Iran level za kwenda front na Israel anazo kwasababu mbili ama tatu;
-Ana medani nzuri kivita,kuhimili vita ya miaka nane na kushinda dhidi ya jeshi la Saddam Hussein linalosaidiwa Na USA sio jambo dogo.
-Iran ana missile power kubwa kushinda hata Israel.
Iran majenerali wake wanauwawa na Israel. Mbona haendi frontline? Kama uwezo anao ataenda lini sasa.
Kuhimili miaka 8 hata Iraq iliweza. Hapo Iran ilitumia US made weapons kama F-14 Tomcats na F-5 Phantom ingawa ilinyimwa spare parts ila ilifanya kuhamisha spares.
Suala la kusaidiwa ni silaha gani ya Marekani ilienda Iraq kama msaada? Haipo.
Wakati Iran wao walikuwa na nchi kama Chinaz Yugoslavia, Bulgaria, North Korea (ambako ndio walitoa missile technology) na wengine. Hata Iraq naye alikuwa na nchi za kumuunga mkono, mbona unaandika as if Iran ilikuwa peke yake.
Alafu kama ni suala la missile power mbona Israel ina nukes. Sasa maelfu ya makombora ya Iran yanamtisha nani wakati ukijifanya kuyatumia unajibiwa na nuclear strike moja utulie.
Israel hana uwezo wa kumuondoa Assad pale hata akitaka hana uwezo.
Kama Hizbollah amemshindwa atamuweza Iran!?
Israel imekua ikipigwa katika street battles na Hamas video zimekua zikisambaa mkuu IDF wanakimbia street battle na Hamas.
Kwahiyo Iran itapigana street battles na Israel alafu ishinde? Israel inashinda wars, sio battles. Hapo Gaza nani kamkimbia mwenzie. Nani amevuruga mji wa mwenzie na vita inapiganiwa wapi. Yani Israel wameamuru watu zaidi ya milioni wa Gaza wahame na wametii, wamelipua makazi, wameua zaidi ya watu 39,000 na hapo ni bila kukusudia kama ambavyo Hamas wanadhamiria kabisa kuua. Alafu unasema street battles Israel inakimbia. Kama ingekuwa inakimbia hizo streets zingekuwa hivi?
Hapa katika silaha mkuu hapa patizame vizuri,umeteleza.
Silaha za Iran ziko more offensive,hivi unajua ile Drone ilopenya Tel Aviv pasi na kugunduliwa ni Iranian made!?
Unajua drone iliyoiona helicopter ya Raisi iliyodondoka milimani ni ya wapi na ilitumia muda gani. Baada ya Iran kutumia masaa mengi siku nzima bila mafanikio wakaomba msaada Uturuki, ikaja Akinci drone ikatumia 2 and ½ hours ikatumia sensors zake ikaona kwenye ukungu na gizani. Wairan wana drones hazina hata NV likiingia giza au ukungu hamna kitu.
Iran anaonekana sababu analazimisha aonekane, kwamba kisa hujawahi ona silaha za South Korea zinatumika basi hazina uwezo. Uturuki ina silaha bora maradufu kuliko za Iran ila tu haina fujo.
Tofautisha kuwa na fujo na kuwa na nguvu.
Silaha za Iran zimeonesha ubora sehemu nyingi hususan Lebanon,Yemeni na Syria na Russia pia.Iran ina silaha offensive kuliko Israel.Mbaya zaidi Israel airdefense system zake za iron dome zimeonesha udhaifu mkubwa sana mkuu.
Nitajie air defense system yeyete duniani yenye effectiveness percentage kubwa kuliko Iron Dome. Itaje na useme success rate yake niko nasubiri.
Sijaona hata iwe Patriot, S-400, S-300 wala nani. Kama unaijua ilete nami nilete numbers za Iron Dome.
Hakuna nchi inayopenda vita ila kama ukiigusa Iran huwezi ukasalimika lazima italipiza kisasi.
Israel unayojaribu kuizungumzia hapa mkuu uvamizi wa Hamas imetumia wanajeshi laki tatu na silaha nyingi kiasi cha kuomba misaada ya silaha USA na wote tunajua na ushahidi tunao kuwa USA ilituma meli vita ikiwa na askari 2000 na silaha za kutosha kwenda Israel.
Askari 2,000 ni kitu gani kwenye vita ya taifa. Hiyo si ni infantry brigade moja ya Israel.
Hamas hupokea silaha vilevile, Israel silaha imenunua.
