TANZIA Ephraim R. Mwansasu, Nguli wa Nyimbo za Injili Afariki Dunia

TANZIA Ephraim R. Mwansasu, Nguli wa Nyimbo za Injili Afariki Dunia

Mwimbaji mkongwe wa nyimbo za injili na Askofu wa Hossana Assemblies of God Ephraim R. Mwansasu amefariki dunia usiku wa kuamkia leo (29/08/2021). Mwasasu alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu, kwa sasa msiba upo Kimara Mwisho.

Mwansasu atakumbukwa kwa nyimbo zake nyingi alizoziimba kwa mvuto wa aina yake na kutoa ujumbe mzuri kwa kila aliyesikiliza na kuona video za nyimbo hizo zilizopendwa na kupata umaarufu Tanzania na nje ya Tanzania.

Baadhi ya nyimbo za Mwasasu ni:
  1. Siku nikilala mauti.
  2. Nangojea wakati.
  3. Kutesa kwa zamu.
  4. Dunia inapita.
  5. Tukimaliza kazi.
  6. Kiama.
  7. Heri wenye moyo safi.
  8. Tutatesa milele.
  9. Wosia wa baba.
  10. Watoto wachanga.
  11. Wanawake.
  12. Maumivu ya Yesu.

Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina Lake Lihimidiwe, Pumzika kwa amani nguli wa nyimbo za injili Askofu Ephraim R. Mwansasu.

View attachment 1914996
View attachment 1915817
View attachment 1915016
Poleni sana wafiwa. Kweli nyimbo zake ni maarufu sana pengine hata kuliko jina lake hasa huo wimbo wa ' Siku nikilala mauti'. Apumzike kwa amani mtumishi wa Mungu. Amefanya kazi kubwa ya utume.
 
Poleni sana wafiwa. Kweli nyimbo zake ni maarufu sana pengine hata kuliko jina lake hasa huo wimbo wa ' Siku nikilala mauti'. Apumzike kwa amani mtumishi wa Mungu. Amefanya kazi kubwa ya utume.
Amen, ni kweli kazi kubwa ya uimbaji ameifanya kwa unyenyekevu wa hali ya juu jambo lililopelekea mafanikio.
 
Je waweza fafanua zaidi Kufa kabla ya wakati?

Na je wakati sahihi ni upi?
Mwalimu ninamaanisha ukiondoa emergency za kifo kama Ajali...vinginevyo ni kujitakia.
Vifo vingi chini ya miaka 80 ni vya kujitakia, maana yake ulaji, unywaji wenye makosa na kuishi mazingira yasiyo sahihi hupelekea vifo vya mapema.
Consciousness ni kujitambua na kujua hatari zinazokuzunguka ambazo usipozijua huleta vifo vya mapema.
Ivo yaani.
 
vinginevyo ni kujitakia.
Vifo vingi chini ya miaka 80 ni vya kujitakia, maana yake ulaji, unywaji wenye makosa na kuishi mazingira yasiyo sahihi hupelekea vifo vya mapema.
Consciousness ni kujitambua na kujua hatari zinazokuzunguka ambazo usipozijua huleta vifo vya mapema.
Nashukuru sana kwa ufafanuzi huu wa kina.

Kwa hakika Jamii yetu bado inahitaji elimu ya utambuzi na kujitambua zaidi, maana mitindo ya maisha kwa sasa inaharakisha kifo/vifo kutokea mapema katika jamii yetu.

Tuko pamoja.
 
Amen, mchango wake tutaukumbuka daima.
Tutamkumbuka
Mimi nasema wazi kuwa nyimbo za Mwansasu ndizo zilizonibariki sana miaka ya 2004-2010 na ndizo zinazofundisha bila mbwembwe nyingi za kisasa, pamoja na za Mch. Abihudi Misholi na Faustine Munishi

Hakika huyu alikuwa ni hazina ya Mbeya na Tanzania kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom