Enyi Manabii wa kizazi kipya ni kweli mmepewa nguvu na Mwenyezi Mungu, au ni ushirikina tu?

Enyi Manabii wa kizazi kipya ni kweli mmepewa nguvu na Mwenyezi Mungu, au ni ushirikina tu?

• Mkuu mungu yupo, ukipitia pitia baadhi ya vitabu, Biblia : Kitabu kitakatifu cha Ukristo kinachojumuisha Agano la Kale na Agano Jipya.

• Qur'an : Kitabu kitakatifu cha Uislamu.

• Vedas : Maandiko matakatifu ya Uhindu, ambayo ni pamoja na Rigveda, Samaveda, Yajurveda, na Atharvaveda.

• Tanakh : Maandiko matakatifu ya Uyahudi, ambayo ni pamoja na Torati, Nabi, na Maandiko


• Mojawapo ya mistari inayojulikana ni mwanzo wa Biblia, katika Kitabu cha Mwanzo, sura ya 1, ambapo inaanza na maneno "Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi."

• Pia, Yesu Kristo katika Agano Jipya anazungumza mara kwa mara kuhusu Baba yake wa mbinguni na kutoa mafundisho kuhusu ufalme wa Mungu.


• Hata ukiangalia jaribio la Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni. Wanajaribiwa kutii amri ya Mungu ya kutokula tunda fulani, lakini wanashindwa na kutokea madhara.

• Katika Agano Jipya, Yesu mwenyewe anapitia majaribu. Mathayo 4:1-11 na Luka 4:1-13 zinatoa maelezo ya majaribu ambayo Yesu alikutana nayo jangwani baada ya kufunga kwa siku 40. Katika kila jaribio, Yesu anapinga majaribu ya Shetani kwa kutumia Maandiko.
Vitabu hutungwa na kuandikwa na watu, kwaio uwepo wa stori za kwenye vitabu si uthibitisho mungu yupo, hizo ni stori kama stori zingine za kufikirika.Mbaya zaidi vitabu vyenyewe havipo consistency ni full contradiction. Mkuu mungu angekuwepo hata hizi thread za kumjadili zisingewezekana kuwepo kwa namna yoyote.
 
Mtu anabinywa tumbo kama anakanda chapati..utaacha kutapika dagaa kweli?.ila kwny screen wanaonyesha kono kono...hahahah

😄😀😀, hao ni manabii walio vaa ngozi ya kondoo. Lakini wanatumia mazingaombwe.
 
Nina imani mda wako hautoshi wa kumjua mungu, inaelezwa kwamba mitume walikuwa karibu na Yesu wakati wa huduma yake duniani, wakishuhudia miujiza, kusikia mafundisho yake, na kushiriki katika huduma yake. Lakini hawakufanikiwa kumjua mungu vilivyo. Na baadhi yao walipokea mafunuo maalum kutoka kwa Roho Mtakatifu baada ya Pentekoste.
Mungu angekuwepo, kila mtu angemjua bila utata.

Ukishaona Mungu anaanza kuelezewa, kuhubiriwa, kutangazwa, ujue hizo ni siasa na hadithi za watu tu.
 
Moderators badilisheni kichwa cha habari kiwe :

Enyi Manabii wa kizazi kipya ni kweli mmepewa nguvu na Mnyaazi Mungu, au ni ushirikina tu?​

 
Kumuaminisha mtu kuwa kuna Mungu halafu yeye na misingi yake hairuhusu kuamini kuhusu Mungu ni jambo gumu sana tena sana ....ni Bora ubaki na unacho kiamini kaka
Siongelei imani tu hapa, naongelea ukweli unaoweza kupimwa kimantiki.

Wewe unaelewa hata tofauti kati ya viwili hivyo?
 
Hao matapeli kwa kivuli cha unabii wakikutapeli huna tofauti na wanaotapeliwa na Yahoo boys.
 
Nyinyi manabii mnao vaa visuluali vimebana, manabii mmesuka rasta, manabii mnawapiga mateke wagonjwa, manabii mnawalisha majani waumini, manabii mnawanywesha mafuta ya taa waumini, manabii mnataka sadaka kuazia elfu Tsh 30,000 na kuendelea, je ni kweli hizo nguvu/mamlaka mmepewa na Mwenyezi mungu?? 🤔🤔

"Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo watafanya miujiza mikubwa na maajabu ili kuwapoteza, kama ingewezekana, hata wateule."

