Enzi zako zimekwisha P FUNK pole sana

Enzi zako zimekwisha P FUNK pole sana

Status
Not open for further replies.
Huyu p,foku mwehu wengine alikua anadiriki kuwalazimisha awa0713.yote tunayajua tumenyamaza huna lako nenda kavute bangi na mateja wenzako usitake sifa kwa mhongo wa ngwear wewe umeishiwa na hao clouds huwawezi wako juu utawasoma mawinguni mwehu wewe mvuta bangi

kila mtu atakua juu kwenye sekta yake. p funk alikuwepo kabla ya clouds wafu. na bado anadunda. juzi amewapa makonde leaders club na kuwashutumu ushoga aibu aibu badala yake mkaomba msamaha mpige naye picha. mia
 
Nimesoma hii michango nikagundua ya kwamba watu wengi hawafahamu kinachoendelea kwenye ulimwengu wa muziki Tanzania.

Iko hivi: P funk akishirikiana na mjasiriamali mmoja wa hapa town wanajenga studio moja ambayo kama ikikamilika itakua moja ya studio tishio sana hapa mjini. Hawa jamaa wamejipanga mno na tunavyoelekea huko mbele kuna tetesi kwamba wataelekea kufungua radio ambayo itakuja kuwa tishio kwa hawa jamaa wa mawingu.

Pfunk huyu huyu aliyefulia na kuishi kwa mama yake ugali shkamoo au amezaliwa mwingine? kama ni huyu huyu wa mabange tutasubiri sana kuiona hiyo studio na redio. Labda kama ni mwingine amabaye majina yamefanana
 
Hivi kuna producer wa hiphop East and Central Africa level za P Funk?
Naomba mnitajie mmoja tu! P Funk alikuwa DJ kabla ya kuwa producer kama inavyokuwa kwa maproducer nguli wa hiphop.
Sikiliza cheza kidogo ya Jay Mo usikie alivyosugua santuri wengine wanatumia effects za computer tu.
Pamoja na mapungufu yake kama binadamu jamaa ni kichwa.
 
Mi Naona unajitangaza tu,. Kaka p.funk harekodi watu wasiojua ilimradi tu apate pesa kama. Wafanyavyo mengine. Yeye anachagua wenye vipaji,. Kama huna kipaji hakubebi,. Na kumbuka pia, wenye vipaji kama pig black walirekodiwa Nyimbo hata bure,. Alikutosa kwakuwa hakuona kipya,. Usimlaumu
 
Asante kaka,. Wanataka kusema mensen selekta ndo mkali kuliko p.funk kisa ana tuzo? Au ni maneke mzee wa ku-sample? Mako chali mpiga viduku,. Lamar beat moja.. wanasahau p.funk ndo ameweka foundation ya beat za bongo flavour,. Yeye ndiyo ameidefine bongo flavour,. Yeye ndiyo aliyetengeneza miziki ambayo wazazi wetu walielewa bongo fleva cyo uhuni na kuturuhusu kuwasha radio sebleni,. P.funk mpaka sasa hana mpinzani Kwani hakuna producer aliyeaccomplish makubwa kama Yeye,. Ni sound engineer mzuri na msije mkasema na ludigo kaisha Maana nitawashangaa zaidi..
 
Huyu Pfunk namkumbuka alikuwa bwana mdogo sana wakati mimi naanza rap pale SINZA. Nilipokuja sikia baadae kuwa ndo producer mkubwa pale kijitonyama alafu anawapeleka mputa wasanii just kurecord, alafu siyo bure bali kwa hela zao tena na appointment zake mwenyewe pfunk. Nikawa naongea na rafiki yangu mwingine pale bongo akaniambia jamaa (pfunk)noma, anajiona sana. Nakumbuka nikamwambia rafiki kuwa asijali sana kama kuna nyimbo anataka kirecord aende kwa master jay akarecord aachane na pfunk. Akanisikiliza. So pfunk kaishiwa...sababu kubwa za kuishiwa ni zifuatazo:
1. Hakujiandaa kukabiliana na upinzani wa studios zingine zilizofuatia
2. Hakuwa innovative enough na ndo maana hadi leo ukisikiliza productions zake hamna kipya, yale yale tu madudu
3. Bado hajui what is music business, ndo maana anaropoka wasanii wanaonewa wakati hakuna hata msanii mmoja bongo (si jidde wala ali kiba) ila diamond tu ambaye rasmi anatumia music publisher - Babu tale kupeleka nyimbo zake radioni na ktk TV stations.
MSIMLAUMU BABU TALE YEYE NI MUSIC PUBLISHER ILAINABIDI AWE RASMI NA ALIPIE USHURU NA AWE NA MIKATABA RASMI YA WAZI WAZI ILI WASANII WAWE WANAMTAFUTA.

