EPA na mambo yake

Nashukuru kwa marekebisho.

Baada ya kukwapua hizo hela walifanya nini? wamefungua viwanda wakaajiri? etc...

NAAMINI Leo wamo miongoni mwa hawa hapa:

Money Planners & Consultants inayomilikiwa na Paul Nyingo na Fundi Kitungi na kampuni ya Njake Hotel & Tours Limited inayomilikiwa Japhet Lema, Anna Lema, Abel Lema, Derick Lema na Benard Lema wa Arusha.

G&T International Limited, ya Octavio Timoth na Beredy Malegesi.

Excellent Service Limited inayomilikiwa na Emil Samanya, Peter Sabas na Elisifa Ngowi. Clyton Marketing ya Ngowi na Edwin Mtoi.

Rajabu Maranda na Thabit Katunda wanatajwa kumiliki kampuni ya Liqiud Service Limited .

Mibale Farm ya Kizza Selemani na Farijala Hussein na Malegesi Law Chambers inayomilikiwa na Beredy Malegesi.

Wamiliki wengine ni Paul Nyingo na Fundi Kitungi, wanaomiliki Kampuni ya Money Planners & Consultants na Kiloloma & Bros Enterprises inayomilikiwa na Charies Kissa.
 


Elisifa Ngowi (Afisa Mwandamizi TISS)Sidhani kama wartamweka kizuizini labda kama ni danganya toto,

ni mmoja ya watu ambao wanaweza wakafanya nchi isitawalike kama akiweza kuzungumza anachokijua..Ana SIRI kubwa na nadhani kwenye dili ya kampuni ya kilimo Kagoda 'Agriculture' atakuwa alihusika
 
Nafuu walifungua makampuni kuliko wangeenda kuweka(kulimbikiza) hizo hela benki Uswisi, Marekeani n.k.(silisifii hili ila ni katika kuchambua mambo)
 
Jamani wana JF
Hamna mwenye data hawa watu wanamiliki vitu gani? na wapi?
Nimesikia mmjoa aliajiza range rover UK. Tunataka majumba n.k

Kama muuliza swali ni mmoja wa wale mnaojifanya wajanja wa mjini mlionununua Apartment kwa Lukaza mhesabu maumivu mwaweza jikuta hampati hizo Apartments na Hela zenu hazirudi na mkileta za kuleta na nyie itabidi msaidie kueleza pesa za kununua hizo Apartment mlipata wapi na mlijuanaje na Fisadi Lukaza hadi mkaingia dili za kuuziana Apartments kwenye mabaa bila mikataba ya kueleweka kama na nyie sio mafisadi.

Mtajijua mkitaka itabidi mfungue kesi ingine ya EPA dhidi ya Lukaza kwa kuwauzia Apartment hewa!
 
Wanabodi,

Kuna baadhi yetu humu wanachukulia kupelekwa mahakamani kama ni kitu kidogo. Naomba niwaambie mtu kama Jeetu Patel kukaa kwenye hilo bench la kizimbani kisutu kama maji mtungini akisikiliza mashitaka dhidi yake sio kitu kidogo.

.

Mulize Alex Massawe atakwambia nn maana ya kuka kwenye hila bench ... hadi kesho ukimkuta pale kijiweni chagga street kwenye sambusa anasimulia nn maana ya RAIS. maana wakati wa kampeni walikuwa nae JK alivyowageuka duh!
 
jamani hakuna jipya?ingizo jipya?

Vi nzi bado vinaruka ruka kwenye uchafu vikisha shiba vitakuja kucheua hapo usikonde mambo ndo yameeanza sasa nani wa kulizima mmh!! ni hakimu..

Ila kuna news nimepata kuwa Jeet Patel alikuwa Dubai hapo wajanja wakamrubuni akarudisha pesa kibao akaona mambo sasa yatakuwa shwali na walio kuwa wanamfatilia wakamlizisha kuwa mambo sasa yatakuwa shwali akajiloga akarudi TZ ndipo walipo mbana hakuna kutoka ndania ya 18 ndio hivyo tena macho yamemtoka haamini na utajiri wake woote kama anaweza akayakalia mabench yale.
 


Aisifue mvua, imemnyeshea!
Unadhani ni sifa kuwasifia waliopata pesa kwa wizi?Hapa watu wanaongelea mambo mazito wewe unaleta upambe! Tafuta forum nyingine ya kuwafagilia mafisadi.Kwani nani asiyewajua wanapataje fedha zao au unataka tuwaaibishe zaidi humu??
 
