Wiwachu,
Mimi naamini alifanya hayo MAKOSA kwa sababu ameshalipa advansi ya milioni mia moja na ameahidi kumalizia milion 170 ndani ya miezi 6(siku 180 alipe milioni 170).
Kwangu Mimi ni sawa na kusema mwizi amekiri kuiba na ameonyesha alichoiba, sasa utasemaje amelazimishwa kukiri?
Nashindwa kuamini eti mwandishi wa Kawaida anaweza kuwa na 100mls kulipa kwa mkupuo mmoja
Huenda pia zile tetesi kwamba kwenye akaunti kulikutwa mamia ya mamilioni sambamba na ujenzi wa ghorofa aliokuwa anaendesha.
Tukio hili linanikumbusha kisa cha yule mama wa Uingereza aliyeishi na mumewe miaka 50 bila kujua kama ni jasusi mpaka mume alipofariki ndio akagundua kupitia nyaraka alizoacha.
Funzo kubwa hapa ni kwamba wabongo tupunguze kujifanya tunajua kila kitu mpaka yale anayofanya mtu sirini.
Kuna watu wamekomaa mitandaoni kumtetea KABENDERA wakati hawajui wala hawajawahi kukutana naye. Kibaya zaidi wanapinga hata alichokiri mwenyewe na kuanza kumlisha maneno eti amelazimishwa.
Ukitaka tukuamini kuwa amelazimika basi lete ushahidi kuwa kalazimishwa na uonye hizo 100'000'000/= kazipata wapi na ulete ushahidi kuonyesha alikozipata
Vinginevyo tukubaliane na taarifa rasmi zilizotolewa mahakamani, serikalini na Kabendera mwenyewe