Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Rais wa Uturuki ndugu Tayeb Erdogan amesema nchi yake inakusudia kuingia ndani ya Israel kuwasaidia wapalestina wanaouliwa na Israel.
Hayo aliyasema kwenye mji aliozaliwa wa Rize wakari akizungumza na wanachama wa chama chake cha AK chenye kufuata mrengo wa dini ya kiislamu.
Akifafanua kusudio hilo,Erdogan amesema hilo ni jambo jepesi kwa nchi yake yenye teknolojia kubwa za kivita kama ambavyo wamewahi kufanya huko Nagoro Karabakh na Libya ambapo matokeo yalionekana.
Serikali ya umoja wa kitaifa inayoongoza sasa nchini Libya na kutambuliwa na umoja wa mataifa imedumu madarakani baada ya Uturuki kuingilia kati na kuiunga mkono kwa kuilinda dhidi ya wapinzani wake.
Hatua hiyo ya Uturuki japo itakuja katika muda wa kuchelewa lakini ni yenye kuhitajika sana kutokana na dhulma kwa wapalestina na tishio dhidi ya msikiti wa Alaqsa.
Kwa upande mwengine Uturuki ina uwezo huo japo mara nyengine huwa inakuwa na kigeugeu kisichokuwa na sababu kwenye maamuzi yake.