Enyi Manabii wa kizazi kipya ni kweli mmepewa nguvu na Mwenyezi Mungu, au ni ushirikina tu?

Enyi Manabii wa kizazi kipya ni kweli mmepewa nguvu na Mwenyezi Mungu, au ni ushirikina tu?

Yupo na ukitaka kuthibitisha, tenga muda wako japo mchache na omba kwa imani unayoamini wewe kuwa naomba nipe ishara fulani niamini uwepo wako

Kisha subiria, jibu litakuja kwa wakati wake, inaweza isiwe leo kesho au hata baadae ila jua tu litakuja na utakumbuka ombi lako ndipo utakiri na kusadiki.
Kitendo cha kufikia haja ya kuomba chochote nacho ni uthibitisho Mungu hayupo.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote, na upendo wote, angekuwepo, angemkamilishia kila kiumbe mahitaji yake kabla ya kuombwa.

Mungu huyo si mchoyo, ni mwingi wa rehema, ana utajiri wote, ana uwezo wote, ana upendo wote, hana sababu ya kutomkamilishia kila kiumbe cho chote anachotaka ambacho ni kizuri, na kila kibaya akafanya kisiwepo na kisiweze hata kufikirika.

Ukiona kuna haja ya kumuomba Mungu chochote kile, ujue huo ni uthibitisho Mungu huyu hayupo.

Angekuwepo angekukamilishia haja zako kabla hujafikiria kuomba na usingekuwa na haja ya kuomba.
 
Katika muktadha wa dini za Abrahamiki (Uyahudi, Ukristo, na Uislamu), vitabu vitakatifu kama vile Biblia na Qur'an ni vyanzo vikuu vya mafundisho kuhusu Mungu
Vitabu hivyo vina mikanganyiko ya kimantiki inayoonesha Mungu hayupo, mikanganyiko hiyo ya kimantiki inatuonesha kwamba Mungu huyo katungwa na watu tu, nje ya hadithi za watu hayupo.
 
Angalau mimi nipo kwa kuonekana, kushikika na kusikika.

Mungu huyo Hayupo kwa namna yoyote ile zaidi ya mawazo ya kufikirika tu, imagination just an illusion.

Mungu hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
Kama unasubiria umuone Mungu akikatiza mtaani utapata tabu sana...

Mungu ni Roho, hivyo ukitaka kumuona lazima uombe Roho Mtakatifu akupe macho ya Rohoni...

Hakuna Raha kama kumjua Mungu, unapata uwezo wa kujua mambo yajayo...

Unapiganiwa, unaona aisee!

Bwana Yesu Kristo atukuzwe
 
Kwanini mkuu?

Mbona kuna ambao ni Manabii na wana karama za kuhubiri...

Kuna watu wamepewa karama zaidi ya moja na Mungu.

Ukisoma vizuri Biblia utaona kuwa nabii ni mtu mwenye jukumu la kupitisha taarifa tu kwa wanadamu na mpeleka taarifa za wanadamu kwa Mungu...

Pia ni mtu aliyewekwa wakfu na Mungu mwenyewe kwa ajli ya kupatanisha watu na Mungu wao...

Hesabu 12
6 Kisha akawaambia,Sikizeni basi maneno yangu;Akiwapo nabii kati yenu,Mimi,Bwana,nitajifunua kwake katika maono,Nitasema naye katika ndoto.

Jaribu kutazama namna ambavyo Musa, Daniel, Eliya, Elisha, Samuel, Yohana Mbatizaji n.k, hawa hawakuwa wakiongoza watu wala kuwa na wafuasi kwa namna ya kusanyiko la kiibada kama kanisa au hekalu au sinagogi...

Nitaandika zaidi nipo mzigoni
 
Yupo na ukitaka kuthibitisha, tenga muda wako japo mchache na omba kwa imani unayoamini wewe kuwa naomba nipe ishara fulani niamini uwepo wako

Kisha subiria, jibu litakuja kwa wakati wake, inaweza isiwe leo kesho au hata baadae ila jua tu litakuja na utakumbuka ombi lako ndipo utakiri na kusadiki.
Ameni, je kuna haja yeyote ya kanisani kwa sasa, au hata inatosha kusali/kuswali?
 
Kama unasubiria umuone Mungu akikatiza mtaani utapata tabu sana...

Mungu ni Roho, hivyo ukitaka kumuona lazima uombe Roho Mtakatifu akupe macho ya Rohoni...

Hakuna Raha kama kumjua Mungu, unapata uwezo wa kujua mambo yajayo...

Unapiganiwa, unaona aisee!

Bwana Yesu Kristo atukuzwe
Roho ni nini?

Vyote hivyo ni nadharia za kufikirika tu.
 
11 Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi.
12 Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa.
13 Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
14 Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja. [Mathew 24:11-14].
Hawa manabii waabudu mashetani watakokota wengi kuzimu. Pasipo maarifa, kuangamia ni 100%.Maranatha
Kwa nini mungu alitupa huu mtego, au anatamani hapo baadae aje atengeneze kizazi kingine, tofauti na hichi kilichopo?? 🤔🤔
 
Jinga!
Hakuna Mungu sukari kwenye muwa na nanasi aliweka babayenu? Watu hamna fadhila mmbwa nyie!! [emoji32][emoji32]
Mchakato wa sukari kwenye miwa na matunda ulishaelezwa apa kitambo, nyie ndio wale sayansi darasa la sita mlikua mnasinzia mkishtushwa na swali mnakurupuka " sikulamba sukari".
 
Manabii wa uongo wapo na wa kweli wapo...

Kazi ipo kwako wewe ambaye unaongozwa na mwili na kukariri neno bila kulifanyia kazi...

Wanaoongozwa na Roho Mtakatifu wanajua Nabii wa kweli na wa uongo...
Mkuu, Kitabu cha Biblia kinasema, nabii wa mwisho kwa upande wa kikatoliki ni yesu, na Mungu bado hajatuma nabii yeyote yule, je hao manabii wengine wamekuja kwa njia ipi??
 
Back
Top Bottom