Wasanii wengi walikuwa wanapeleka nyimbo radioni kiholela holela tu, kishkaji kukwepa kuuza copyright zao kwa publishers kama babu tale, lakini wanasahau kuwa hata akina dr.dre wanafuata misingi ya music business yaani kutumia pubishers alafu baadae mnakubaliana upya jinsi ya kugawana catalogue value ya copyrights za nyimbo zako. Jambo ambalo diamond atalifanya baadae.
4. Tanzania tunapenda kuepuka kufanya mambo kiholela holela. Wengi walikuwa wanapeleka nyimbo radioni kishkaji tu. Leo wanalalamika haki zao wakati radioni nyimbo zilifika kishkaji tu hakuna contract yoyote signed.
5. Nenda google tafuta music publisher hakuna mbali ya remmy ongala na ochestre matimila.( haya remmy aliyaina mapema sababu alifanya music na akina peter gabriel). Alikuwa mjuzi.
6. Ushauri kwa pfunk na wasanii wote wa bongo flava (kama watasoma yangu): jifunzeni kupita vyombo maana hapo mlipo copyright zenu anamiliki priducer wa studio. Mkishajua kupiga vyombo mnaweza kujadiliana na music publisher kuhusu haki zenu mkaeleweka. Ni rahisi that way kuliko kivingine..
- tumieni publishers ili mjulikane rasmi, na mlipwe haki zenu rasmi, hata mkifa kama akina ngwear ndugu zenu waweze kufuatilia haki zenu wazi wazi. Jiulizeni..NDUGU ZA NGWEAR WATAMDAI NANI HAKI ZA KIMUZIKI ZA NGWEAR??

wasalaam. Ni mimi msanii mwenzenu ughaibuni lakini soon nakuja bongo kiachia nyimbo zangu RASMI..

Aaaaah babu!ebu acha zako bwana! Yan badala uachie wajukuu akina diamond na wewe unataka ukirudi uachie ngoma???????!
Yan naimagine kama p funk ni dogo kwako we utakuwa kama nani?!!labda mzee gurumo,kitime hivi!
Pumzika bwana umri umesogea huo,cheza cheza na wajukuu tu!

Aaah samahani nlisahau, SHKAMOO

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Enzi hizo ukiwa na studio ulikuwa kama mfamle . wasanii wanakuja kurekodi kwa hela zao tena kwa apointment yako lakini ulikuwa na uwezo wa kuwafukuza kama mbwa tena na matusi juu kama sio makofi. Leo hii studio zimejaa tele za kumwaga hapa mjini vijana wadogo akina Marco chali, 69 record... Etc wamekufunika wanapiga hela . Wasanii sasa ndio wafalme . Sasa ndio unastuka unatafuta mchawi unapagawa na kuona radio clouds fm wanafaidi. Au sio wewe majani ulikuwa umemweka mvuta bangi mwenzako Juma Nature awe kama sekretali wako eti yeye ndio awafanyie usaili wasanii na hela zao kabla ya kuingia kwako kurekodi. Juma nature mwenyewe wanamkuta kalewa bangi ,tambuu na guberi.sio wewe ulikuwa unavunja makundi ya wasanii ili wawe wengi kisa tu wakiwa kundi hawana maslahi kwako . Unadai una uchungu na marehemu Mangwair. Vipi na mateja wengine katika studio yako mbona huwaongelei akina MOX, daz baba,TID, Juma nature, Q chief, Terry au Fanani wa hard brasters ....etc hadi wakifa nao utasema una uchungu na wameuliwa na Clouds. Watanzania tujifunze hela ikikimbia usitafute mchawi.

wewe utakuwa mmoj wa hao kina clouds jinsi tu unavoongea..
 
Baada ya lady Jaydee sasa mmehamia kwa P-funk??!!

Tatizo la clouds hawapendi kukosolewa, nyie vibaraka wa clouds nijibuni-DJ Venture wa clouds alikuwa Manager wa Mangweha,album ya a.k.a Mimi walimpa pesa isiyozidi million 3 na gari ambayo alikija kupokonywa kwani ilikua haijalipiwa,je ni haki????!!!

P-funk kamrecodia Madilu System Mamuu remix,kamuuzia beat Chameleon,Kamuuzia beat Whine Wonder,kamtengenezea beat Mims, who else than Majani aliefanya japo robo tu ya hayo??!!

