TANZIA Ephraim R. Mwansasu, Nguli wa Nyimbo za Injili Afariki Dunia

TANZIA Ephraim R. Mwansasu, Nguli wa Nyimbo za Injili Afariki Dunia

Mwimbaji mkongwe wa nyimbo za injili na Askofu wa Hossana Assemblies of God Ephraim R. Mwansasu amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. Mwasasu alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu, kwa sasa msiba upo Kimara Mwisho.

Mwili wa marehemu Askofu Mwansasu unatarajiwa kusafirishwa kesho jumatatu Agosti 30, 2021 kutoka jijini Dar Es Salaam kwenda Mbeya kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika 31 Agosti 2021.

Mwansasu atakumbukwa kwa nyimbo zake nyingi alizoziimba kwa mvuto wa aina yake na kutoa ujumbe mzuri kwa kila aliyesikiliza na kuona video za nyimbo hizo zilizopendwa na kupata umaarufu Tanzania na nje ya Tanzania.

Baadhi ya nyimbo za Mwasasu ni:
  1. Siku nikilala mauti.
  2. Nangojea wakati.
  3. Kutesa kwa zamu.
  4. Dunia inapita.
  5. Tukimaliza kazi.
  6. Kiama.
  7. Heri wenye moyo safi.
  8. Tutatesa milele.

Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina Lake Lihimidiwe, Pumzika kwa amani nguli wa nyimbo za injili Askofu Ephraim R. Mwansasu.

View attachment 1914996

View attachment 1915016
He short-lived his singing talent, he was ill advised to quit singing carrier and join his Askofuship so early, funny he couldnt run all then together. Bye bye legend the icon, the league gospel the endless relevancy in all songs inter-generational relevancy of all time in gospel songs album.
 
Linga po tumalile imbombo twisa kufwala ingigha...supa nyambala ghwa Jhesu mma akabhalilo kakufwene ghwe mwana ghwa bhalondo...
Aliimba na kufikisha ujumbe kupitia lugha ya asili ili kuwafikia watu wengi zaidi.
 
Back
Top Bottom