Hakukataa kuwa covid haipo, na ndio maana kuna juhudi kadhaa zilifanyika kama kupiga nyungu na hata kujaribu kutafuta dawa kutoka Madagascar.
Kikubwa alichokataa ni watu kujifungia ndani eti sababu ya covid alitaka shughuli ziendelee kama kawaida hata ivyo ili work na hata nchi za magharibi zilizotaka watu wajifungie walirudi kwenye mtazamo huo.
Kitaaalam mwili wa binadamu unauwezo wa kupambana na mazingira yake kwakutengeneza kinga wenyewe. Unapokuwa kwenye certain harmed environmental or disease mwili unatengeneza resistance to that certain antigen. Na ndio maana kuna watu hawakuchanja na wapo mpaka leo na wanadunda vizuri.
Mkuu, Wanadamu wakikuchukia wanaweza kukupaka kila aina ya matope!! Hata hivyo bado Mungu anasimama kutetea watu wake wawe hai au wamekufa.
Kwa Wakristo haturuhusiwi kumjadili Marehemu maana hatujui wakati ana aga dunia alisemezana nini na Mungu wake! Na inawezekana hata kama alikuwa na dhambi kiasi gani, kama alitubu Mungu amemsamehe! Ndio maana tunasema “Mwanga wa milele umpe eee Bwana, apumzike kwa amani” Au RIP au Mwendo ameumaliza nk Kinachobaki ni Siku ya hukumu!
Yote kwa yote Mungu yupo na atahukumu kwa haki yake!! Hata Kaini alipomuuwa ndg yake Mungu alimwambia damu ya ndg yako ipo ardhini inakulilia!! Na kutokana na aliyekufa kushindwa kujitetea damu iliyomwagika ilia na ililipa kisasi kwa uwezo wa Mungu.
Tuje kwenye hili la COVID 19. Ngoja niungane nawe kama ifuatavyo:-
1. JPM hakukataa kama COVID 19 ipo! Na uthibitisho ni Viwanda vyetu kutengeneza mpaka yale manguo wataalamu walikuwa wanavaa.
2. JPM ktk kupambana na COVID 19 alitumia nguvu kubwa kuwashawishi watu wamrudie Mungu na alisimama na 2 Nyakati 7:14
3. JPM aliwaomba watoa mikopo waipatie nchi fedha na sio vifaa kama barakoa nk. Mikopo hiyo ililetwa akiwa amefariki na imefanya kazi kubwa sana zikiwemo Ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Afya, Ununuzi wa Ambulance, Ujenzi wa madarasa, vifaa mbalimbali vya matibabu nk
4. JPM alikemea kitendo cha wagonjwa kukimbiwa na kuna vifo vilitokana na wataalamu kuwaogopa wagonjwa!! Alisema “sio kila ugonjwa wa kupumua ni COVID 19”! Pia mtu yoyote akiwa na hofu lazima pumzi ipate shida na kila anayetaka kukata roho lazima pumzi ianze kukata nk kwanini tukimbie wagonjwa?
5. Kwanini Rais wa sasa wa Marekani Ndg Trump iliita COVID 19 ni scam? Je! Kuna nini alikijua na alikisimamia mpaka mtandao wa Tweeter wakamfungia.
6. Kwanini Marekani nk imewapeleka Mahakamani vinara wote wa COVID 19?
7. Kwanini Rais Trump amemteua mpingaji namba moja wa COVID 19 kuwa Waziri wake wa Afya? JFKennedy Jr. unadhani nini kinafata hapo?
8. Baada ya JPM kufa COVID 19 ilipotea ghafla na hatukuona tena vifo hasa vya viongozi!
9. Msiba wa JPM Ulijaza watu kila kona kuanzia Dar, Zanzibar, Dodoma, Mwanza hadi Chato!! Kwa msongamano ule tulitegemea covid 19 ingewamaliza Watanzania na sasa ndio wangeanguka kama mbwa barabarani! Kumbuka Prof. Janabi alitoa tathmini ya vifo kila siku, kila wiki na mwezi watu watakufa wasiopungua 500! Mbona ghafla ilikata?
10. Watanzania wangepewa lockdown ni wangapi wangekufa kwa njaa nk?
11. Kungekuwa na lockdown UCHUMI leo ungekuwaje?
11. Watanzania wangelazimishwa kuvaa barakoa ya N95 ambapo zinatakiwa karibu 3 kwa Siku na moja ilikuwa Shs. 5,000/-. Ni wangapi na familia zao wangefanikiwa kununua kila siku?
12. Wote ni mashuhuda vifo kwenye nchi za wenzetu waliofata miongozo yote, yamkini kwa namna moja au nyingine vilikuwa vifo vingi kuliko TZ.
Hebu tusimkufuru Mungu tumrudishie sifa na utukufu kwani alitutetea Watanzania sawa na tulivyomwamini.
By the way hakuna anayejua nini kitakuwa sababu ya kifo chake atakapodondoka!
13. Hivi ni kwanini COVID 19 ilikuwa inawaondoa zaidi wanaume? Mke anauguza havai barakoa nk na hapati ugonjwa na anazika mume na yeye ni mzima wa Afya mpaka leo!
14. Wote tumeshuhudia kuna wimbi fulani limepita la mafua, wengine wameliita bby covid! Mbona tumesepa nalo kimya kimya na wengine limewaondoa?
14. Maswali ni mengi unaweza kuongezea..!
Kikubwa najua mkuu unafatilia yaliyopo huko duniani! Tayari kuna gonjwa jipya linakuja! Ni wakati SAHIHI kuangalia maambukizi yanayozungumzwa yakifika TZ tutapambana vipi? Tumejipangaje? JPM kama alikosea basi Mungu amrehemu na tumuombee apumzike kwa amani! Tujipange sisi tulio hai ktk mambo yaliyo mbele yetu!
Mwisho kama kulikuwa na MICHEZO mchafu kwenye janga la COVID 19 na watu waliondolewa Uhai, basi tuwe na uhakika damu zinalia ardhini na hukumu ya Mungu ipo njiani!!
Kuhusu kauli ya mama SAMIA, wale wanaompa hizo taarifa ndio wakuangaliwa kwa jicho la tatu!! Yeye hana makosa! Maana ndiye aliwatangazia Watanzania kifo cha JPM! Iweje tena abadilike? Tuendelee kunywa mtori nyama tutazikuta chini!
Bye for now!
Queen Esther