Manabii ni watu wanaoaminiwa kuwa na uwezo wa kupokea ujumbe au mwongozo kutoka kwa nguvu za kimungu, Katika muktadha wa dini mbalimbali, manabii mara nyingi wanachukuliwa kama watu wanaotekeleza mapenzi ya mungu au nguvu za juu. Wanaweza kutabiri mambo ya baadaye, kutoa mafundisho ya kiroho.

Muktadha wa manabii unaweza kutofautiana kulingana na dini na imani. Kwa mfano, katika Ukristo, manabii wanaweza kutazamwa kama wale waliotumiwa na Mungu kutoa ujumbe wa kimungu. Yesu Kristo mwenyewe anachukuliwa na Wakristo wengi kama Mwana wa Mungu na Mtume wa mwisho.

Hata hivyo, mifumo mingine ya imani inaweza kuwa na maoni tofauti kuhusu manabii na uhusiano wao na nguvu za kimungu.

Katika imani ya Kikristo, manabii wanachukuliwa kuwa watu ambao Mungu aliwatumia kutoa ujumbe wake kwa binadamu. Manabii wa Agano la Kale, kama vile :- Isaya, Yeremia, Adamu, Nuhu, Abrahamu, Musa, Miriamu (dada ya Musa), Haruni, Debora, Samweli, Nathani, Eliya, Elisha
, Yona, Amosi, Hosea, Isaya, Mika, Nahumu, Habakuki, Zefania, Haggai, Zakaria na Malaki , wanachukuliwa kuwa wawakilishi wa Mungu waliotabiri mambo ya baadaye na kutoa maonyo na mafundisho. Hapa ni baadhi ya manabii na kazi zao walizo zifanya:-

• Musa: Alipelekwa na Mungu kuwaongoza Waisraeli kutoka utumwani.

• Eliya: Mmoja wa manabii wakubwa wa Kiyahudi, aliyefanya miujiza mingi.

• Isaya: Alikuwa nabii wa wakati wa Ufalme wa Yuda na aliandika kitabu cha Isaya.

• Yeremia: Alionywa kuhusu uharibifu wa Yerusalemu na utumwa wa Waisraeli.

• Ezekieli: Nabii wa kipindi cha utumwa Babeli, aliyeandika kitabu cha Ezekieli.

• Danieli: Alikuwa nabii katika utawala wa Babeli, na aliwekwa katika mazingira ya kifalme.

• Hosea: Alikuwa nabii wa Israeli na alionya juu ya unafiki wa kidini.

• Yoeli: Alitoa unabii kuhusu siku ya Bwana na mwisho wa nyakati.

• Amosi: Alikuwa mkulima na mchungaji, nabii wa haki na hukumu.

• Obadia: Alikuwa nabii mfupi, akitabiri juu ya hukumu ya Edomu.

• Mika: Alikuwa nabii wa haki na alihoji dhuluma na udanganyifu.

• Nahumu: Alikuwa nabii wa hukumu dhidi ya Ninawi.

• Habakuki: Alisimulia mazungumzo yake na Mungu na kuuliza maswali.

• Sefania: Alikuwa nabii wa hukumu na toba kwa watu wa Yuda.

• Yohana Mbatizaji: Alijitokeza kama mtangulizi wa Yesu Kristo na alibatiza watu kwa kutumia ubatizo wa toba. Kuhusiana na Yesu Kristo, yeye mwenyewe anachukuliwa kama Mwana wa Mungu na kama mwisho wa unabii.

Biblia inaonya kuhusu uwepo wa manabii wa uongo. Katika Agano Jipya, hasa katika kitabu cha Mathayo, sura ya 24, Yesu anatoa unabii wake wa mwisho, na miongoni mwa mambo aliyotabiri ni kuja kwa manabii wa uongo. Mathayo 24:24 (NIV) inasema:

"Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo watafanya miujiza mikubwa na maajabu ili kuwapoteza, kama ingewezekana, hata wateule."

Hapa, Yesu anawaonya wafuasi wake kuhusu hatari ya kupotoshwa na manabii wa uongo watakaofanya miujiza ili kuwapotosha watu.

Mimi kama Nyafwili Nasema ni muhimu kuwa macho na kuwa na busara katika kufuatilia ujumbe wa kiroho.... ✍️✍️✍️
Wakiristo jamani JITOKEZENI kuchangia Mwl. Francis Ndacha kumuwezeshe ahudhurie Mdahalo na Waislam hapa Dar tarehe 16 na 17 December 2023 katika ukumbi wa PTA SABA SABA. Mchango wako wa fedha upeleke kwa Bw Jaffari Massawe muwakilishi wake hapa Tanzania kwa namba +255757722557


View: https://www.youtube.com/live/xg7IQgi2W-E?si=SypOSE5vlRzCHWEV
 
akainama

Nani akainama? Binadamu? Embu soma hiyo sentensi vzuri, nalimngoja bwana kwa saburi; akainama.
Zaburi 40:1, maneno "akainama" yanarejelea Mungu. Hapa, "Nalimngoja Bwana kwa saburi; akainama, akaisikia kilio changu" inamaanisha kwamba mwombaji (mwenye kusali) amekuwa akimngojea Mungu kwa uvumilivu na subira, na Mungu, kwa fadhili na huruma, anajitokeza kusikiliza kilio chake. Hii inaonyesha uhusiano wa karibu kati ya mwombaji na Mungu, ambapo sala inajibiwa kwa huruma na upendo wa Mungu.,,,.. Kidogo utakua umenielewa hapo.
 
Vitabu hutungwa na kuandikwa na watu, kwaio uwepo wa stori za kwenye vitabu si uthibitisho mungu yupo, hizo ni stori kama stori zingine za kufikirika.Mbaya zaidi vitabu vyenyewe havipo consistency ni full contradiction. Mkuu mungu angekuwepo hata hizi thread za kumjadili zisingewezekana kuwepo kwa namna yoyote.
Kwa hiyo mkuu, imani yako inasema mungu hayupo, je kama hayupo umeangalia nini ukaona mungu hayupo?? 🤔🤔.
 
Zaburi 40:1, maneno "akainama" yanarejelea Mungu. Hapa, "Nalimngoja Bwana kwa saburi; akainama, akaisikia kilio changu" inamaanisha kwamba mwombaji (mwenye kusali) amekuwa akimngojea Mungu kwa uvumilivu na subira, na Mungu, kwa fadhili na huruma, anajitokeza kusikiliza kilio chake. Hii inaonyesha uhusiano wa karibu kati ya mwombaji na Mungu, ambapo sala inajibiwa kwa huruma na upendo wa Mungu.,,,.. Kidogo utakua umenielewa hapo.
Hapo ndo nilipopata,
Mungu aliniinama kutoka wapi?
 
😄😄, Tupe stori kidogo kuhusu yahoo Boys, ina maana gani.
Ni matapeli wa kimtandao wengi wakiwa ni raia wa Nigeria.

Walikuwa wanatumia account fake za yahoo zenye majina mbali mbali kutapeli watu kwa mtandao huo.
 
Hapo ndo nilipopata,
Mungu aliniinama kutoka wapi?
• Jamii ya Waebrania katika Agano la Kale. Zaburi zina utajiri wa hisia, sala, sifa, na maombi, zikiwa zimetungwa na watu kama Daudi, Asafu, Heman, na wengine.

• Dini za Ukristo, Uislamu, na Uyahudi, Mungu ni mtungaji wa ulimwengu, Muumba, na kiumbe cha kiroho bali si binadamu.

•Sasa kutokana na maelezo hapo juu, "akainama" katika muktadha wa Zaburi 40:1 hayatafsiriwi moja kwa moja kama kitendo cha kimwili cha Mungu kuinama. Badala yake, hii ni taswira au lugha ya kiroho inayoelezea huruma na kusikiliza kwa upendo wa Mungu kuelekea wale wanaomngojea kwa subira
 
Mipango ya Mungu, Katika imani nyingi, kuwa manabii wa zamani walihusishwa na mpango wa Mungu na sio uchaguzi wa kibinadamu. Ni wachache wanaitwa kwa kazi hii kulingana na mpango wa Mungu...

Lakini hawa manabii wa sasa, nina mashaka nao, Maana hawaendani na uhalisia wa zamani...
Shida sio wa Sasa wewe hata Hawa manabii wazamani unasema walitumwa kweli na Mungu we una uhakika gani na ushahidi Gani... kingine huyo Mungu cjui roho mtakatifu si yupo kila mahali kwa Nini Mungu ategemee mtu kufikisha ujumbe wake...yaani Leo hii naweza amka nikasema nimetumwa na Mungu nikafanya mazingaombwe mawili matatu tayari mi nabii...hizi dini ndo maana kila mtu anakuja na yake coz ni rahisi Sana kudanganya wapuuzi
 
Back
Top Bottom