Iran majenerali wake wanauwawa na Israel. Mbona haendi frontline? Kama uwezo anao ataenda lini sasa.
Kuhimili miaka 8 hata Iraq iliweza. Hapo Iran ilitumia US made weapons kama F-14 Tomcats na F-5 Phantom ingawa ilinyimwa spare parts ila ilifanya kuhamisha spares.
Suala la kusaidiwa ni silaha gani ya Marekani ilienda Iraq kama msaada? Haipo.
Wakati Iran wao walikuwa na nchi kama Chinaz Yugoslavia, Bulgaria, North Korea (ambako ndio walitoa missile technology) na wengine. Hata Iraq naye alikuwa na nchi za kumuunga mkono, mbona unaandika as if Iran ilikuwa peke yake.
Alafu kama ni suala la missile power mbona Israel ina nukes. Sasa maelfu ya makombora ya Iran yanamtisha nani wakati ukijifanya kuyatumia unajibiwa na nuclear strike moja utulie.
Kwahiyo Iran itapigana street battles na Israel alafu ishinde? Israel inashinda wars, sio battles. Hapo Gaza nani kamkimbia mwenzie. Nani amevuruga mji wa mwenzie na vita inapiganiwa wapi. Yani Israel wameamuru watu zaidi ya milioni wa Gaza wahame na wametii, wamelipua makazi, wameua zaidi ya watu 39,000 na hapo ni bila kukusudia kama ambavyo Hamas wanadhamiria kabisa kuua. Alafu unasema street battles Israel inakimbia. Kama ingekuwa inakimbia hizo streets zingekuwa hivi?
Unajua drone iliyoiona helicopter ya Raisi iliyodondoka milimani ni ya wapi na ilitumia muda gani. Baada ya Iran kutumia masaa mengi siku nzima bila mafanikio wakaomba msaada Uturuki, ikaja Akinci drone ikatumia 2 and ½ hours ikatumia sensors zake ikaona kwenye ukungu na gizani. Wairan wana drones hazina hata NV likiingia giza au ukungu hamna kitu.
Iran anaonekana sababu analazimisha aonekane, kwamba kisa hujawahi ona silaha za South Korea zinatumika basi hazina uwezo. Uturuki ina silaha bora maradufu kuliko za Iran ila tu haina fujo.
Tofautisha kuwa na fujo na kuwa na nguvu.
Nitajie air defense system yeyete duniani yenye effectiveness percentage kubwa kuliko Iron Dome. Itaje na useme success rate yake niko nasubiri.
Sijaona hata iwe Patriot, S-400, S-300 wala nani. Kama unaijua ilete nami nilete numbers za Iron Dome.
Askari 2,000 ni kitu gani kwenye vita ya taifa. Hiyo si ni infantry brigade moja ya Israel.
Hamas hupokea silaha vilevile, Israel silaha imenunua.
Hao wanajeshi laki tatu walikuwa mobilized in case Waarabu watajiunga iwe total war. Yalikuwa maandalizi maana Iran ilijifanya inataka kuwapanda kichwani. Brigades zinazotumika Gaza hata 10 hazifiki, hao wanajeshi 300,000 walikuwa vitani wapi.
Jinsi ambavyo Israel ilipigana na jeshi la Egypt na Syria yaliyokuwa na wanajeshi mara 2 zaidi ya Israel. Ndivyo ambavyo Iran itakuwa. Wanajeshi 600,000 wa Iran hawapakani na Israel, je:
Watakuja kwa ungo vitani?
Wataenda kwa airlifters, zipi? Kwanza wana paratroopers wangapi Iran na mazoezi hufanyia wapi maana zana hizo hawana.
Wataenda kwa magari, Israel ina air dominance si itawachoma moto kabla hata hawajakanyaga ardhi yake?
Watavuka ardhi wapitie Iraq, itawaruhusu? Ikiwarusu si inakuwa mshirika wa vita na ina haki ya kupigwa. Iraq ikubali kuua nchi yake kisa Iran.
Israel iliteka maeneo ya Lebanon tangu miaka ya 1980s mpaka mwaka 2000 baada ya Barak kushinda uchaguzi na aliahidi kuiondoa Israel Lebanon. Sijajua hiyo occupation ya 2006 ilikuwaje, hata hivyo kama Hezbollah wanajiweza uwanja upo wazi wajaribu. Maana kupigana kwao ni ushujaa na sifa.
India iliipiga Pakistan ikaitenga Bangladesh. Hakuna vita ambayo Pakistan iliishinda India, alafu mkuu hivi kwa akili yako kabisa unaiona India hii ni ya kushindwa na Pakistan???