Mbona Mkapa hayumo ? lini mtamfikisha mahakamani kwa wizi alioufanya? yeye ndio alieimaliza nchi hii !! Its a shame
 

Singel D kelele tuendeleze kwa sheria kucuhukua mkondo wake, lakini pia tuendeleze kelele kwa ajili ya mipapa ya EPA, siyo tushangilie hivi vidagaa na kafara tu tusahu kwamba wahusika wakuu, walo alo wasema pinda kwamba wanaweza angamiza taifa? wapo wanapeta!

Siamini kama wale vijana wadogo nilo waona ukiondoa Jeetu na Lukaza eti ndo serikali ilikuwa ikiwagwaya!!, Lazima tuzidi kupaaza sauti, na wale baba zao (vigogo) washughulikiwe!

Inashangaza sana eti Mgonja aliye kuwa akiidhinisha yeye mambo haya ahayamgusi?? na wako wapi watendaji wa BOT wali husika? tunataka zaidi ya hapa... hatutaki kushangilia 'kupewa kijiko kimoja cha sukari wakati gunia zima lime jaa sukari' wkamatwe wote, sheria iache ichukue mkondo wake ndipo tutawapongeza, vinginevyo tutaendelea kupaaza sauti hadi kieleweke!
 

SOA, you can't be serious, hebu read what you wrote aloud.... make sure no one hears you, usije ukawa incarcerated for mental health reasons
 
Jamani Jeetu ameshatoka??? Nasikia kina Tanil na Manji wamesema hata kama bail ni 100million USD, lazima Jeetu arudi kwenye hekalu lake Msasani!!

Sasa tuambieni yaliyotokea huko Kisutu, maana kina Lukaza na Malegelesi nasikia serikali inataka wakae rumande muda wote wa kesi sababu ya matusi na kejeli waliyowapa tume ya Mwanjika.
 

Nakubaliana na wewe mkuu especially kwenye kuhusu watuhumiwa wengine.
Tunajuwa kabisa kuwa watumishi wa BOT walijuwa wazi kuwa documents zote zilkuwa forgery...Deal ilikuwa na vi memo kutoka kwa viongozi wa nchi nk.

Hawa kina Jeetu na Lukaza waliplan deal na walishirikiana kwenye implementation na ndio maana wakawatumia wanasheria wa Malegesi ili kujidai ku "Confirm" kwamba makampuni hayo ni real.

Accompanied by vimemo kutoka kwa watop flani flani dili lilipita na hata Ballali alikiri.

Ni paka anavishwa kengele so tutaona mwisho wa movie..Kama ni kweli haki inatendeka tutajuwa na kama si kweli pia tutajuwa.

Jambo moja namuomba Mh Rais ni kwamba hili lisiwe kiini macho hata mara moja...Kwasababu tunafuatilia kwa karibu sana...
 


Huyu ni wa kumpa Kidonge ili akae kimya milele ,kwani anafaida gani kwake mwenyewe na kwetu sisi?
 
Wangapi wamefikishwa mahakamani leo?

Mtanzania, bahati mbaya sana nimeondoka Dar na huku nilipo mawasiliano si mazuri sana, lakini kabla ya kuondoka nilifahamu kuhusu kufikishwa kwa mtu anayeitwa Rajabu Maranda na wenzake na pia wamiliki wa Njake wa Arusha, ambao ni kina Lema.

Maranda ni maarufu kama mfadhili wa CCM mkoani Kigoma.
 

Nimefahamishwa Maranda yumo na mmoja kati ya waliokwenda kumdhamini ni Dk. Walid Aman Kabourou wa CCM, yule aliyehamia huko akitokea Chadema.

Sijapata hakika hasa kama alidhaminiwa na wengine ni kina nani lakini wanasema wanakaribia wanne
 
Nimefahamishwa Maranda yumo na mmoja kati ya waliokwenda kumdhamini ni Dk. Walid Aman Kabourou wa CCM, yule aliyehamia huko akitokea Chadema.

Sijapata hakika hasa kama alidhaminiwa na wengine ni kina nani lakini wanasema wanakaribia wanne

Asante sana Mkuu Halisi,

Mimi nakuamini kwa data, nikiona breaking news ya Halisi huwa najua hapo kuna jambo zito kitaifa.

Mungu awape nguvu wanaosimamia hili maana litakuwa fundisho kubwa kwa hawa wafanyabiashara majambazipamoja na walinzi wao kwenye vyama vya siasa.

Sasa Lowassa kama ana nguvu si aende akamwokoe Lukaza?

Tusubiri yule lawyer Malegesi kama sijakosea jina lake, tuone kama anaweza kujiokoa mwenyewe.
 

No wonder this njake guy has littered the ms - ars highway with gas stations..... Lile ghorofa kule njiro halitakalika vizuri sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…