, zikiwa zimetungwa na watu kama Daudi, Asafu, Heman, na wengine.

• Dini za Ukristo, Uislamu, na Uyahudi, Mungu ni mtungaji wa ulimwengu, Muumba, na kiumbe cha kiroho bali si binadamu.

•Sasa kutokana na maelezo hapo juu, "akainama" katika muktadha wa Zaburi 40:1 hayatafsiriwi moja kwa moja kama kitendo cha kimwili cha Mungu kuinama. Badala yake, hii ni taswira au lugha ya kiroho inayoelezea huruma na kusikiliza kwa upendo wa Mungu kuelekea wale wanaomngojea kwa subira
 
Shida sio wa Sasa wewe hata Hawa manabii wazamani unasema walitumwa kweli na Mungu we una uhakika gani na ushahidi Gani... kingine huyo Mungu cjui roho mtakatifu si yupo kila mahali kwa Nini Mungu ategemee mtu kufikisha ujumbe wake...yaani Leo hii naweza amka nikasema nimetumwa na Mungu nikafanya mazingaombwe mawili matatu tayari mi nabii...hizi dini ndo maana kila mtu anakuja na yake coz ni rahisi Sana kudanganya wapuuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…