Ephraim Mrema na Ufisadi TANROADS


Yeah yuko Sweden huyo mjinga mjinga ngedere magari
 

I think the burden of proof should be on you. You'll need to demonstrate what possible "performance" criteria would justify any local CEO to be paid that kind of ridiculous annual bonus in an impoverished country like Tanzania.
 


Sasa kwa sababu tumeamua kuchukua mmoja wetu, ningedhani kuwa tungeangalia zaidi uwezo wetu na hali ya nchi yetu. Hao wote tunaowalipa mishahara ya kufuru, tunafanya hivyo kwa kuwapunguzia wananchi wa kawaida.


tunawapunguzia nini?

Kwa maoni yangu ni dhambi kumlipa mwenzetu mishahara ya namna hiyo wakati tunashindwa kumlipa mwalimu wa shule ya msingi mshahara ambao utamtosheleza kwa mahitaji yake basic ya maisha.

Tunashindwa? kwanini unaamini kuwa tunashindwa?

Tunampa mtu bonasi ya dola 102000 wakati tunashindwa kuokoa maisha ya wakina mama lukuki wanapojifungua!

Tunashindwa? kwanini unaamini tunashindwa kuokoa maisha ya wakina mama wakijifungua?
 
tunawapunguzia nini?

[/SIZE][/FONT]

Tunashindwa? kwanini unaamini kuwa tunashindwa?



Tunashindwa? kwanini unaamini tunashindwa kuokoa maisha ya wakina mama wakijifungua?

You are asking rhetorical questions that don't serve any useful purpose. You (and everybody else) know very well that there are thousands of women and newborns all over Tanzania that lose their lives during childbirth due to inadequate health care. By the way, Tanroads appears to be a World Bank Project and there's good reason to believe the unusually high remuneration the CEO is paid for by WB.
 
tunawapunguzia nini?

[/SIZE][/FONT]

Tunashindwa? kwanini unaamini kuwa tunashindwa?



Tunashindwa? kwanini unaamini tunashindwa kuokoa maisha ya wakina mama wakijifungua?

Pato la taifa ni finite. Tunazalisha kiasi fulani na kiasi fulani ndicho kinachoingia katika coffers za taifa. Hizi ndizo zilizopo kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watanzania wote. Ni kutokana na pato hili ndiyo mishahara ya wafanyakazi wa umma, madispensari na dawa zake, shule za umma, safari za wakuu n.k. n.k zinalipwa. Tukimlipa Mrema mabilioni ina maana ni lazima kuna sehemu tutapunguza. Huo ndio ukweli uliopo. Katika nchi zenye mifumo ambayo ni egalitarian hawalipani mishahara ya kufuru kwa sababu hiyo. Mishahara ya watumishi wa umma katika nchi za Nordic ikiwa mfano. Kutokana na hili hakuna anaekosa huduma muhimu. Katika nchi wanazolipana mishahara ya kufuru kama Marekani basi wanapunguza katika huduma za jamii. Ndiyo maana kuna raia na wakazi wa nchi hiyo hawana tofauti na mlala hoi wa nchi nyingi zinazoendelea. Lakini hata huko hawajifikia tulipo sisi. Nchi yenye GNP per capita chini ya dola 1000 kwa mwaka haiwezi kutetea kumlipa mtu mmoja bonasi ya dola 100,000. Au mshahara wa dola 8000 kwa mwezi ambao hata huko kwa wenzetu si wa watu wa kawaida. Unataka kujua tunawapunguzia nini? Tunawapunguzia uwezo wa kuweza kumudu maisha. Kula angalau mlo mmoja kwa siku, kuweza kupata huduma ya tiba wanapohitaji, uwezo wa kupata elimu n.k. Kwa kifupi, uwezo wa kuishi kama binadamu.

Pamoja na hadithi za alinacha kuhusu utajiri wa nchi hii ukweli ni kuwa bado tu masikini wa kutupwa. Hatuna uwezo wa kuokoa maisha ya wakina mama waja wazito wote bali tuna uwezo wa kupunguza vifo hivyo. Hata huo unaathiriwa na sense ya entitlement ya wale tuliowapa dhamana ya kutuongoza. Wanachofanya ni kutia chumvi kwenye kidonda cha umasikini wetu!

Amandla.......
 

Agreed. He should know better.

