Erdogan anaongoza kwa kuwa Rais Ndumilakuwili duniani

Erdogan anaongoza kwa kuwa Rais Ndumilakuwili duniani

Umekasirika kweli... wachezaji Saba Tu wamekuuma...hebu nenda katoe pongezi kule Kwa Kardinali mpya...ukimaliza uanzishe thread ya kumtukana Samia 🤣
Utapata nafuu I am sure
Hehehe,unaota shekhe.Samia nimtukane wa nini sasa?Mimi ninaongea mara moja then ninaendelea na mishe zangu za kujenga Taifa Tanganyika. Huyo nitamsema akibugi tena.
 
Yaani lijinga hili.NATO na EU wapi na wapi?Kwenye NATO kuna US,Canada ambao hata hawapo bara la Ulaya. Mzee hajui NATO kwa nini ilianzishwa,na nini?Hivi atajua USSR kweli?Halafu ana udini jamaa.
Ana udini kuliko wewe?.
 
Mimi naiheshimu sana nchi ya Uturuki ambako nimekaa kidogo na kuwa ni taifa lenye historia muhimu kwetu waislamu.Zaidi ya hivyo ni nchi yenye kujali sana kuwaendeleza watu wake.Hata ukisikia uchumi umeyumba usidhani ni kama kuyumba kwa uchumi wa nchi zetu za kiafrika. Ukisikia hivyo basi ukiwa Uturuki unaweza ukala na kushiba bure kila siku ikabaki kuoga na kulala tu.

Pamoja na hayo kuingia kwa raisi wa chama cha mrengo wa kiislamu Erdogan kumebadili sana sera zilizokuwa na uhasama mkubwa na imani halisi ya kihistoria ya watu wake ambayo ni uislamu,Lakini raisi huyu amekuwa ni mtu asiyetabirika kabisa hasa katika mahusiano yake na nchi za nje.

Wakati alipouliwa Jamal Kashogi aliyekuwa mchumba wa raia wake wa kituruki na Uturuki kuwa na video za mauwaaji hayo tulidhani Uturuki isingerudisha uhusiano na Saudi Arabia mpaka hukumu ya tukio hiyo itolewe.
Yako mengi lakini kubwa kwa sasa ni huu uhusiano na Urusi na Ukraine. Mara nyingi inaonekana kama kwamba Uturuki ipo karibu zaidi na Urusi katika vita vinavyoendelea baina yake na Ukraine.Wakati vita vinaendelea mara nyingi Erdogan amekuwa akimualika raisi Putin kwa mazungumzo.

Wakati akifanya hivyo Uturuki ndiyo nchi iliyoiuzia Ukraine droni hatari za Bayaktar na ndizo zilizochangia kuitia hasara kubwa urusi katika msafara wa vifaru vilivyokuwa vikielekea Kyiv mwanzoni huko kwa vita.

Mara ikatiliana saini na Urusi kujenga kitujo kikubwa cha kuuza mafuta ya Urusi ili kuisaidia kukwepa vikwazo vya nchi za magharibi katika biashara hiyo na baadae ikafuatia mkataba wa kuuza ngano za Ukraine ili kuisaidia kiuchumi baada ya bandari zake zote kushikiliwa na Urusi.

Baada ya jeshi la Ukraine kushindwa kwenye mapambano ya Azovstal kule Mariupol na vikosi vyoke kuzingirwa na jeshi la Urusi nchi ya Ukraine ilisalimu amri lakini kwa kutaka kuwaokoa makamanda wake na wanajeshi waliobaki hai wakiwa wamekondeana kwa njaa. Uturuki ilikubali kuwachukua makamanda wake kwa makubaliano na Urusi kwamba watabaki huko milele.

Inashangaza juzi raisi Zelensky amekwenda Uturuki ghafla kuonana na riaisi Erdogana.Tangazo la kigeugeuj lililotolewa wazi katika mkutano huo ni Uturuki kuiunga mkono Ukraine kujiunga na NATO juu ya kwamba hilo ni chanzo kikuu cha vita vinavyoendelea.Kumbe hilo lilikuwa ni dogo.

