Enyi wanawake acheni ligi na wanaume mtaumia

Enyi wanawake acheni ligi na wanaume mtaumia

Nipo zangu eneo langu la biashara... Ni kasoko flani hivi kalikochangamka kwahiyo nikaona niwe na kastationary pale kakuzugia, mambo yote ya photocopy, printing, scanning, binding na kuchapa chapa material nini unapata na huduma ya passport size zile za fasta dakika 3 pia zipo fresh tu.

Mwezi uliopita kulitokea kutokuelewana kati yangu na mwenye frem pale mzozo ukawa mkubwa kiasi cha kurushiana ngumi. Ebwana yule mwenye frem kipigo kikamzidi akakimbilia frem ya jirani ambayo ni saluni ya kike ya sistaduu mmoja anamdomo balaa na hatuivi hata kidogo... nikamfata jamaa huko huko... Kichapo kikaendelea.

Ile vuta nikuvute vuta nikuvute nikamlima jamaa bonge la buti jamaa chini.. yule dada na wateja wako ... Bwana tokenii mpiganie hukooo hatutaki magomvi... Sasa ile namvuta jamaa twende nje mchiz alinirukia kichwa kimoja hivi matata. Kumbe alikuwa ananivizia bana... Nikaenda kugonda dryer kubwa la yule dada nikadondoka nalo mpaka chini mzee likaasukaa. Na huyu dada hatuiviiiiii.. yani elewa maana ya hatuivii.

Aaaaa bibie akapata stata. Hilo draya nimenunua 220,000 nalihitaji kama lilivyo aisee ukawa mzozo mkubwa nikamuomba msamaa nilipe nusu ilikuwa bahat mbaya na wadau wakawa wanamsihi nilipe nusu yani 110,000 ooohooo bibie yuko wapii? Ashachukua boda kaenda polisi fasta.. mazee akasema pamoja na usumbufu niliomfanyia ofisini kwake nilipe 300,000 nikajiumauma palee mwisho nikatoa yakaisha. Ila moyoni nikawa nakinyongo kisicho na mfano...

Hiyo ni mwezi uliopita mwanzoni. Mungu si zakayo aisee naye jana si kayatimbaa.

Kuna kadem ni kafanyakazi kangu nakaachaga ofisini sasa huyu sista duu si hatuivi! Nisipokuwepo kumbe anaingiaga ofisini kwangu kupiga stori na yule mfanyakazi wangu, sasa kutokana na tatizo la umeme pale nina kajenereta kangu kadogo kwa ajili ya emergency ya umeme ikitokea umekatika kazi zisisimame.

Sasa nikawa nimeacha chaji sim yangu ofisini pale aina ya SAMSUNG GALAXY S23 ULTRA ya Tsh 2,500,000/= na risiti ninayo.

Kumbe wakati sipo kaingia kupiga stori akaanza kuishikashika sim yangu ananiangalia.. aisee Mungu akiwa upande wako yuko kwako tu. Si akaitwa na wenzie fasta ofisini kwake akasikilize mteja! Katoka mbio na sim yangu akajisahau kakaa nayo huko mtoto wako anatambaa kaishika kaitia kwenye ndoo ya maji kuoshea nywele ikakaa humo zaidi ya lisaa.

Narudi moyo unadunda sim yangu iko wapi? Ndo yule mfanyakazi wangu akaniambia alikuwa nayo ashura (yule sista duu) nikasema whaaaaaaaaaat??? Ashura kuulizwa akaanza kuitafuta ndo mteja wake mmoja akasema aliishika mwanao hapa.. ebwana baada ya kuitafuta weee tukaikuta kwenye ndoo ya maji... kuiwasha hauwakiiii... inavuja maji kama kuitambaa kimelowekwa vile.

Nikasema Asante Mungu nimempata kwenye anga zangu huyu, kwanza bibie kidogo azimie.

Nilichokifanya nikaenda hom nikaja na risiti ya simu inasoma Tsh 2,500,000/= akaanza kulia pale wenzake wanamuombea msamaha, nilitoa kauli moja tu...

"Hiyo simu nakuachia baki nayo naitaka ikiwa mpyaa nafikiri bei yake umeiona kwenye risiti hapo"

Bibie akajifanya kizimia hapo watu kibao wanamuombea msamaha nikawakumbusha tukio langu alilinifanyia watu kimyaaa.