Unfortunately hakuna free lunches kutoka WB. Kama wanamlipa hivyo mheshimiwa huyu ni lazima watakuja kutudai siku za mbeleni!

Amandla.......
.
 
Tanzania tuna mambo ya ajabu. Kuna contractor anaisulubu TANROADS mahamakani halafu lawyer wao ni Mkono, mbunge, muwakilishi wa wananchi...! Go figure

 
Mchezo mchafu watikisa TANROADS
• Vigogo wapoka mradi wa mkandarasi

na Mwandishi Wetu



WAKALA wa Barabara nchini (TANROADS), inadaiwa kupata hasara ya mabilioni ya shilingi baada ya kupoka mradi wa ujenzi wa barabara ya Dodoma - Manyoni uliokuwa ukitekelezwa na Kampuni ya ujenzi ya Konoike.
Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata, zinaeleza kuwa kupokwa kwa mradi huo kutoka kwa Kampuni ya Konoike kumeisababishia TANROADS kulipa sh bilioni 30.1, kinyume cha utaratibu.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya TANROADS, vimeeleza kuwa uamuzi wa uongozi wa juu wa TANROADS wa kuuondoa mradi huo kwa Kampuni ya Konoike una kila dalili za shaka, kwa sababu ukaguzi wa ujenzi wa barabara hiyo unaonyesha kuwa mkandarasi alikuwa akitekeleza kazi yake sawasawa.
Mmoja wa viongozi wa juu wa TANROADS, aliliambia gazeti hili kuwa uamuzi huo ulichukuliwa na ‘bosi’ bila kushirikisha bodi zinazohusika na kuikabidhi kampuni nyingine ya ujenzi ambayo gharama zake za ujenzi kwa kilometa ni za juu kuliko za Konoike.
“Sote tunashangaa jinsi mkubwa alivyochukua uamuzi huu, tulisikia tu kuwa mradi huo umepokwa kutoka kwa Konoike na kupewa mkandarasi mwingine. Maamuzi yalichukuliwa bila kufuata taratibu na hatujui Konoike walikosea nini, kwa sababu walikuwa wanatekeleza ujenzi kwa mujibu wa mkataba wao.
“Cha kushangaza zaidi ni taarifa tulizopata kuwa mkandarasi mpya analipwa sh bilioni 1.4 kwa kila kilomita anayojenga, wakati Konoike alikuwa analipwa sh milioni 820.5 kwa kila kilomita,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Habari zaidi zilizopatikana zinaeleza kuwa wakati Konoike wakipokwa mradi huo, walikuwa wamekwisha kujenga kilomita 110 kati ya kilomita 127 zilizomo katika mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo.
Zinaeleza zaidi kuwa kampuni mpya iliyopewa mradi huo imelipwa sh bilioni 30.1 badala ya sh bilioni 13.9, jambo linalodaiwa kuzua maswali ya kuwapo dalili za rushwa katika ubadilishaji wa mkandarasi wa ujenzi huo.
“Unajua, hawa Konoike wana kiburi, wanalingia ubora wa kazi zao, sasa wakubwa walitaka wawape chochote, wakakataa, ndiyo yakatokea haya. Lakini swali kubwa tunalojiuliza, hizi sh bilioni 16.8 zilizozidi katika malipo zimekwenda wapi?” alihoji mmoja wa watoa habari hizi ambaye jina lake tunalihifadhi.
Barabara hiyo ya Dodoma – Manyoni, yenye urefu wa kilomita 127, ilianza kujengwa na Kampuni ya Konoike Machi 14, 2007 kwa gharama ya sh bilioni 63.8.
Desemba 16, 2008, TANROADS ilisitisha mkataba na Konoike wa kujenga barabara hiyo na kuteua kampuni nyingine ambayo zabuni inadaiwa kutowekwa wazi.
Akipoulizwa kuhusu madai hayo, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Ephraem Mrema, alikiri kulifahamu jambo hilo na kueleza kuwa anaweza kuliongelea kwa kina akiwa katika hali nzuri. “Unajua sipo katika hali nzuri, suala hili kweli lipo, lakini si kubwa kiasi hicho, linaweza kurekebishwa tu. Ni makosa madogo madogo ambayo sijui hata kwenu yamefikishwa na nani. Hapa nilipo siwezi kusema lolote. Lakini naandaa majibu, nitayatoa kwa waandishi wa habari,” alisema. Aliongeza kuwa suala hilo litapatiwa ufumbuzi na ofisi yake, kwa sababu ina uwezo wa kubatilisha chochote kilicho chini ya uwezo wake kama kilifanyika kimakosa.
 