Kubwa ni kuwa kumbe raisi Zelensky amerudi na makamanda wote waliobaki hai na kupelekwa nchini humo kwa mkataba maalum na Urusi. Hilo limetangazwa wakati Zelensky akiwa amerudi Kyiv na makamanda hao wakiwa wamenenepa na huenda tayari kuongoza tena mapambano na Urusi.

Kwa dunia ya leo nadhani wako sahihi, wanaweka mbele maslahi ya taifa lao✌🏿 Hilo ni jambo zuri na muhimu zaidi.
 
Uturuki anacheza both sides Kwa maslahi yake...wala sio unafiki....

Hao NATO waliizuia Uturuki kuingia European Union kisa ni dini tu...
Wakati wako nao NATO...

Wamarekani wamesababisha tetemeko ili Erdogan atoke na wameshindwa
Marekani wamesababisha tetemeko?

Wabongo bana.
 
Uturuki anacheza both sides Kwa maslahi yake...wala sio unafiki....

Hao NATO waliizuia Uturuki kuingia European Union kisa ni dini tu...
Wakati wako nao NATO...

Wamarekani wamesababisha tetemeko ili Erdogan atoke na wameshindwa
We jamaa kumbe akili huna
Achana na udini
 
Uturuki ipo kwenye ukanda wa tetemeko na huwa inayapata mara kadhaa, hata Iran ndio iko eneo hatari zaidi kwenye weak joints za earth's crust. Na Japan nayo iko eneo hatari la tectonic plates za baharini. Hivyo Uturuki na Iran kupata matetemeko sio suala la ajabu wala Japan kupata tsunami halitafutiwi mchawi.

Hayo matukio yana mamilioni ya miaka yanatokea. Marekani yenyewe inakumbwa na dhoruba na tufani mara nyingi tu. Mambo ya kusingizia HAARP kwa matukio ya kijiografia ni conspiracy theories, no evidence at all.


Huwa kuna watu wakiongea tunaamua tu kuwasikiliza wakijiona ni wenye maarifa.
Haina tofauti na obama akihojiwa kwenye na ellen degeneres pamoja na matty presidential expert huyu mtoto akaulizwa kuhusu kuwepo kwa alien akasema wapo na tunafanya nao KAZI.
Hizo ni conspiracy theory ambazo hazina ushahidi wowote wajinga kama hao ndo huja kudanganya watu.
 
We jamaa kumbe akili huna
Achana na udini
....
Screenshot_2023-07-10-17-31-10-526_com.android.chrome.jpg
 
Hiyo ndio hofu yenu, Ila Uturuki ina maendeleo makubwa sana kuliko baadhi ya EU members, sasa uoga wa nini ?

Tena inawasaidia kuzuia immigrants wasifike kwenu ila wao hamuwataki kabisa.
Watawakubali kwa shinikozo la US
 
Sisi hatuwezi kitu. Aje mwarabu, aje mhindi, aje muisraeli ni mikataba ya hovyo na kuibiwa tu.
Huwa tunasingizia wakija wataleta ajira wakati mkataba ukiwa mzuri hats wakihiajiri wenyewe bila wazawa bado gavoo itapata ela ndefu
 
Tupo 2023.Halafu source yako ni google. Mfyuuuu. KYLIAN NI MKRISTO. Halafu hao uliowataja ni kati ya wachezaji 25. Halafu France waislam wapo million 5 tu kati ya population ya watu million 67 France. Chefuuuuuu.
Huyu jamaa mdini sana hivyo jipange
 
Yaani lijinga hili.NATO na EU wapi na wapi?Kwenye NATO kuna US,Canada ambao hata hawapo bara la Ulaya. Mzee hajui NATO kwa nini ilianzishwa,na nini?Hivi atajua USSR kweli?Halafu ana udini jamaa.
Unabishana na wajinga wa madrasa
 
Back
Top Bottom