Wakiwa wenzake wanampepea aamke mimi fastaa kituoni... Baada ya saa moja nikampgia jirani yangu mwngine wa frem pale kwamba waambie wamlete huyo atazindukia huku. Dem akaja kashikiliwa huku na huku na weupe ule uso umekuwa mwekunduuu kwa kulia.. nikajisemea moyoni na "badooo... hili ni tela tu"

Nikaunganisha kesi kama yeye nikamwambia polisi kaingia ofisini kwangu wakati sipo akabeba simu. Kwanini abebe kitu sio chake tena kwenye ofisi ya watu? Pamoja na usumbufu wa kuingia ofisini kwangu bila ruhusa siwezi kujua kachukua nini kingine, Kwa hiyo kwenye hiyo 2,500,000 ya simu aongeze 500,000 ya usumbufu jumla iwe 3,000,000/=

Dem akaanza kulia tena kwa kwikwi nyungiiii.. mimi waalaaaaa.... Tena naona kama ananicheka kwanza.

Hivi tunavyoongea saluni yake tumefunga na vitu vyote vikiwa ndani na polisi wakiwepo...

Aisee kumbe saluni za kike zina gharama aisee.. Kwa hesabu niliyopiga harakat harakat hii ofisi yeke inalipa simu na gharama zangu zotee na machenji juu.

Halafu nilichofurahisha zaidi kumbe hela za kufungulia ile saluni alikopa mkopo BLACK kwa wahindi.

Hata sijui namba yangu kaitoa wapi.. anapiga simu balaa kuomba msamaha namsikiliza weeeeee siongei kitu alafu nakata simuu

Nafikiri hapo nimecheza kama Pele wazee mpaka alipe.. hapa ligi ligi tu si wanataka haki sawa?
Sawa alikosea, sema huko nyumbani mkeo si hua unamsusia hadi mdudu maan 😂😂😂
 
Kwa namna yoyote ile epuka ugomvi wa aina yoyote na jirani yako,, nyuma ya hizi biashara kuna mambo mengi mno ambayo najua yako juu ya uwezo wako... Hivo visasi sio vizuri katika maisha
Wanawake wote leo mpo nyuma ya mwenzenu.
Sisi Maustaz tunasema Al Qiswas Haq yaani kisasi ni haki yako. Japo kusamehe ni bora zaidi.
Mtoa mada shikilia hapo hapo, usilegeze.
 
Yaani Unamsichana Dukani aache mtu mgeni aingie dukani aanze kuchezea simu ya Bosi wake/ hadi kuondoka naye na yeye yupo?
Lakininpia, unamiliki simu ya Samsung Galaxy 23 - ambayo haina password? na maanisha kama ingekuwa na password angechukua ya nini?
Kuna maswali mengi tu kwa hii hadithi yako.....
 
Mkuu mademu wanaroho mbaya,ww mwenyewe ukasome.Kifupi tumia busara upate haki yako salama
 
Huwajuwi wanawake, usidhani umeshinda.

Anakuweka deka huyo.

Huwezi kushindana nan
kiumbe kilichokuweka tumboni miezi na miezi na kikakuchambisha kwa vidole.
Tuliza mishono wewee na kauli zennu za kujipa moyo eti miezi tisa sasa ulitaka nikae minne ama? Yeye Kwa mamaake alikaa mitano au? Kama anaweza hii ligi aendelee.
 
Na ole wako umsamehe sitakuelewa hata kidogo. Namaanisha sitakuelewa hata
 
Tuliza mishono wewee na kauli zennu za kujipa moyo eti miezi tisa sasa ulitaka nikae minne ama? Yeye Kwa mamaake alikaa mitano au? Kama anaweza hii ligi aendelee.
Miezi tisa ni kitu gani hizi pumbu zilizotoa mbegu tupo nazo maisha yote wewe unaongellea miezi tisa. Stupid kabisa
 
Huhitaji kumlipa mtu mjinga kwa ujinga wake chief. Ungemuonyesha wewe ni Smart Zaid yake kwa kumsamehe angejifunza kitu. Life is full of experience mkuu. Kila tunajifunza kitu.
Kwa mapepe na mdomo alionao sio mtu wa kujifunza Kwa makosa inabidi afundishwe kwa vitendo mujarab kama hivi
 
Nakupongeza mno kwa hili.

NONGWA na GUBU is inevitable when the situation is alarming.

Mimi mwenyewe huwa nikilianzisha varangati nahakikisha nakufanyia NONGWA na GUBU kweRi kweRi mpaka unaomba poo au unaomba KUJIUZULU bila mafao.

cc Lamomy Extrovert
 
Back
Top Bottom