Majenerali wa Iran kuuliwa IRAN ALISHALIPIZA KILA KISASI CHA MAJENERALI WAKE KUULIWA.
Hili mbona nishalisema mkuu!?Hapa unarudia point ile ile,katika kila shambulio la Israel kuua jenerali wa Iran basi huwa linalipwa kwa shambulio la Hizbollah au Syria.
Na mbona ushahidi upo ukitaka unawekewa!?
Hata Iran consulate pale Syria ilivyolipuliwa Iran alilipa kisasi kwa kurusha makombora na drones 300+.
Na sababu za kutokwenda front nilishazitaja ngojea nizirudie tena;
-Iran ina struggle economically kwasababu ya kuwa na economic sanctions,hivyo uchumi huo sio mzuri kwa vita hata kiduchu.
-Iran ina maadui wengi ambao wanasubiri chanzo tu ili wamshambulie.Na kama akithubutu kuivamia Israel basi huwenda ndio mwisho wake maana kila taifa la Ulaya na USA wataweka full force ili kumuangusha,kwasababu tokea 1980 mpaka leo wanajaribu kufanya regime change pale Iran.
-Mwisho nilitaja ni umbali,umbali pia imesababisha moto kutokusambaa.
Usijifiche kichaka cha kuuawa kwa majenerali wa Iran hapo Syria,ilhali Iran Nae analipizaga kisasi kupitia hapo hapo Syria.Kama mtu wa kuingia frontline wa kwanza ni ISRAEL.
Kwasababu zifuatazo;
1)Amani ya Israel ipo mashakani kwa Syria kuwa command center ya vikundi vya kiasi vya Hamas,Hizbollah na Houthi.
2)Iran ndiye mfadhili wa mashambulizi ya Hizbollah dhidi ya Israel.Na hayo mashambulizi yameleta maafa makubwa Israel kwa kuleta vifo na ulemavu wa kudumu wa askari takriban 5000 kaskazini kwa Israel.
Hivyo hizi sababu mbili ni sababu kubwa tosha za Israel kumvamia Iran kuliko Iran kumvamia Israel.
Maana vita zote anazo kumbana nazo Israel mfadhili ni Iran.Je nani ana sababu kubwa ya kumvamia mwenzake!!??
Kuhusu vita ya Iraq na Iran,Iran ilikua ina jeshi dogo ambalo bado halikua stable maana ndio kwanza mwaka uliopita lilitoka kufanya mapinduzi.
Pia hayo mataifa ulotaja yalisaidia silaha tu ilhali Iraq ya Saddam Hussein ilisaidiwa kwa silaha na wanajeshi pia,na kwa kipindi kile inajulikana USA alikua baba wa majeshi na Iraq alikua baba wa majeshi middle east.
-Kuhusu missile power mkuu hivi unadhani nuclear inatumika tu kiwepesi!??
Kama ni hivyo basi Israel angeshapiga bomu pale Syria ambapo panatumika kama command center ya vikundi vyote vya uasi mashariki ya kati ambavyo vinaishambulia Israel kila leo.
Na Iran alishafikia hatua ya urutubishaji silaha na ripoti ilitoka,ndio maana USA na Israel kila leo wanakataa Iran kurutubisha vinu vya Nuke kwasababu wanajua kama akiyapata hakuna cha kumdhibiti tena middle east.
Israel hii unayoisemea wewe ambayo imeshindwa kuhimili vita ya miezi 9 tu.
Na tizama chini madhara iliyopata na hapo imepigana na Hamas tu pekee yake.
Sasa jiulize kama kundi dogo ambalo lina askari elfu 30 limewatia ulemavu je jeshi lenye watu zaidi ya laki 6 kitawafanya je!!??
View attachment 3056628View attachment 3056629
Mkuu unadanganya sana punguza uongo unadanganya sana punguza uongo bana.
Battle is synonymous to war hiyo ni linguistics.
Israel imekua ikilipua majengo hovyo kimakusudi na ushahidi umekua ukitolewa hapa,wakidai eti Hamas wanajificha humo ndani.
Wameua wanawake na watoto wasio na hatia.Ukitaka ushahidi nakuletea hapa we sema niulete.
Street battles vita za uso kwa uso ISRAEL AMESHINDWA GAZA NA WALEMAVU WENGI WA IDF WALIPATIKANA KATIKA VITA ZA MITAA KWA MITAA HAPO GAZA.
Wengi wakiwa wana matatizo ya saikolojia wengine wakiwa wamevunjwa miguu kwa grenade na risasi.
Ukitaka ushahidi nakuletea.
Watu kuhamishwa kutoka Central Gaza kwenda Khani younis ni kwa usalama wao ni sahihi kuhama,japo huko huko Khani younis imeripotiwa kuwa Israel imekua ikishambulia kimakusudi ilhali hakuna Hamas wala sign of Hamas huko.Ukitaka ushahidi nakuletea pia.
Hao askari wa IDF laki tatu waliletwa kwaajili ya kupambana na HAMAS wala usisingizie waarabu eti kama watajaribu kuungana ndio hilo jeshi litatumika.
Mbona wanajeshi waliisha na sasa hivi Israel imekua ikilazimisha raia kuingia jeshini??
Au hauna habari kaka kama Israel inalazimisha raia kuingia jeshini ili kupunguza uhaba wa askari!?
Hapo pia usisahau kaskazini kwa Israel haikaliki kwa mashambulizi madogo tu ya Hizbollah.
-Kuhusu suala la Iran kushindwa kumuokoa na kumpata rais wake hilo linafahamika kuwa Iran haijajipambanua katika teknolojia ya aerospace.Uturuki ni nchi ambayo imejipambanua sana katika teknolojia ya aerospace,kuna ndege yao inaitwa RAAD niliwahi ifuatilia ilivyo na ufanisi.
Ila kutokua na upembuzi katika teknolojia ya anga Iran haimaanishi haijiwezi kisilaha.Iran ilijikita katika uundaji ADS pamoja na ballistic missiles.Na middle east inafahamika Iran ameendelea katika masuala ya makombora.
Ana makombora ambayo yana uwezo wa kukwepa hata ADS ili yafikie lengo.Kwahiyo mtu kutokua vizuri sehemu ya anga haimaanishi hata sehemu zingine yuko vibaya.
Hii analysis hujaifanya vizuri kaka.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂Mkuu tuache utani na masihara.
Hii iron dome unayoisemea tarehe 7 October Hamas walirusha roketi tena ni homemade roketi zilizoundwa na mabomba ya maji Hamas walirusha roketi 5000 katika hayo 5000 roketi 2300 zimepenya.
Tusiende mbali,kambi ya kaskazini kwa Israel Galilee au Galilaya ilipigwa na cruise missiles za Hizbollah ikiwa na iron dome kama tatu iliteketea kambi nzima.
Na katika makombora yote Hizbollah alorusha kaskazini hakuna hata moja Iron dome iloweza kudungua.Sasa huu ufanisi wa iron dome uko wapi!??
Basi tusiende mbali,juzi tukio la drone ya Yemeni kuingia Tel Aviv pasi na kuonekana na kushambulia Tel Aviv Iron dome ikiwa active.
Ufanisi wa Iron dome uko wapi!!??
Ukiniambia nichague kati ya Iron dome Na Bavaar-373 nitaichagua Bavaar-373.Maana walau Bavaar ilionesha ufanisi hapo Iran.
Hiyo S-300 mwaka 2021 iliangusha ndege za Israel kama tatu zilipoingia Syria baada ya kuwa activated.
Hakuna ADS mbovu kama iron dome.
Tafuta namna nyingine ya kuipamba mkuu ila imeonesha udhaifu mkubwa sana katika vita hivi vya Gaza.
Still hapa bro unatereza tena.
Iran ina jeshi kubwa hapo Syria.
Na kila siku silaha na askari wanasafirishwa toka Iran kuja Syria kuingia Lebanon.Je hiyo Israel haioni na ikauzia hilo!?
Maana hizo silaha na askari ndio hao wanaoingia katika proxies na kuishambulia Israel.
Syria ni command centre ya Iran na vikundi vyake.
Israel 2000 walitangaza kutoka Lebanon ila hawakuiachia ardhi yote.
Pia kilichochochea vita zaidi ni Israel kumkamata kiongozi mmoja wapo wa Hizbollah 2006 ndipo Hizbollah ilivuka mpaka ikaua askari wa mpaka 8 na kuteka wanne japo wawili walifariki kwa majeraha.
IDF ndio iliamua kuvamia bint jubeir ili kuiweka iwe buffer zone ku demand askari wao.
Na waligoma kumrudisha kiongozi wa Hizbollah.
Yaliyotokea nadhani unayajua,kama isingekuwa USA kuingilia kati basi Israel ingepoteza hadi shebaah Farms.Maana walikua wanarudishwa nyuma kwa bunduki sio kwa kutaka wao.Israel ina sababu ya kuivamia Lebanon ila mbona hujiulizi hawajaivamia mpaka sasa!?
Ilhali mashambulizi ya Hizbollah yameleta maafa Israel kiasi cha kuleta internal displacement.Pia askari 5000 kati ya wale 70000 waliopata ulemavu wa kudumu wamepatikanika kaskazini kwa Israel as a result ya mashambulizi ya Hizbollah.Raia laki 2 wa Israel wameyakimbia makazi.Ila sijaona Israel ikiivamia Hizbollah.
Nadhani itakua unajua sababu.
Israel is millitary crippled ndio maana hata Biden na Macron walimwambia Netanyahu is unhealthy to go full out war with Hizbollah.Sasa mpaka hao watu wazima wanazungumza hivyo jiulize mkuu.
