Epuka, hii ni mojawapo kati ya makufuru!

Epuka, hii ni mojawapo kati ya makufuru!

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!!

Kumekuwa na picha zinazotembea mitandaoni Hasa mtandao wa FB ikimuonyesha mtu mwenye mapembe mwenye mkia ana six parks, ambaye ni Rahisi kumhusisha na shetani, pia mwingine anaonekana akiwa amevaa vazi jeupe naye Kwa mara kadhaa amechorwa Kwa mwonekano kama mtu mwana mazoezi, mikono yake Ina matundu na miguu Ina alama za misumari,mwili umejengeka vizuri. Na mtu huyo ni Rahisi kumhusisha na YESU aliyekufa na kufufuka siku ya tatu.

Makufuru yanakuja pale watu Hawa wawili wanapowekwa pamoja wakishindana nguvu wakiwa wameshikana mikono. Kwa kutojua , wengi wamekuwa wakipiga LIKE kwenye picha hizo wakidhani ni sahihi kufanya hivyo.

Yesu ni Mungu, na Mungu tangu kuumbwa Kwa Ulimwengu huu, hakuwahi Kupambana na shetani katika vita.

Hata ulipotokea uasi Mbinguni, Yesu/ Mungu hakupambana na shetani Bali alimtuma Malaika Mkuu Mikael apambane naye Kwa kuwa Shetani Si level ya Mungu.

Shetani ni Malaika muasi, level yake Kupambana naye ni Malaika mwenzie Si MUNGU/ Yesu.

Tangu Leo usomapo onyo hili, usiweke Like yoyote kwenye picha za namna hiyo ,maana aliyezitengeza picha hizo ni shetani kupitia agents wake, Nia ni kuwakosanisha Wana wa Mungu na Mungu wao.

Mungu ni Mungu, kamwe hawezi shindana na shetani Kwa kupimana nguvu!!

Mungu awabariki.

Mungu ni MMOJA na YESU KRISTO/YESHUA HAMASHIACH ndilo JINA lake. Amen

Ikiwa hujampa Yesu maisha Yako fuatisha Sala hii;

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN

Mbarikiwe nyote 🙏
 
Malaika hawezi kuasi, malaika hana hiari ya kutii au kutotii amri za Mungu. Malaika ameumbwa kumtii Mungu siku zote.

Sisi wanadamu ndio tumeumbwa na hiari ya kutii au kutotii amri za Mungu. Miongoni mwenye kutii ana malipo yake na asiyetii ana malipo yake.
 
Kwahiyo hujui kuwa palitokea uasi Mbinguni na kiongozi wa Malaika waasi akatupwa chini kabisa?

Unapinga HOJA Kwa kutumia source ipi?
 
wangetulipa mapema hayo malipo
 
Kwahiyo hujui kuwa palitokea uasi Mbinguni na kiongozi wa Malaika waasi akatupwa chini kabisa?

Unapinga HOJA Kwa kutumia source ipi?
Shetani ni jini, hakuna malaika aliyeumbwa kuasi hao ni viumbe watukufu watiifu wenye kufanya wanayoamrishwa, kama hujui shetani alifikaje mpaka kuwa mkaazi wa huko mbinguni bora ungeuliza.
 
Barikiwa pia mtumishi 🙏
Lakini,nia yao umejuaje kama ni mbaya?Wanawajengea wasomaji picha tu na wala hawajawahakikishia kwamba kweli yule ni Yesu na mwingine ni shetani.Hapa ndiyo unataka kurudi kwenye sanamu kanisani RC.Tunapoelekea utatupatia onyo kwamba hata michoro ya ramani ni kufuru kuchora vitu vilivyoumbwa kwa "mikono" ya Mungu.
 
Shetani ni jini, hakuna malaika aliyeumbwa kuasi hao ni viumbe watukufu watiifu wenye kufanya wanayoamrishwa, kama hujui shetani alifikaje mpaka kuwa mkaazi wa huko mbinguni bora ungeuliza.
(Soma Ezekiel 28:13-18)

Waislamu kitabu chenu kimetiwa mseto wa hatari hakieleweki, na hakina mpangilio.

Ndio maana mnaabudu na majini!!
 
Lakini,nia yao umejuaje kama ni mbaya?Wanawajengea wasomaji picha tu na wala hawajawahakikishia kwamba kweli yule ni Yesu na mwingine ni shetani.Hapa ndiyo unataka kurudi kwenye sanamu kanisani RC.Tunapoelekea utatupatia onyo kwamba hata michoro ya ramani ni kufuru kuchora vitu vilivyoumbwa kwa "mikono" ya Mungu.
Nia ni ovu sababu Yesu Si size ya shetani kimamlaka Hadi washindane wrestling!!

Si vyema kuwa wabishi.
 
Nia ni ovu sababu Yesu Si size ya shetani kimamlaka Hadi washindane wrestling!!

Si vyema kuwa wabishi.
Kwani ni kweli wamepiga mieleka?Umejengewa picha tu mawazoni kwamba kuna uadui kati ya Yesu na shetani.Na ukumbuke,siyo wote ni watu wazima wenye uelewa kwamba hatuna picha za Yesu wala shetani halisi.Wengine ni watoto wanaohitaji vielelezo kukuza tu uelewa zaidi.Mbona tunafanya mambo yanakuwa magumumagumu kila nyakati?
 
Ndio nasemaje,

Hizo picha imagine Rabbon ndiye achorae, asingechora hivyo.

Wasio na uelewa wanatakiwa waeleweshwe vizuri.
 
Wewe unashauri angefanyaje?
Si Rahisi kuzuia mtu asiwaze au kutenda UOVU,

Nia ya mada hii ni kuwakumbusha Wana wa Mungu kutolike picha za namna hiyo.

Mungu ni Mungu, kamwe hawezi kushindana na kiumbe alichokiumba.

Mungu ni MMOJA na YESU KRISTO/YESHUA HAMASHIACH ndilo JINA lake. Amen
 
Back
Top Bottom