Yani wewe unapima kutazamwa kwa Laliga kwa reference ya Tanzania?
Ufatiliaji wa ligi ni mazoea tu yaliyojijenga toka miaka ya nyuma, zipo nchi zinatazama laliga zaidi kuliko epl.
EPL is full of avarage players na ndio mana unaona kuna ushindani, ushindani hauletwi na ubora wa juu, ukisema ushindani wa timu moja kufunga nyingine ni kipimo cha ubora basi ligi ya bongo nayo ni bora kuliko laliga??
Man U anafungwa na Cristal Palace sio kwasababu Cristal Palace ni bora, ni kwasababu Man U ni mbovu, same applies kwa hizo timu nyingine. Unataka kuniambia Cristal Palace ataenda laliga akaisumbue Baca au Real Madrid pamoja na kiwango chake kibovu kwa sasa??
Kipimo pekee ni champions league na Europe league. Ndio mana ikaitwa ligi ya mabingwa. Inamana kwamba wenye uwezo wa juu katika kila ligi wanawakilisha ligi zao kwenye michuano kuona nani bora zaidi.
Hii mambo ya kuambiana kwamba timu yoyote inaifunga timu nyingine ndio ubora ni invalid kabisa. Hii ni ushindani, kushindana sio lazima muwe na ubora wa juu.
Hii kusema laliga sio bora kwasababu timu ni 2 tu alafu mnasahau kwamba hizi timu mbili kwa misimu kadhaa sasa zimekua zikipokezana kikombe kinachotambulisha mabingwa wa ulaya nzima ni uvivu wa kufikiri.
Real na Baca zimekua katika ubora wajuu sana sio tu laliga bali ulaya nzima.
Sasa timu bora ulaya nzima zitaachaje kushinda vikombe kwenye ligi yao??
Na ukiwatoa hawa real na Baca, hembu angalia records za hawa wengine kutoka laliga kwenye michuano mingine ya ulaya alafu urudi tena.