ERDOGAN: Hakuna namna zaidi ya kuingia vita kamili na Israel kwa manufaa ya utu

ERDOGAN: Hakuna namna zaidi ya kuingia vita kamili na Israel kwa manufaa ya utu

Wafanyakazi wa bandari wa italia wamesema ikiwa flotilla inayoenda Gaza kupeleka msaada itazuiliwa na israel au wakakosa nayo mawasiliano walau kwa dk 20 tu,basi watazuwia misafara ya meli ulaya, wakati huohuo Trump amesema israel imepoteza ushawishi kwa congress ya marekani,na 60% ya vijana wa marekani wanaunga mkono Hamas
Siku za uwongo wa taifa teule kuisha zimefika
Ah! Kumbe ni wafanyakazi wamesema. Thubuutuuu! Wakijaribu kuleta fyoko-fyoko, then the next day Mkataba wa utumishi utakuwa umekiukwa na wote hao ni "Fukuza kazi na kuajiri wengine chap". Mbona majobless hata huko wapo?
Shida iko wapi.
 
U Imara wa Jeshi unaujua kwenye uwanja wa vita na wala si vinginevyo!!!!

Nawashangaa sana hasa Wafuga Midevu na Majini kwa kusema kuwa Israel ili pigwa na Iran katika vita vya siku 12 kitu ambacho si kweli ni uongo wa kutaka kujifariji na kujipa moyo kutokana na kipondo walichopewa Iran na Majeshi ya Israel.

Katika vita vya siku 12 Iran iliweza kupoteza Makamanda wake wabobezi 30+ na wanasayansi wa Nuclear 60+ na iliweza kupoteza watu wake zaidi ya 1,000 katika vita hivyo.

Katika vita hiyo Jeshi la anga la Iran halikuweza kuonekana likirusha ndege-vita zake kupambana na Wazee wa anga Israel Air Force (IAF) Jeshi hilo liliufyata mkia mbele ya wababe hao!! Pili Mifumo ya ulinzi wa anga ya Iran haikuweza kufurukuta mbele ya Ndege-vita za Israel hivyo walishindwa hata kudondosha hata ndege-vita moja ya Israel Tatu wanamaji wa Jeshi la Iran huko Bandar Abbas na kwingine walipewa Jambajamba nao hawa kuweza hata kujionyesha tu kuwa wapo. Kwa hali hiyo nashindwa kujua Israel ilipigwaje na Iran

Kwa upande wa Israel ni majengo ya kiraia ndiyo yaliyokuwa yanashambuliwa sana au Kwa wafuga Midevu na Majini ukishambulia maeneo ya raia ndiyo ushindi wenyewe?
Hao makamanda waliuawa kabla Iran hajaanza kushambulia Israel alikuwa anafanya targeted killing ya maafisa wa jeshi la Iran.

Iran alikuwa anaishambulia Israel na aliharibu miundo mbinu mingi tu ya kijeshi ya Israel.

Kwanini Marekani aliingilia Vita baada ya kuona Israel anachapika ?
Kwanini Marekani na Israel ndiyo walioanzisha ceasefire badala ya Iran aliyekuwa anachapika kwa matazamo wako ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom