Erick Kabendera: Rais Samia “Thucydides Trap” haitakuacha salama

Erick Kabendera: Rais Samia “Thucydides Trap” haitakuacha salama

Tulichokiona wiki iliyopita wakati wa ziara za Makonda kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa ni kutumia mbinu zile zile alizozitumia kwa Magufuli kumhadaa Rais Samia; anaonekana kama vile anampigia kampeni Rais Samia wakati huohuo anasafisha jina lake na kuandaa mtaji wake wa kisiasa wa huko mbeleni....

Nmeamin jamaa ni mwanadishi mpuuzi kuwahi kutokea.

Haya Makonda anaandaa mtaji wake kisiasa Kwan ni dhambi???.

Kwan Makonda anataka kushindana na Samia??.

Sikuna watu wanashindana na Samia, wapi wanojiandaa Urais 2030?? Kwan Makonda sio haki yake kujiandaa Urais hiyo 2030??.

PUMBAVU KABISA, JANDISHI KANJANJA.
 
Wengine majina makubwa ya bure, kazi ni kudanganya watu tu.

Unaleta "theory" ya himaya kamili kwa mtu mmoja?

Kwa andiko hili nimeamini Makonda anatisha.
 
Nani asiye kufahamu Kabendera kwa namna unavyotumika na wanasiasa wasio mpenda yeyote awaye ahatarishaye chakula cha mafisadi?!

Hata sasa, ni wazi wale waliokutumia kipindi cha Magufuli ndiwo hao hao wameanza kukutumia kipindi hiki Makonda anapoanza kuhatarisha chakula cha vipenzi wako mafisadi.

Wape salamu wapendwa wako;-

Zitto
January
Nape
Kinana.

..Makonda sasa amejiunga na anafanya kazi na genge la kina Kinana, January, na Nape.
 
Huyu arudi kwao huko ambako vita ni km chakula,
Cucydide trap ndo nini?
 
Huyu kabendera si ndo miongoni mwa waliotunga kitabu cha kumnanga Magu 'the state' nafikri kiliishia kwa wauza vitumbua kwa ajili ya kufungia wateja.
Nilivinunua nikavikojolea na kuvichoma moto.

Ilibakia kidogoo tu niviharishie ila sikuwa na tumbo la kuhara.
 
Kama kuna ukweli juu ya tetesi zimuhusuzo Makamu wa Mwenyekiti Taifa wa chama, basi teuzi ya mwenezi mpya inaweza kuwa ni mojawapo ya mambo yanayopelekea hali ya mtafaruku unaofukuta chini kwa chini. Utendaji wa muenezi mpya wa kutoa maagizo ya moja kwa moja na kuyaelekeza kwa mawaziri, ambao mamlaka yao ya uteuzi ni Rais mwenyewe, ni kitu ambacho hakitarajiwi kutoka kwa mtu wa nafasi ya katibu muenezi wa chama.

Hii ni aina ya nguvu mpya ya mamlaka inayojijenga ndani ya chama dola, pengine isingalionekana ni jambo geni endapo maagizo kama hayo yangalitoka katika kinywa cha PM ama kidogo hata kwa KM wa chama. "It is plain reality that an hegemony is threatened by this new emerging power, there will be likelihood of war between the two powers in the near future".

Kupanga ni kuchagua. "SSH must be real smart in this time, otherwise things will fall apart".

Acheni kumtisha Madam President na vocabularies zenu za kuungaunga!

Kwamba ninyi humu ndani ndio mnajua sana na mnaona yajayo kuliko Rais?

Kwamba ninyi mnayajua maelekezo ya Rais kwenda kwa muenezi kuliko Rais mwenyewe?

Endeleeni kumchukulia poa Madam President, yajayo yanafurahisha zaidi.
 
Kwenye historia ya vita na mahusiano ya kimataifa, kuna nadharia inaitwa “Thucydides Trap” ambayo utumika kuelezea ulazima wa kutokea mgogoro au vita endapo taifa linalochipukia linapotishia kulizidi nguvu na ushawishi taifa lenye nguvu.

Kama wewe ni msomaji wa siasa za Nicollo Machiavelli, utakumbuka kuwa msingi wa nadharia zake ni kuwa kiongozi akihodhi madaraka na mamlaka, hawezi kutengeneza muhimili mwingine wa kisiasa wenye nguvu na ushawishi kama wake. Ndiyo maana marais ushauriwa wasiwateue wagombea wenza au mawaziri wakuu wenye nguvu au ushawishi wa kisiasa kuliko wao.

Bado hatujui sababu za Rais Samia kumteua Makonda lakini tunajua kuwa Makonda alimhadaa Magufuli kiasi kwamba “aliogopa” kumuondoa kwenye nafasi ya mkuu wa mkoa licha ya kukabiliwa na tuhuma nzito. Tulichokiona wiki iliyopita wakati wa ziara za Makonda kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa ni kutumia mbinu zile zile alizozitumia kwa Magufuli kumhadaa Rais Samia; anaonekana kama vile anampigia kampeni Rais Samia wakati huohuo anasafisha jina lake na kuandaa mtaji wake wa kisiasa wa huko mbeleni.

Mwanasiasa yoyote mkongwe hawezi kuamini maneno ya Makonda kutokana na historia yake na ukweli kwamba anachokiwaza kichwani mwake ni tofauti na matendo yake.

Kufanikiwa kwake kisiasa kumetokana na kuwahadaa watu, kuwadhalilisha wana CCM, wapinzani na viongozi washaafu. Hawezi kushidwa kumfanyia vitendo kama hivyo Raisa Samia hata kama amekula kiapo cha utii kwake. Kwahiyo ni wazi kuwa Makonda anazitumia ziara hizi kujenga taswira kuwa serikali ipo chini yake kwa kutoa maelekezo kwa mawaziri na viongozi waandamizi wa serikali.

Kumruhusu aendelee kufanya hivyo ni kurudia makosa aliyoyafanya Rais Mkapa kwa kumjenga Magufuli kisiasa. Natumaini Rais Samia amewaza kwa undani na kupokea ushauri wa watu wake wa karibu kabla ya kufikia uamuzi huu.

Kama hakufanya hivyo, atajikuta anamuandaa mshindani wake kwenye uchaguzi ujao au anamtengeneza mwanasiasa atayeiingiza nchi kwenye matatizo baada ya kuondoka kwake madarakani. Hapo ndipo dhana ya “Thucydides Trap” itakapodhibitika.

c&p
Thucydides's Trap refers to the natural, inevitable discombobulation that occurs when a rising power threatens to displace a ruling power...[and] when a rising power threatens to displace a ruling power, the resulting structural stress makes a violent clash the rule, not the exception

Tunao memo huu: Mgema akisifiwa, tembo hulitia maji
Huyu jamaa ni uwezo wa kufikiri ni mdogo. Makonda chapa kazi!
 
Baada ya Makonda kupewa nafasi kwenye chama chake, kelele za huruma juu ya CCM na viongozi wake imekuwa kubwa kana kwamba hawajui kwanini Makonda yuko pale.

Amewatoa relini wengi, focus imekuwa kwake kwenye kila tukio lake, na hapo ndio CCM anafanikiwa kwa ulaghai wake kwa wajinga.

CCM ni box la Pandora.
 
Kabisa, kafanikiwa kirahisi sana, wapinzani ndio wamekuwa spika yake ya kila anachofanya.

Siku watakayojua kuwa adui yao mkubwa ni CCM na si wateuliwa ambao leo wapo kesho hawapo watafanikiwa.

Na bado CCM sio adui yao.

Unamtazama vipi mtanzania alieridhika na kuiamini CCM kwa kila kitu?
 
Kwenye historia ya vita na mahusiano ya kimataifa, kuna nadharia inaitwa “Thucydides Trap” ambayo utumika kuelezea ulazima wa kutokea mgogoro au vita endapo taifa linalochipukia linapotishia kulizidi nguvu na ushawishi taifa lenye nguvu.

