Enzi zako zimekwisha P FUNK pole sana

Status
Not open for further replies.

kila mtu atakua juu kwenye sekta yake. p funk alikuwepo kabla ya clouds wafu. na bado anadunda. juzi amewapa makonde leaders club na kuwashutumu ushoga aibu aibu badala yake mkaomba msamaha mpige naye picha. mia
 

Pfunk huyu huyu aliyefulia na kuishi kwa mama yake ugali shkamoo au amezaliwa mwingine? kama ni huyu huyu wa mabange tutasubiri sana kuiona hiyo studio na redio. Labda kama ni mwingine amabaye majina yamefanana
 
Hivi kuna producer wa hiphop East and Central Africa level za P Funk?
Naomba mnitajie mmoja tu! P Funk alikuwa DJ kabla ya kuwa producer kama inavyokuwa kwa maproducer nguli wa hiphop.
Sikiliza cheza kidogo ya Jay Mo usikie alivyosugua santuri wengine wanatumia effects za computer tu.
Pamoja na mapungufu yake kama binadamu jamaa ni kichwa.
 
Mi Naona unajitangaza tu,. Kaka p.funk harekodi watu wasiojua ilimradi tu apate pesa kama. Wafanyavyo mengine. Yeye anachagua wenye vipaji,. Kama huna kipaji hakubebi,. Na kumbuka pia, wenye vipaji kama pig black walirekodiwa Nyimbo hata bure,. Alikutosa kwakuwa hakuona kipya,. Usimlaumu
 
Asante kaka,. Wanataka kusema mensen selekta ndo mkali kuliko p.funk kisa ana tuzo? Au ni maneke mzee wa ku-sample? Mako chali mpiga viduku,. Lamar beat moja.. wanasahau p.funk ndo ameweka foundation ya beat za bongo flavour,. Yeye ndiyo ameidefine bongo flavour,. Yeye ndiyo aliyetengeneza miziki ambayo wazazi wetu walielewa bongo fleva cyo uhuni na kuturuhusu kuwasha radio sebleni,. P.funk mpaka sasa hana mpinzani Kwani hakuna producer aliyeaccomplish makubwa kama Yeye,. Ni sound engineer mzuri na msije mkasema na ludigo kaisha Maana nitawashangaa zaidi..
 

Aaaaah babu!ebu acha zako bwana! Yan badala uachie wajukuu akina diamond na wewe unataka ukirudi uachie ngoma???????!
Yan naimagine kama p funk ni dogo kwako we utakuwa kama nani?!!labda mzee gurumo,kitime hivi!
Pumzika bwana umri umesogea huo,cheza cheza na wajukuu tu!

Aaah samahani nlisahau, SHKAMOO

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 

wewe utakuwa mmoj wa hao kina clouds jinsi tu unavoongea..
 
Baada ya lady Jaydee sasa mmehamia kwa P-funk??!!

Tatizo la clouds hawapendi kukosolewa, nyie vibaraka wa clouds nijibuni-DJ Venture wa clouds alikuwa Manager wa Mangweha,album ya a.k.a Mimi walimpa pesa isiyozidi million 3 na gari ambayo alikija kupokonywa kwani ilikua haijalipiwa,je ni haki????!!!

P-funk kamrecodia Madilu System Mamuu remix,kamuuzia beat Chameleon,Kamuuzia beat Whine Wonder,kamtengenezea beat Mims, who else than Majani aliefanya japo robo tu ya hayo??!!

Maproducers wa leo sio wabunifu na ubora ni sifuri kwa wengi sema wanabebwa tu kuwapoteza wakongwe,Maku Chali alianza kumkopi P,Lamar kafundishwa na P,mpeni Majani heshima yake,au hadi nae afe??

Ukuwadi wenu mnaowafanyia majambazi ya mziki hauna tija kwa msanii zaidi ya dhulma,fiesta inalipa kodi % ngapi kwenye viwanja vile vile ambapo timu za mpira znakatwa kodi??!! Wacheni upumbavu wenu

Clouds nyimbo ya kwanza kwenye vipindi inathaminiwa na kampuni kama Airtel,mfano Dosen's selection kwenye xxl,kwenye amplifier-msanii mwenye nyimbo kwa nini hapewi gawio Bali watangazaji na clouds??!! Hii sio dhulma??!!

P-funk akisema,ooh kaishiwa,ni propaganda za kipumbavu mnazofanya watwana na mabwana zenu!!!
 
ngwair walimpa gari ambayo haina spare bongo. yaani ikiharibika unaagizia nje ya nchi. Kwanza gari lenyewe lilikua bovu. kuna siku alikua kwenye mataa ya karume, taa zilivyo ruhusu akaondoka lakini gari ilikua ikitembea upande upande yeye akajua pancha, ikabidi aipeleke pale kituo cha mafuta kuiacha coz haikua na spare tyre. ile anamkabidhi mlinzi, mlinzi akamwambia he! mbona haina tyre moja? kumbe tyre ilibaki mataa. na aliporudi akakuta wahuni washaondoka nayo. mia
 

Japo siyo jambo la kuchekesha lakini nimecheka sana na sidhani kama nitakuja kucheka tena kama nilivyocheka siku ya leo.

R.I.P. Ngwair. Mia.
 
Naikumbuka zamani kipindi cha majani nymbo kali redion zilitoka kwa majani ngoma kali top ten alitengeneza majani,leo majani sio kapuni majani sio gizan leo majani maji ugokoni.
 
Naweza kukups jina langu sio tatizo..lipi? La kusanii au la ubatizo?
 
Kwani dre, timbaland, chuck d wa public enemy, pdiddy babu??mbona bado wana fanya music ya hiphop..au hujasikisikia latest zao.
Kikubwa hapa ni kuchanganua haki za wasanii, nini wafanye ili waweze kuzipata hizo haki zao na maendeleo yao binafsi kimusic na kimaisha..

Pfunk ni produsa mkubwa hatukatai lkn inabidi awe innovative cos yeye ni legend sasa lazima aoneshe mfano wa mbele kuna nini na wafanye nini..yeye aki crack sasa jay moe afanye nini?
 
Hao uliowataja mimi nimewa inspire kurap. Je walipokuwa chini ya pfunk wamepata nini kimuziki mbali ya kurecord na kupata misifa ya kujulikana??

Akuna msanii wa bongo hiphop amefanikiwa chini ya pfunk. Nioneshe mmoja..na nieleze amefika wapi?
 
Msanii atapewaje mgawo wake hapo wakati wimbo wake ulifika radioni clouds dm kishkaji na sio rasmi (kupitia music publisher)??

Biashara ya muziki haiendi hivyo??
Ni sawa na kuingia msikitinina viatu alafu unataka waislamu waliopo hapo msikitini wakusikilize hoja zako? Haiwezekani. Kwanza watakutoa nje alafu ndo wakusikilize kulikoni umeingia na viatu.sio kukusikiliza issue zako.

So wasanii lazima wafuate misingi ya music business..lasivyo itakuwa ni kupoteza muda.
 
Umdhanie ndie kumbe siye...mi nipo zangu usa..wewe unatafuta jina si ingeniuliza mimi tu...!!@
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…