Erick Kabendera: Mwendazake aliendesha genge la wahuni na alikusudia kumkamata Rais Mstaafu Kikwete

Ilikuwa safi sana kwa Jpm Kuwakomesha wahuni wote walioifikisha hii nchi hapa ilipo
Mimi ni mmoja ya watu wanaoamini ni kweli utawala wa Kikwete ulikuwa mbovu na Magufuli alipoingia alikutana na mengi. Tatizo liko kwenye njia ambazo alikuwa anachukuwa kujaribu kufanya marekebisho. Njia za kihuni, za kisiri na zisizofuata sheria. Na mbaya zaidi akadhani kila anayemkosoa ni adui na anafaa kuawa.
 
Ni wengi hawajui undani wa kutekwa kwa MO, na mashambulizi aliyokuwa anarusha yule mhuni mwanaharakati huru. Hata haya maandishi ya Kabendera ni sehemu ya ''undani'' wenyewe. Na kama ukijua undani, na kama wewe kweli ni mzalendo, mtanzania mwenye kutaka haki sana sana utaishia kusema: ''kumbe haya mafisi yalifikia hatua ya kuparurana kiasi hik! Basi tunahitaji katiba mpya haraka sana''
 
Duu yaani yule jamaa aliona baada ya kumtoa Mkapa ilibidi ammalize na JK Ili abakie huru,aisee Dunia ina Siri hii..

Anyway Mungu ni fundi amejua kumkomesha aliyepanga mambo ya Hila za kudhuru gizani.
 
Sasa hayupo na hawezi chunguzwa, Saa 100 mwenyewe lazima alishiriki mambo yanayosemwa mfano ununuzi wa ndege nk

Haina maana kwa sasa,na viongozi wa sasa ni kama mwendazake tu ndio maana waliimba ccm ni ile ile
Pengine alijua ila sio kushiriki..Lisu mwenyewe anakiri kwamba hajawahi pata kashfa yeyote kumhusu Rais Samia.
 
Magufuli nikiongozi bora kuwahi kutokea kwenye Taifa hili.yaani hata mumchafue vipi amewakuna kunako takiwa kwani kumkamata kiongozi wa mafisadi nizambi

Nani aliyemchafua? Kuibuka kwa magenge ya wahuni(sabaya,DAB,Mwanaharakati huru etc) ,watekaji na kupora mali za wafanyabiashara ndio sisi tuliofanya? Fedha za maduka ya kubadilishia fedha walizopora ziko wapi? Nani aliyempiga tundu lissu risasi? Nani aliyempoteza Bensaa8?

Waliomteka Roma/MO? Ni watu wasiojulikana.
Waliompiga risasi Lissu? Ni watu wasiojulikana
 
NI kweli marehemu alikuwa na michezo ya kihuni.
Ila kwa Sasa haya unayofanya bwana kabendera hayana maana.
Yupo zake chato anajigeuza geuza.
Na kule alipo Hana smartphone
Wapo waliotekeleza huu ufala ndio anawalenga Kabendera.. Mwenda zake alikua anatoa maagiizo tuu.
 
Aibu hii sio Magufuli ni ya state nimetoa onyo. Mkitaka msifieni lakini kunajisi state hapana
Wapo viongozi wengi wa nchi waliofanya uhalifu wakiwa madarakani. Mambo hayo yakiwekwa wazi siyo aibu bali ndiyo uthibitisho wa uimara wa state yenyewe.
Hata hivyo, sina maana ya kwamba hili linalojadiliwa lina ushahidi wa kutosha kuthibitisha.
 
Mwendazake alipata urais kwa bahati tu , sio kwa kupangiliwa na kundi la ndani. Sasa hivi nafasi hutokea naturally, na ikitokea akaja mwingine asiye na genge kama hilo utawajibika tena.
Ndio maana uovu wa viongozi waliopita tangu wakiouza mashirika ya Umma kwa bei za kutupa na wale wa Richmond na EPA waliachwa ili kutoendeleza mlolongo wa kulipizana.
Bahati mbaya zaidi Mwendazake hayupo , wala huwezi kumlipiza na ikiwezekana basi Katiba ijayo iangalie makosa yaliyofanywa na viongozi kwa kutumua ofisi zao vibaya washtakiwe na kufilisiwa.
Hapa walio hai na familia zao wawajibike.
 
Hata huyo mkwere naye alivuruga na anajua hilo. Haya mambo ukiyaelewa kwa undani sana sana utasema: ''du mafisi kumbe yalifika hatua ya kusalitiana kiasi hiki?''
Politics πŸ™Œ, ishu ni kwamba Mwendazake bado hakuwa na mbinu za kijasusi za kumuondoa Mkwere, jamaa alikuwa na pupa + mihemuko na huu mchezo hautaki haraka wala hasira, mpaka hii ishu imevuja kwa kina Kabendera ni wazi jamaa hakuwa na watu wa uhakika mpaka siri zikavuja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…