Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kwa mara nyengine tena raisi wa Uturuki ,Tayyib Erdogan amekuja na pendekezo la kupambana na Israel ili kuwatetea wapalestina na kujikinga na hatari za kujitanua kwa Israel kwenye maeneo ya waislamu.
Pendekezo hilo amelitoa hapo juzi kwenye hafla ya shule moja ya kiislamu nje kidogo ya jiji la Ankara.
Ili kuonesha kwamba nchi yake iko mbele kwenye juhudi hizo,raisi huyo amesema hivi karibuni alimkaribisha raisi Elsisi wa Misri kwa madhumuni ya kuleta umoja baina ya nchi za kiislamu.Karibuni hivi atamkaribisha raisi Bashar Al Assad wa Syria ili kurudisha ushirikiano kati ya mataifa yao ambao ulidorora kimakosa miaka kadhaa iliyopita.
Mara baada ya tamko hilo waziri wa mambo ya nje wa Israel amekemea mpango huo na kusema watafanya uchunguzi juu ya raia wa Uturuki mwenye uraia pia wa kimarekani kuuliwa na askari wa Israel eneo la ukingo wa magharibi.
Syria ni moja ya mataifa yanayoizunguka Israel ambayo imekuwa ikidai maeneo yake yanayoshikiliwa na Israel.Vile vile nchi hiyo imekuwa ikipigwa na Israel kama inavyotaka kama sehemu ya kufanyia majaribio silaha zake na kwa ajili ya kuidhoofisha nchi hiyo kijeshi.
Kwa upande wa Uturuki ni moja ya mataifa yenye teknolojia kubwa za kijeshi duniani ambalo hapo zamani Uislamu uliwahi kuwa na makao yake makuu eneo hilo enzi za utawala wa Ottoman uliodumu karne kadhaa.