Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Mimi naiheshimu sana nchi ya Uturuki ambako nimekaa kidogo na kuwa ni taifa lenye historia muhimu kwetu waislamu.Zaidi ya hivyo ni nchi yenye kujali sana kuwaendeleza watu wake.Hata ukisikia uchumi umeyumba usidhani ni kama kuyumba kwa uchumi wa nchi zetu za kiafrika. Ukisikia hivyo basi ukiwa Uturuki unaweza ukala na kushiba bure kila siku ikabaki kuoga na kulala tu.
Pamoja na hayo kuingia kwa raisi wa chama cha mrengo wa kiislamu Erdogan kumebadili sana sera zilizokuwa na uhasama mkubwa na imani halisi ya kihistoria ya watu wake ambayo ni uislamu,Lakini raisi huyu amekuwa ni mtu asiyetabirika kabisa hasa katika mahusiano yake na nchi za nje.
Wakati alipouliwa Jamal Kashogi aliyekuwa mchumba wa raia wake wa kituruki na Uturuki kuwa na video za mauwaaji hayo tulidhani Uturuki isingerudisha uhusiano na Saudi Arabia mpaka hukumu ya tukio hiyo itolewe.
Yako mengi lakini kubwa kwa sasa ni huu uhusiano na Urusi na Ukraine. Mara nyingi inaonekana kama kwamba Uturuki ipo karibu zaidi na Urusi katika vita vinavyoendelea baina yake na Ukraine.Wakati vita vinaendelea mara nyingi Erdogan amekuwa akimualika raisi Putin kwa mazungumzo.
Wakati akifanya hivyo Uturuki ndiyo nchi iliyoiuzia Ukraine droni hatari za Bayaktar na ndizo zilizochangia kuitia hasara kubwa urusi katika msafara wa vifaru vilivyokuwa vikielekea Kyiv mwanzoni huko kwa vita.
Mara ikatiliana saini na Urusi kujenga kitujo kikubwa cha kuuza mafuta ya Urusi ili kuisaidia kukwepa vikwazo vya nchi za magharibi katika biashara hiyo na baadae ikafuatia mkataba wa kuuza ngano za Ukraine ili kuisaidia kiuchumi baada ya bandari zake zote kushikiliwa na Urusi.
Baada ya jeshi la Ukraine kushindwa kwenye mapambano ya Azovstal kule Mariupol na vikosi vyoke kuzingirwa na jeshi la Urusi nchi ya Ukraine ilisalimu amri lakini kwa kutaka kuwaokoa makamanda wake na wanajeshi waliobaki hai wakiwa wamekondeana kwa njaa. Uturuki ilikubali kuwachukua makamanda wake kwa makubaliano na Urusi kwamba watabaki huko milele.
Inashangaza juzi raisi Zelensky amekwenda Uturuki ghafla kuonana na riaisi Erdogana.Tangazo la kigeugeuj lililotolewa wazi katika mkutano huo ni Uturuki kuiunga mkono Ukraine kujiunga na NATO juu ya kwamba hilo ni chanzo kikuu cha vita vinavyoendelea.Kumbe hilo lilikuwa ni dogo.
Kubwa ni kuwa kumbe raisi Zelensky amerudi na makamanda wote waliobaki hai na kupelekwa nchini humo kwa mkataba maalum na Urusi. Hilo limetangazwa wakati Zelensky akiwa amerudi Kyiv na makamanda hao wakiwa wamenenepa na huenda tayari kuongoza tena mapambano na Urusi.