Cha mwisho Syria hajanunua S-300 bali Russia alizileta kulinda askari wake hapo Syria.
Ndio maana Israel inajua kuwa Russia iko Syria na haijawahi kugusa kambi za Russia.
Unazungumzia vita za zamani sana kipindi cha utafutaji uhuru.
Mimi ninazungumza mapigano ya kugombea Kashmir.
Yalitokea mapigano matano India ilishinda pigano moja tu la mwisho la 2010.Kafuatilie mapigano ya kugombea Kashmir.
Jeshi sio tu bajeti kubwa na uchumi peke yake.Bali pia ni mbinu na ari ya vita.Pakistan wana mbinu na ari ya vita kuliko India.
Taleban ilikua inatumia silaha za Marekani.Kumbuka Taleban hiyo hiyo ndio iliyovunja USSR kwa Ufadhili wa USA.
Hivyo USA kui attack Taleban kwa mara kwanza ni rahisi kwasababu jeuri na cheo hapo Afghanistan Taleban alipewa na USA.
Ila ile Taliban iliyotoka madarakani na kuamua kujipanga ilileta vifo vingi vya askari wa USA.
Ndio maana kama ulimsikiliza Trump aliongea wazi kwa Jeshi la USA itabidi liache kulipa gharama kubwa isiyokuwa na faida ya askari wake na pesa zake huko Afghanistan.
Hivyo Afghanistan ijilinde yenyewe.
Kuna vijana wengi pale Afghanistan wa jeshi la Marekani wamekufa na kuwa walemavu.Ungefuatilia namna riaa walivyokua wanakosoa jeshi la USA kuwepo Afghanistan halafu kila siku wanaletewa vijana wao katika majeneza.
😂😂😂😂😂😂😂😂Yani kwa shambulio la Iran kulipiza kisasi Israel mataifa manne yaliisaidia Israel kudungua mashambulizi.
USA,UK,JORDAN NA SAUDI ARABIA.
Still makombora 7 yakapenya na kuharibu airbase ya Israel.
Sasa jiulize kama hayo mataifa manne yasingeshiriki kudungua Israel ingefanya je!??
-Bro tuongee vitu kwa ground,hivyo vitu unavyosema kama Israel anavyo kwanini hajazuia makombora kutoka Lebanon ambayo yameua wanajeshi wake na kusababisha wanajeshi 5000 kuwa walemavu!?
Yani sawa utambe una hela halafu unashindia mlo mmoja wa ugali na Kisamvu.
Mkuu Embu kuwa realistic.
Kama Israel ingekua iko vizuri hivyo ulivyosema basi sasa hivi Galilee ingekuwa salama Salmin na ingekuwa raha mustarehe.
Tunaona yanayojiri tuna macho sio vipofu sisi.
Nimalizie kwa maneno machache huku chini.
Unaongea stori nyingi zisizo na uhalisia.
S-300 Syria haijanunua bali imeletwa na Russia kulinda askari wake pale Syria.
Ndio maana huoni Israel ikishambulia kambi ya Russia.
Hamas wana brigade tatu wana AL QASSAM wanavaa gwanda wana Islamic resistance wanavaa gwanda nyeusi na wana Hamas ambao wao wanavaa randomly.
Madai yako ya kusema kuwa Hamas wanajificha nyuma ya raia,wanajificha hospitali yalishafichuliwa kama ni uongo.
Israel aliunda hadi video fake na zikachunguzwa inajulikana ni staged videos.
Hakuna jipya mnaloweza singizia.
ISRAEL IS A WEAK ARMY.
PKK Na Hamas au Hizbollah ni tofauti.
Japo hao PKK wakifanya shambulio Uturuki huwa inawasaka na inawawajibisha kiukweli.
Operation ya mwisho Uturuki ilituma askari hawazidi 100 na ilirudi na rundo la wapuuzi wa PKK na kuwawajibisha.
PKK ni pana sana maana ni kikundi cha kurudi,pia kipo nchi jirani.
Sio kama Hamas ipo ndani ya OCCUPIED territories ambazo Israel anazi monitor na kuingia anavyotaka.
Mbaya zaidi Gaza ukubwa wake wa Kigamboni ila miezi 9 mmeshindwa hata kuokoa mateka.
Na mmepoteza askari na kupata majeruhi wengi.
Israel haina uwezo wa kuhimili vita muda mrefu.Israel sawa yake ni Hizbollah.
Itetee unavyoitetea ila mimi nikija nakuletea madhaifu ya Israel hapa.
Hizbollah wana gwanda na wana kambi zao kusini mwa Lebanon,mbona wameshindwa kutuma ndege vita zao kuchoma kambi za Hizbollah!!??
😂😂😂😂Baada ya kusikia Iran itatuma ADS pale wakifuata wanaishia na drone strikes tu.