Mpangaji Erick Adam aliyekuwa akishi kijiji cha Ilkirev, wilayani Arumeru mkoani Arusha, ameuawa akidaiwa kuchomwa kisu na mpangaji mwenzake aliyetajwa kwa jina la Blandina Fred, baada ya mzozo kuhusu kuchangia Sh1, 000 ya ankara ya umeme (Luku).
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo alisema tukio hilo lilitokea juzi mchana, ambapo Blandina alikuwa ameshika kisu mkononi akijiandaa kupika.
"Kilichotokea ni kuwa wote ni wapangaji, walikuwa wakigombana, huyu binti alikuwa na kisu kwa kuwa alikuwa jikoni, baada ya kutokea majibizano kati alimchoma mwenzake., 'alidai Kamanda Masejo.
Alisema Adam alifariki kutokana na kutokwa na damu nyingi baada ya kuchomwa kisu na wanamshikilia mtuhu- miwa kwa mahojiano.
"Taratibu zikikamilika atafikishwa mahakamani kutokana na tuhuma zinazomkabili na mwili wa Adam umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi," alisema.
Mkazi wa Kijiji cha Ilkirevr Joram Laizer alisema wapangaji wa nyumba hiyo huwa wanachangia ankara za
umeme kila mwezi. "Hatukujua kilichokuwa kinaendelea, tulisikia kelele na baada ya kufika Erick alikuwa chini
akivuja damu, tulimuwahisha hospitali, lakini alifariki baadaye," alisema.