Hao wanajeshi laki tatu walikuwa mobilized in case Waarabu watajiunga iwe total war. Yalikuwa maandalizi maana Iran ilijifanya inataka kuwapanda kichwani. Brigades zinazotumika Gaza hata 10 hazifiki, hao wanajeshi 300,000 walikuwa vitani wapi.
Sasa tujiulize kama Israel imetumia nguvu hiyo kupigana na Hamas wenye wapiganaji elfu 30 je itatumia nguvu kiasi gani kupigana na jeshi lenye wanajeshi zaidi ya laki 6 kama Iran!?
Jinsi ambavyo Israel ilipigana na jeshi la Egypt na Syria yaliyokuwa na wanajeshi mara 2 zaidi ya Israel. Ndivyo ambavyo Iran itakuwa. Wanajeshi 600,000 wa Iran hawapakani na Israel, je:
Watakuja kwa ungo vitani?
Wataenda kwa airlifters, zipi? Kwanza wana paratroopers wangapi Iran na mazoezi hufanyia wapi maana zana hizo hawana.
Wataenda kwa magari, Israel ina air dominance si itawachoma moto kabla hata hawajakanyaga ardhi yake?
Watavuka ardhi wapitie Iraq, itawaruhusu? Ikiwarusu si inakuwa mshirika wa vita na ina haki ya kupigwa. Iraq ikubali kuua nchi yake kisa Iran.
2006 turejee vita ya Hizbollah na IDF,IDF ilitumia silaha nyingi na makamanda wengi ila wakashindwa kuipoteza bint jubeir mbele ya kundi dogo la Hizbollah.
Israel iliteka maeneo ya Lebanon tangu miaka ya 1980s mpaka mwaka 2000 baada ya Barak kushinda uchaguzi na aliahidi kuiondoa Israel Lebanon. Sijajua hiyo occupation ya 2006 ilikuwaje, hata hivyo kama Hezbollah wanajiweza uwanja upo wazi wajaribu. Maana kupigana kwao ni ushujaa na sifa.
-Border clash mkuu usizidharau,maana ile haikuwa vita ya mipakani tu bali ni vita ya kugombania eneo zima la KASHMIR mkuu.Ni sawa na vita ya Nagorno-Karabakh,vita ya kugombania eneo sio sawa na kugombania kilometa za mpaka.
India iliipiga Pakistan ikaitenga Bangladesh. Hakuna vita ambayo Pakistan iliishinda India, alafu mkuu hivi kwa akili yako kabisa unaiona India hii ni ya kushindwa na Pakistan???
Yaani ukitazama uchumi, ubora na idadi ya silaha, jeshi, population, budget, teknolojia, landmass. Unaona ni kipi Pakistan inaizidi India?
-Afghanistan inaongozwa na Taliban mkuu,Taliban ndilo kundi lililovunja USSR mkuu,tena ni kundi ambalo ukilipia silaha lina ari kubwa ya vita kuliko idhaniavyo,mbaya zaidi huwezi kumaliza vita kwa fighter jets peke yake au missiles peke yake,askari wa ardhini lazima wahusike,katika hilo nadhani mkuu ushahidi upo kuwa Israel ground battle ni weupe.
Taleban walikaliwa na Marekani kwa miaka 20 mpaka pale Trump alipoamua kuondosha majeshi yake. Taliban ilipigwa na coalition iliyokuwa na wanajeshi 5,000 wa Marekani.
Yaani Marekani ilitumia Brigade moja kuipiga Taleban kwa miezi miwili, sasa jeshi linalopigwa na brigade moja ya Marekani ni kitu gani mbele ya Israel?
Tangu mwaka 2001 Marekani wamekaa wee hapo Afghanistan mpaka wakasahau kwanini walienda, siasa zao zikaamua waondoke mwaka 2021.
Uliona lile shambulio la Iran dhidi ya Israel la kulipiza kisasi mkuu?
Madhara gani yalitokea, silaha zipi ziliharibiwa, vifo vingapi mkuu. Israel iliua majenerali watatu, aya sasa Iran ili-achieve nini.
Iran alirusha kwanza drones zilizoihadaa air defense system ya Israel kesha akarusha ballistic missiles na yapo yaliyopenya licha ya kuwa USA na UK Walishiriki kuyadungua.
Sasa tujiulize kama wafadhili wakikaa pembeni hivi Israel atakuwa na uwezo wa kudungua missile power ya Iran!?
Yaliyopenya yalifanya nini. Hivi unajua F-35 Adir za Israel zina command link inayoweza elekeza SAM site ya ardhini ifanye lock-on kwenye aerial target na kufanya interception? Hiyo ni ndoto kwa Iran.