Kama wewe ni msomaji wa siasa za Nicollo Machiavelli, utakumbuka kuwa msingi wa nadharia zake ni kuwa kiongozi akihodhi madaraka na mamlaka, hawezi kutengeneza muhimili mwingine wa kisiasa wenye nguvu na ushawishi kama wake. Ndiyo maana marais ushauriwa wasiwateue wagombea wenza au mawaziri wakuu wenye nguvu au ushawishi wa kisiasa kuliko wao.

Bado hatujui sababu za Rais Samia kumteua Makonda lakini tunajua kuwa Makonda alimhadaa Magufuli kiasi kwamba “aliogopa” kumuondoa kwenye nafasi ya mkuu wa mkoa licha ya kukabiliwa na tuhuma nzito. Tulichokiona wiki iliyopita wakati wa ziara za Makonda kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa ni kutumia mbinu zile zile alizozitumia kwa Magufuli kumhadaa Rais Samia; anaonekana kama vile anampigia kampeni Rais Samia wakati huohuo anasafisha jina lake na kuandaa mtaji wake wa kisiasa wa huko mbeleni.

Mwanasiasa yoyote mkongwe hawezi kuamini maneno ya Makonda kutokana na historia yake na ukweli kwamba anachokiwaza kichwani mwake ni tofauti na matendo yake.

Kufanikiwa kwake kisiasa kumetokana na kuwahadaa watu, kuwadhalilisha wana CCM, wapinzani na viongozi washaafu. Hawezi kushidwa kumfanyia vitendo kama hivyo Raisa Samia hata kama amekula kiapo cha utii kwake. Kwahiyo ni wazi kuwa Makonda anazitumia ziara hizi kujenga taswira kuwa serikali ipo chini yake kwa kutoa maelekezo kwa mawaziri na viongozi waandamizi wa serikali.

Kumruhusu aendelee kufanya hivyo ni kurudia makosa aliyoyafanya Rais Mkapa kwa kumjenga Magufuli kisiasa. Natumaini Rais Samia amewaza kwa undani na kupokea ushauri wa watu wake wa karibu kabla ya kufikia uamuzi huu.

Kama hakufanya hivyo, atajikuta anamuandaa mshindani wake kwenye uchaguzi ujao au anamtengeneza mwanasiasa atayeiingiza nchi kwenye matatizo baada ya kuondoka kwake madarakani. Hapo ndipo dhana ya “Thucydides Trap” itakapodhibitika.

c&p
Thucydides's Trap refers to the natural, inevitable discombobulation that occurs when a rising power threatens to displace a ruling power...[and] when a rising power threatens to displace a ruling power, the resulting structural stress makes a violent clash the rule, not the exception

Tunao memo huu: Mgema akisifiwa, tembo hulitia maji
Pamoja na maelezo marefu ya kurembaremba na kizungu ndani yake, Bado hujaeleweka mkuu! 😳
 
Je, kuna ukiukwaji wa katiba kwa Makonda kutoa maagizo kwa mawaziri na watendaji wengine wa serikali? Nijuavyo kazi ya chama ni kuisimamia serikali na hicho ndicho akifanyacho katibu mwenezi wa CCM. Tukumbuke kipindi Cha kikwete Kinana alitembea maeneo mbalimbali ya Tanzania na kuja na hoja ya mawaziri Mizigo.

Kwa mzee Kinana umeenda mbali.

Kazi aliyoifanya Nape 2010-2014 jimbo kwa jimbo hawataki kuikumbuka.
 
Huyu kabendera si ndo miongoni mwa waliotunga kitabu cha kumnanga Magu 'the state' nafikri kiliishia kwa wauza vitumbua kwa ajili ya kufungia wateja.
Kaja na kingine!
 
Huyu kabendera si ndo miongoni mwa waliotunga kitabu cha kumnanga Magu 'the state' nafikri kiliishia kwa wauza vitumbua kwa ajili ya kufungia wateja.
Kimenunulia sana na nakala kuisha. Nimekiagiza UK ndiyo nikakipata! Haikusaidii usema ujinga ukashangiliwa na wajinga wenzio.
 
Back
Top Bottom