Erdogan anaongoza kwa kuwa Rais Ndumilakuwili duniani

Erdogan anaongoza kwa kuwa Rais Ndumilakuwili duniani

Halafu anajiona the smartest person in the room.
Mda mwingine mjinga unamuangalia tu
Bongo tuna majasusi wa viwango vya juu sana, mtu mpaka anagundua habari ya marekani kutengeneza tetemeko [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hapo wapi pameandikwa marekani imesababisha tetemeko uturuki?

Suala la earthquakes kusababishwa na human causes hilo linaeleweka.

Weka ushahidi wa marekani kusababisha tetemeko la uturuki.

Sio ujitungie tu theory zako kisa umeona "can be caused by humans" halafu unakuja kumwaga humu as a fact.

Weka ushahidi na details zinazoi link marekani na tetemeko la uturuki tuuchambue.
 
Achana nae huyo Kilasa.Uturuki ipo kwenye Faults ,inafahamika kabisa Tectonic movements pale ziko active ,ndo maana kuna matetemeko.
 
Turkiye kasema kuwa ataruhudu Sweden ijiunge NATO kama Maongezi kuhusu Turkiye kuwa EU yakirudishwa
Anatamani EU,anataka mahela ya EU.Kamwe EU hawawezi ruhusu Uturuki iingie EU.Wakifanya hivyo basi nchi kama France mwanzilishi wa EU watajitoa ,nchi nyingi za mlengo wa kulia kama Hungary zitajitoa EU.Halafu EU ili ujiunge lazima wanachama wote wakubali. Nchi hata moja tu ikiweka Veto,basi hauingii EU.Bora Sweden isiingie Nato kuliko Uturuki kuingia EU.
 
Uturuki anacheza both sides Kwa maslahi yake...wala sio unafiki....

Hao NATO waliizuia Uturuki kuingia European Union kisa ni dini tu...
Wakati wako nao NATO...

Wamarekani wamesababisha tetemeko ili Erdogan atoke na wameshindwa
Mkuu unajua tuna kuheshimu ilo tetemeko lilisababishwaje na marekani?
Uje na ushahidi usio tia shaka unapo toa tuhuma kama hizi
 
Turkiye kasema kuwa ataruhudu Sweden ijiunge NATO kama Maongezi kuhusu Turkiye kuwa EU yakirudishwa
Yap!...wajanja sana hawa Waturuki ila sio watu wenye msimamo, Erdogan alimuandama sana MBS baada ya mauaji ya Khashogi ila baadae alilegea kilaini tu na kesi ya wahusika ilishaisha.

Ila US akiongeza shinikizo kwa Turkiye kuiruhusu Sweden......... Erdogan atalegeza msimamo na kuiruhusu Sweden kujiunga hata kama EU watagomea ombi lake.

Victoire
 
Turkiye kasema kuwa ataruhudu Sweden ijiunge NATO kama Maongezi kuhusu Turkiye kuwa EU yakirudishwa
Kama wanataka Sweden iingizwe NATO na yeye aingizwe EU.Kumbuka Turkey ina kura ya veto katika NATO. lazima wakae hao.
 
Yap!...wajanja sana hawa, tungoje tuone kama EU watakubali..

Ila US akiongeza shinikizo kwa Turkiye.... Erdogan atalegeza msimamo na kuiruhusu Sweden kujiunga hata kama EU watagomea ombi lake.

Victoire
EU hawawezi ruhusu Uturuki kuingia EU. Bora Sweden asiingie NATO. Ujue ili uingie EU lazima wanachama wote 27 wakubali.Simuoni Poland,Hungary, France wakikubali.
 
EU hawawezi ruhusu Uturuki kuingia EU. Bora Sweden asiingie NATO. Ujue ili uingie EU lazima wanachama wote 27 wakubali.Simuoni Poland,Hungary, France wakikubali.
Erdogan na Uturuki ni rahisi sana kubadili misimamo yao, mwishowe Sweden itaingia NATO tu.
 
Achana nae huyo Kilasa.Uturuki ipo kwenye Faults ,inafahamika kabisa Tectonic movements pale ziko active ,ndo maana kuna matetemeko.
Hata ikitokea mlipuko wa volcano, mafuriko, kimbunga tutaambiwa marekani kasababisha [emoji1787][emoji1787]

Ujinga mtupu.
 
We mrundi na wewe member wa EU?[emoji28] ..
Eti hatuwataki...tayari Ulaya yote Islam ndo second religion na fastest in growing... Ufaransa timu ya taifa nusu or more are Muslims...

Waislam majina au maana wametoboa had masikio.
 
Mimi naiheshimu sana nchi ya Uturuki ambako nimekaa kidogo na kuwa ni taifa lenye historia muhimu kwetu waislamu.Zaidi ya hivyo ni nchi yenye kujali sana kuwaendeleza watu wake.Hata ukisikia uchumi umeyumba usidhani ni kama kuyumba kwa uchumi wa nchi zetu za kiafrika. Ukisikia hivyo basi ukiwa Uturuki unaweza ukala na kushiba bure kila siku ikabaki kuoga na kulala tu.

Pamoja na hayo kuingia kwa raisi wa chama cha mrengo wa kiislamu Erdogan kumebadili sana sera zilizokuwa na uhasama mkubwa na imani halisi ya kihistoria ya watu wake ambayo ni uislamu,Lakini raisi huyu amekuwa ni mtu asiyetabirika kabisa hasa katika mahusiano yake na nchi za nje.

Wakati alipouliwa Jamal Kashogi aliyekuwa mchumba wa raia wake wa kituruki na Uturuki kuwa na video za mauwaaji hayo tulidhani Uturuki isingerudisha uhusiano na Saudi Arabia mpaka hukumu ya tukio hiyo itolewe.
Yako mengi lakini kubwa kwa sasa ni huu uhusiano na Urusi na Ukraine. Mara nyingi inaonekana kama kwamba Uturuki ipo karibu zaidi na Urusi katika vita vinavyoendelea baina yake na Ukraine.Wakati vita vinaendelea mara nyingi Erdogan amekuwa akimualika raisi Putin kwa mazungumzo.

Wakati akifanya hivyo Uturuki ndiyo nchi iliyoiuzia Ukraine droni hatari za Bayaktar na ndizo zilizochangia kuitia hasara kubwa urusi katika msafara wa vifaru vilivyokuwa vikielekea Kyiv mwanzoni huko kwa vita.

Mara ikatiliana saini na Urusi kujenga kitujo kikubwa cha kuuza mafuta ya Urusi ili kuisaidia kukwepa vikwazo vya nchi za magharibi katika biashara hiyo na baadae ikafuatia mkataba wa kuuza ngano za Ukraine ili kuisaidia kiuchumi baada ya bandari zake zote kushikiliwa na Urusi.

Baada ya jeshi la Ukraine kushindwa kwenye mapambano ya Azovstal kule Mariupol na vikosi vyoke kuzingirwa na jeshi la Urusi nchi ya Ukraine ilisalimu amri lakini kwa kutaka kuwaokoa makamanda wake na wanajeshi waliobaki hai wakiwa wamekondeana kwa njaa. Uturuki ilikubali kuwachukua makamanda wake kwa makubaliano na Urusi kwamba watabaki huko milele.

Inashangaza juzi raisi Zelensky amekwenda Uturuki ghafla kuonana na riaisi Erdogana.Tangazo la kigeugeuj lililotolewa wazi katika mkutano huo ni Uturuki kuiunga mkono Ukraine kujiunga na NATO juu ya kwamba hilo ni chanzo kikuu cha vita vinavyoendelea.Kumbe hilo lilikuwa ni dogo.

Kubwa ni kuwa kumbe raisi Zelensky amerudi na makamanda wote waliobaki hai na kupelekwa nchini humo kwa mkataba maalum na Urusi. Hilo limetangazwa wakati Zelensky akiwa amerudi Kyiv na makamanda hao wakiwa wamenenepa na huenda tayari kuongoza tena mapambano na Urusi.

Ngoja waandae jaribio lingine la kumpindua
 
Yap!...wajanja sana hawa Waturuki ila sio watu wenye msimamo, Erdogan alimuandama sana MBS baada ya mauaji ya Khashogi ila baadae alilegea kilaini tu na kesi ya wahusika ilishaisha.

Ila US akiongeza shinikizo kwa Turkiye kuiruhusu Sweden......... Erdogan atalegeza msimamo na kuiruhusu Sweden kujiunga hata kama EU watagomea ombi lake.

Victoire

Sio kwamba hawana msimamo, wanaangalia maslahi yao yakowapi. In this modern times nchi huwa zinangaalia nani anawafaidisha bila kujali wanamuumi nani
 
Back
Top Bottom