Yaani ukitazama uchumi, ubora na idadi ya silaha, jeshi, population, budget, teknolojia, landmass. Unaona ni kipi Pakistan inaizidi India?
Taleban walikaliwa na Marekani kwa miaka 20 mpaka pale Trump alipoamua kuondosha majeshi yake. Taliban ilipigwa na coalition iliyokuwa na wanajeshi 5,000 wa Marekani.
Yaani Marekani ilitumia Brigade moja kuipiga Taleban kwa miezi miwili, sasa jeshi linalopigwa na brigade moja ya Marekani ni kitu gani mbele ya Israel?
Tangu mwaka 2001 Marekani wamekaa wee hapo Afghanistan mpaka wakasahau kwanini walienda, siasa zao zikaamua waondoke mwaka 2021.
Madhara gani yalitokea, silaha zipi ziliharibiwa, vifo vingapi mkuu. Israel iliua majenerali watatu, aya sasa Iran ili-achieve nini.
Yaliyopenya yalifanya nini. Hivi unajua F-35 Adir za Israel zina command link inayoweza elekeza SAM site ya ardhini ifanye lock-on kwenye aerial target na kufanya interception? Hiyo ni ndoto kwa Iran.
Israel inaweza shoot ballistic missile kwa kutumia AH-64 Apache na fighter jets. Iran inaweza?
Then baada ya hapo unajua Israel ilifyatua air launched ballistic missile na likapenya anga la Iran, na likaacha missile booster Iraq. Iran inaweza?
Makombora ya Iran yana uzito wa makumi ya tani na yanabebwa na launchers nzito kama semi trucks, sasa Israel ina kombora ambalo hata tani halifiki ila linarushwa na fighter jet linapita Iraq linaingia Iran. Na liko very resistant na jamming, ni dogo na precise. Huogopi?
Iraq kuna Washia na Wasuni almost nusu kwa nusu. Wasuni hawaitaki Iran na wakipata nafasi wataipinga.
Iran ina majimbo yanataka kujitenga, ni kuwapa silaha waanzishe proxy muda huohuo Iran iko busy na Israel.
Israel hawezi pigana miaka vita ya kufa na kupona, ni miezi kadhaa ikizidi. Achana na operation ya Gaza.
Unaisema Israel ambayo inafanya airstrikes nyingi Syria na wana air defense systems wamenunua Russia ila kila muda huwa hawajui nini kimetokea angani kwao. Wairan wenyewe wahanga huwa wanapigwa sana Syria wakiwa wanapeleka shehena ya silaha kwa makundi.
Kwani mkuu Israel haina makombora? Jericho I, Jericho II, Jericho III zote hizo ni ICBM. Nitajie ICBM hata moja ya Iran nasubiri hapa.
Israel ina nuclear warheads, ina submarines na zinaweza kufyatua makombora. Iran haina vyote hivyo.
Iran ina ballistic missiles nyingi ambazo ikifyatua kama mvua inajibiwa na nuke strike. Mjanja nani hapo.
Haphapo kwa Uturuki, kwa kuwa PKK haijaisha basi Uturuki ina jeshi bovu si ndio unamaanisha ambavyo Hamas haijaisha basi Israel mbovu?
Sasa Wakurdi wako Syria, walimsaidia Assad kupigana na ISIS. Alipowalipa fadhira akawafuga na PKK wakaishambulia Uturuki. Basi Uturuki ikaja Kaskazini mwa Syria ikampiga vibaya na silaha zake za Urusi na Wakurdi wake. Si ndipo Urusi ikafanya mkataba na Uturuki kufanya ukaguzi wa pamoja na mapigano yakaisha. Bila hivyo Syria ingepigwa vibaya.
Sasa huoni PKK wakiwa Uturuki wanavaa kiraia, wakija Syria bwana wao anapigwa sembuse wao.
Chukua Hamas wavalishe sare, wape kambi za jeshi watoke kwenye makazi na mahospitalini. Wape mwezi uone kama watakaa frontline. We unadhani kwanini siku zote hudai Israel inauwa wanawake na watoto. Wao Hamas huwa wanakuwa wapi.
Iran ikipigana na Israel hakuna kukaa mafichoni, hakuna kuvaa kanzu ukaficha grenade mfukoni ukategeshea troops wa Israel wakitazama nyuma wakidhani wewe ni raia mwema ndio uwalipue. Unavaa gwanda uonekane ni IRGC au regular forces utuambie jinsi Israel ilivyo mbovu.