Maproducers wa leo sio wabunifu na ubora ni sifuri kwa wengi sema wanabebwa tu kuwapoteza wakongwe,Maku Chali alianza kumkopi P,Lamar kafundishwa na P,mpeni Majani heshima yake,au hadi nae afe??

Ukuwadi wenu mnaowafanyia majambazi ya mziki hauna tija kwa msanii zaidi ya dhulma,fiesta inalipa kodi % ngapi kwenye viwanja vile vile ambapo timu za mpira znakatwa kodi??!! Wacheni upumbavu wenu

Clouds nyimbo ya kwanza kwenye vipindi inathaminiwa na kampuni kama Airtel,mfano Dosen's selection kwenye xxl,kwenye amplifier-msanii mwenye nyimbo kwa nini hapewi gawio Bali watangazaji na clouds??!! Hii sio dhulma??!!

P-funk akisema,ooh kaishiwa,ni propaganda za kipumbavu mnazofanya watwana na mabwana zenu!!!
 
ngwair walimpa gari ambayo haina spare bongo. yaani ikiharibika unaagizia nje ya nchi. Kwanza gari lenyewe lilikua bovu. kuna siku alikua kwenye mataa ya karume, taa zilivyo ruhusu akaondoka lakini gari ilikua ikitembea upande upande yeye akajua pancha, ikabidi aipeleke pale kituo cha mafuta kuiacha coz haikua na spare tyre. ile anamkabidhi mlinzi, mlinzi akamwambia he! mbona haina tyre moja? kumbe tyre ilibaki mataa. na aliporudi akakuta wahuni washaondoka nayo. mia
 
ngwair walimpa gari ambayo haina spare bongo. yaani ikiharibika unaagizia nje ya nchi. Kwanza gari lenyewe lilikua bovu. kuna siku alikua kwenye mataa ya karume, taa zilivyo ruhusu akaondoka lakini gari ilikua ikitembea upande upande yeye akajua pancha, ikabidi aipeleke pale kituo cha mafuta kuiacha coz haikua na spare tyre. ile anamkabidhi mlinzi, mlinzi akamwambia he! mbona haina tyre moja? kumbe tyre ilibaki mataa. na aliporudi akakuta wahuni washaondoka nayo. mia

Japo siyo jambo la kuchekesha lakini nimecheka sana na sidhani kama nitakuja kucheka tena kama nilivyocheka siku ya leo.

R.I.P. Ngwair. Mia.
 
Naikumbuka zamani kipindi cha majani nymbo kali redion zilitoka kwa majani ngoma kali top ten alitengeneza majani,leo majani sio kapuni majani sio gizan leo majani maji ugokoni.
 
Naweza kukups jina langu sio tatizo..lipi? La kusanii au la ubatizo?
 
Kwani dre, timbaland, chuck d wa public enemy, pdiddy babu??mbona bado wana fanya music ya hiphop..au hujasikisikia latest zao.
Kikubwa hapa ni kuchanganua haki za wasanii, nini wafanye ili waweze kuzipata hizo haki zao na maendeleo yao binafsi kimusic na kimaisha..

Pfunk ni produsa mkubwa hatukatai lkn inabidi awe innovative cos yeye ni legend sasa lazima aoneshe mfano wa mbele kuna nini na wafanye nini..yeye aki crack sasa jay moe afanye nini?
 
Hao uliowataja mimi nimewa inspire kurap. Je walipokuwa chini ya pfunk wamepata nini kimuziki mbali ya kurecord na kupata misifa ya kujulikana??

Akuna msanii wa bongo hiphop amefanikiwa chini ya pfunk. Nioneshe mmoja..na nieleze amefika wapi?
 
Msanii atapewaje mgawo wake hapo wakati wimbo wake ulifika radioni clouds dm kishkaji na sio rasmi (kupitia music publisher)??

Biashara ya muziki haiendi hivyo??
Ni sawa na kuingia msikitinina viatu alafu unataka waislamu waliopo hapo msikitini wakusikilize hoja zako? Haiwezekani. Kwanza watakutoa nje alafu ndo wakusikilize kulikoni umeingia na viatu.sio kukusikiliza issue zako.

So wasanii lazima wafuate misingi ya music business..lasivyo itakuwa ni kupoteza muda.
 
Umdhanie ndie kumbe siye...mi nipo zangu usa..wewe unatafuta jina si ingeniuliza mimi tu...!!@
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom