Erasto Mfugale: Kilichotokea kazini sisi hatujui

Erasto Mfugale: Kilichotokea kazini sisi hatujui

Erasto Mfugale: Kusema kweli hatukuwa tumepata taarifa dhahiri hata imetokea nini kwasababu mimi Jumapili iliyopita nilikuwa kwake Temboni, nimekuwa na mazungumzo naye mpaka saa saba usiku lakini akaniambia kesho nina kikao kidogo kule Dodoma, kwahiyo nitatoka na ndege ya mchana. Nikamuaga nikasema naenda.

Alivyokuwa kule, mtoto wake Aron Mfugale alikuwa anaumwa pia akamtakia hali. Asubuhi amepata chai pale nyumbani kwake Dodoma, akatoka kwenda kazini.

Sasa kilichotokea kazini sisi hatujui, mwisho wa siku nashkuru wizara ya ujenzi kupitia Edgar Msigala nikapigiwa simu lakini akaona hatuelewani, baadae Hija akapiga simu na akaniambia moja kwa moja Engineer amefariki dunia, nilikuwa barabarani Bagamoyo, nilitaka nigongwe na gari maana sikuwa nimetegemea kwasababu jana yake mimi nimekuwa na dada yangu, Frida Mfugale alikuwa na andiko, akasema mimi silielewi peleka kwa kaka yako, Frida ilikuwa aje Bagamoyo kwaajili ya usaidizi wa hilo andiko ili liwe andiko makini.

Basi ni maajabu, sijui kimetokea nini. Tumefika jana Dodoma, tunawashkuru serikali, tumeenda hospitali, tumefatilia ile nyaraka, wanasema hatujui ugonjwa, sasa kulikoni?

Mgonjwa alikuja ameshafariki, alikuwa wapi? Baadae habari zinasemekana alikuwa kazini, sisi hatukuelewa kabisa, tukaendelea kuchanyikiwa, kusema kweli ilituuma kweli lakini hata hivyo Binadamu njia yake ni moja.

PIA, SOMA=> Waziri Chamurilo: Familia(Mfugale) wameonyesha ombwe kwamba ilikuwa haifahamu, Mhandisi Mfugale alisema anajisikia vibaya kikaoni


Death is just death,one way or the other all we gonner die one day,
Let's not make a big deal out of it,watu wanakula risasi moja wanakufa,Tundu lisu alikula 19,na Bado yupo ,kesho unaweza kusikia amekufa usingizini.
 
Mungu kazi yake ni kufanya wengine vichekesho na kutoa adhabu tu? Hapo hapo mnasema Mungu ni mwenye huruma na mwenye nguvu zote. Kazi sana kumuelewa Mungu wenu.

Ukifikiria zaidi ni kama vile ni kazi kubwa zaidi kumwelewa Binaadam mwenyewe na concept yake nzima kuhusu Mungu, pengine hata huyu “Mungu” hausiki kabisa?!?
 
Mungu kazi yake ni kufanya wengine vichekesho na kutoa adhabu tu? Hapo hapo mnasema Mungu ni mwenye huruma na mwenye nguvu zote. Kazi sana kumuelewa Mungu wenu.

Mungu huwezi kumuelewa isipokuwa utumie kumuamini na kumuabudu kwa Roho na Kweli. Na ataendelea kufanya hivyo mpaka muelewe kuwa ile kauli yenu ya tunaenda na dunia ni ukengemfu mkubwa. Narudia, Kutoka kumtegemea Mungu wa Mbinguni mpaka kwenda na dunia inavyo enda ni ukengemfu mkubwa.
 
KIFO HAKIKOSI SABABU.


Kufariki kwa mwanadamu si lazima hadi aumwe...

Wapo watu wanaofariki kwa amani kabisa bila mateso wala ugonjwa...

Muda unatika moyo unafeli tu wenyewe na mtu anaenda zake...

Vijijini huko, kuna wazee muda wao wa kuondoka ukifika unapata anawaita watu wake wa karibu na kuwaaga kabisa...

Kuna wengine utakuta wanafanya usafi nyumba zao, wanakusanya nguo zao na kuweka mahali pazuri, muda ukifika analala zake na anapotelea huko
 
Waanze na mamako kwanza. Usilete utani kwenye uhai wa mtu mbwa wewe
Kwani wewe unamfahamu huyo aliyetajwa ni nani? Mbona umekuwa mkali?

NB. Uhai wa mtu ni kitu cha thamani sana, sifurahii mtu kutolewa uhai wake kwa na namna yoyote ile.
 
Je, ajenda za kikao zaweza sababisha? Tuanzie hapo, pia tuangalie na ripoti ya kamati ya bot, kwa kuwa zimekaribiana na kuwasilishwa kwake na dokezo la tanroad na TPA kuwa na ukakasi, tusiende mbali tuanzie hapo!
 
Sina mengi ya kueleza ila kwa ufupi nazungumzia kifo cha kimiujiza cha bwana Mfugale
 
Back
Top Bottom