Jambo hili linatia utata kabisa na hii inaoneka wazi kuwa hizi ni njia za awali ya kuanza kukusanya pesa za kampeni kweli huu ni mchezo mchafu.
 
Jambo hili linatia utata kabisa na hii inaoneka wazi kuwa hizi ni njia za awali ya kuanza kukusanya pesa za kampeni kweli huu ni mchezo mchafu.

OOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOhhhhhhhhhhhhh yeeeeeeees

there u"r
 
Huyu Mrema aliwekwa na B. Mramba, sasa huyu mramba ambaye ameramba pesa za jasho la watanzania kiufisadi kwanini aiife ti jamani pamoja na mafisadi wengine wote
 
Wandugu,

Zimefumuka tena taarifa za Ephraim Mrema CE TANROADS kupewa rushwa kubwa katika mradi wa barabara hapa Kagera.

Vyanzo visivyoelezeka hapa vyasema mradi huu wa KAGOMA - LUSAHUNGA ulikuwa na mkandarasi mchina, aliyekuwa anajenga 150km kwa 48Bilion. Mrema akamtimua na sasa kampatia mkandarasi mwingine mradi huo huo kwa urefu huo huo kwa 190Bilion!!....WHAT A BIG DEAL!

Maelezo yanaonyesha kuwa mkandarasi wa kichina wa awali alishafanya kazi ya asilimia 38, sasa twajiuliza imekuwaje huyu mkandarasi wa sasa apewe kwa zaidi ya 100Bilion kazi hiyo hiyo? NA KWANINI ALIMFUKUZA WA AWALI?

Nikwamba anajenga 1km kwa 1.2Bilion!!! ...WHOH!!! juzi waziri wake kasema 1km ni 800milion!...

HIVI HIZI HELA 100BILION ZIMEKWENDA WAPI? KWANI HATA KWA 40BILIONI MKANDARASI MPYA ANGEFANYA KAZI ILIYOBAKI KWASABABU KAZI KUBWA ILISHAFANYWA NA MKANDARASI WA MWANZO.....what a shame upon you Mrema....?

Pia huyo mkandarasi wa awali kaenda kortini, hivyo si ajabu serikali ikalimwa 37Bilioni tena na kufanya mradi wote ugharimu 260Bilion.

JE UFISADI HUU HADI LINI?
 
TANRODS ni uozo tu!! Yet CEO yupo madakani na anapeta tu!!!

Hii ndo Tz..Mrema sii alikuwa chaguo la Mramba?

sasa kama Mramba hayupo tena..kwa nini asiondolewe na hizi kelele zote???
 
Hivi hamfahamu kuwa tupo mwaka 2009?

Miaka ya nyuma walikuwa wanachota BoT uchaguzi ukifika na baadaye wanazirudisha. Ila sasa hivi huko kutakuwa kumewaka maana watu wanaangalia kila siku. Sasa watakuwa wanachota Tanroad, Tanesco, ATCL, Bandarini nk ili kugharamia nguo za njano na kijani mwakani wakati wa uchaguzi.
 
Tanroads kuna shida upande wa Contract selection na management nadhani. mara nasikia wamelalamikiwa kwa arbitrator na mahakamani ; watajikuta kwa uzembe wa manpower wanaingia gharama ya ajabu.

Taasisi kama ile ilitakiwa iwe mfano kwa taasisi binafsi kwa jinsi ya kuendesha na kusimamia miradi ila ndio bonge la kimeo
 
inabidi tuelewe kiundani zaidi, kwani CEO ndo anatoa na kuidhinisha tender kubwa namna hii?hapana. wachina wana tabia ya kuunder bid(tender kwa kiasi kidogo cha fedha0 kwani wnajua tz the lowest bidder ndo anachukuliwa, sasa katikati ya kazi anjua kucheza na variations, au na mapungufu kama alivyoandika mtu hapo juu ya tanroads kutender.so usimshutumu mzee mrema kula hela kabla hujajua ni nini kimetokea, thinga are not easy as we see them, hawzi kupandisha hela yote hiyo atinya wapi?good day
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…