Israel inaweza shoot ballistic missile kwa kutumia AH-64 Apache na fighter jets. Iran inaweza?
Then baada ya hapo unajua Israel ilifyatua air launched ballistic missile na likapenya anga la Iran, na likaacha missile booster Iraq. Iran inaweza?
Makombora ya Iran yana uzito wa makumi ya tani na yanabebwa na launchers nzito kama semi trucks, sasa Israel ina kombora ambalo hata tani halifiki ila linarushwa na fighter jet linapita Iraq linaingia Iran. Na liko very resistant na jamming, ni dogo na precise. Huogopi?
Iraq kuna vikundi vingi vya mujahiddin Israel hawezi kuteka eneo hata punje la Iraq.
Hata akiamua kuteka na kupenyeza askari kuja Iran kupigana vita ya ardhini Israel hana medani hiyo ya vita mbele ya Iran ambayo imehimili vita ya miaka nane ikichangiwa na Iraq na USA.
Iraq kuna Washia na Wasuni almost nusu kwa nusu. Wasuni hawaitaki Iran na wakipata nafasi wataipinga.
Iran ina majimbo yanataka kujitenga, ni kuwapa silaha waanzishe proxy muda huohuo Iran iko busy na Israel.
Israel hawezi pigana miaka vita ya kufa na kupona, ni miezi kadhaa ikizidi. Achana na operation ya Gaza.
Israel bado sana kupimana ubavu na Iran mkuu.
Iran hii ambayo iliipa mafunzo Houthi kundi dogo lililosumbua Saudi Arabia na USA ndio Iran hii hii iliyoisaidia Hizbollah 2006 kumfukuza Israel pale bint jubeir kwa mapigano sio kwa mkataba au makubaliano.
Unaisema Israel ambayo inafanya airstrikes nyingi Syria na wana air defense systems wamenunua Russia ila kila muda huwa hawajui nini kimetokea angani kwao. Wairan wenyewe wahanga huwa wanapigwa sana Syria wakiwa wanapeleka shehena ya silaha kwa makundi.
Na vita ya makombora ni hatari zaidi ya vita vya ndege,na hata vyombo vya usalama vya kimataifa vimethibitisha kuwa silaha za Iran zina uwezo na athari kubwa maana zimetumika sehemu mbali mbali na zimeonesha matokeo chanya.
Kwani mkuu Israel haina makombora? Jericho I, Jericho II, Jericho III zote hizo ni ICBM. Nitajie ICBM hata moja ya Iran nasubiri hapa.
Israel ina nuclear warheads, ina submarines na zinaweza kufyatua makombora. Iran haina vyote hivyo.
Iran ina ballistic missiles nyingi ambazo ikifyatua kama mvua inajibiwa na nuke strike. Mjanja nani hapo.
Kuhusu silaha za UTURUKI sina ujuzi sana kaka,labda niende nikachunguze ndio nitarudi hapa kuelezea.Ila PKK kila leo wanapigwa na kukamatwa hawaisumbui Uturuki kihivyo.
Haphapo kwa Uturuki, kwa kuwa PKK haijaisha basi Uturuki ina jeshi bovu si ndio unamaanisha ambavyo Hamas haijaisha basi Israel mbovu?
Sasa Wakurdi wako Syria, walimsaidia Assad kupigana na ISIS. Alipowalipa fadhira akawafuga na PKK wakaishambulia Uturuki. Basi Uturuki ikaja Kaskazini mwa Syria ikampiga vibaya na silaha zake za Urusi na Wakurdi wake. Si ndipo Urusi ikafanya mkataba na Uturuki kufanya ukaguzi wa pamoja na mapigano yakaisha. Bila hivyo Syria ingepigwa vibaya.
Sasa huoni PKK wakiwa Uturuki wanavaa kiraia, wakija Syria bwana wao anapigwa sembuse wao.
Chukua Hamas wavalishe sare, wape kambi za jeshi watoke kwenye makazi na mahospitalini. Wape mwezi uone kama watakaa frontline. We unadhani kwanini siku zote hudai Israel inauwa wanawake na watoto. Wao Hamas huwa wanakuwa wapi.
Iran ikipigana na Israel hakuna kukaa mafichoni, hakuna kuvaa kanzu ukaficha grenade mfukoni ukategeshea troops wa Israel wakitazama nyuma wakidhani wewe ni raia mwema ndio uwalipue. Unavaa gwanda uonekane ni IRGC au regular forces utuambie jinsi Israel ilivyo mbovu.