Carlos The Jackal
JF-Expert Member
- Feb 6, 2017
- 25,725
- 78,589
Nani asiye kufahamu Kabendera kwa namna unavyotumika na wanasiasa wasio mpenda yeyote awaye ahatarishaye chakula cha mafisadi?!
Hata sasa, ni wazi wale waliokutumia kipindi cha Magufuli ndiwo hao hao wameanza kukutumia kipindi hiki Makonda anapoanza kuhatarisha chakula cha vipenzi wako mafisadi.
Wape salamu wapendwa wako;-
Zitto
January
Nape
Kinana.
Nilivinunua nikavikojolea na kuvichoma moto.Huyu kabendera si ndo miongoni mwa waliotunga kitabu cha kumnanga Magu 'the state' nafikri kiliishia kwa wauza vitumbua kwa ajili ya kufungia wateja.
Kama kuna ukweli juu ya tetesi zimuhusuzo Makamu wa Mwenyekiti Taifa wa chama, basi teuzi ya mwenezi mpya inaweza kuwa ni mojawapo ya mambo yanayopelekea hali ya mtafaruku unaofukuta chini kwa chini. Utendaji wa muenezi mpya wa kutoa maagizo ya moja kwa moja na kuyaelekeza kwa mawaziri, ambao mamlaka yao ya uteuzi ni Rais mwenyewe, ni kitu ambacho hakitarajiwi kutoka kwa mtu wa nafasi ya katibu muenezi wa chama.
Hii ni aina ya nguvu mpya ya mamlaka inayojijenga ndani ya chama dola, pengine isingalionekana ni jambo geni endapo maagizo kama hayo yangalitoka katika kinywa cha PM ama kidogo hata kwa KM wa chama. "It is plain reality that an hegemony is threatened by this new emerging power, there will be likelihood of war between the two powers in the near future".
Kupanga ni kuchagua. "SSH must be real smart in this time, otherwise things will fall apart".
Huyu jamaa ni uwezo wa kufikiri ni mdogo. Makonda chapa kazi!Kwenye historia ya vita na mahusiano ya kimataifa, kuna nadharia inaitwa “Thucydides Trap” ambayo utumika kuelezea ulazima wa kutokea mgogoro au vita endapo taifa linalochipukia linapotishia kulizidi nguvu na ushawishi taifa lenye nguvu.
Kama wewe ni msomaji wa siasa za Nicollo Machiavelli, utakumbuka kuwa msingi wa nadharia zake ni kuwa kiongozi akihodhi madaraka na mamlaka, hawezi kutengeneza muhimili mwingine wa kisiasa wenye nguvu na ushawishi kama wake. Ndiyo maana marais ushauriwa wasiwateue wagombea wenza au mawaziri wakuu wenye nguvu au ushawishi wa kisiasa kuliko wao.
Bado hatujui sababu za Rais Samia kumteua Makonda lakini tunajua kuwa Makonda alimhadaa Magufuli kiasi kwamba “aliogopa” kumuondoa kwenye nafasi ya mkuu wa mkoa licha ya kukabiliwa na tuhuma nzito. Tulichokiona wiki iliyopita wakati wa ziara za Makonda kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa ni kutumia mbinu zile zile alizozitumia kwa Magufuli kumhadaa Rais Samia; anaonekana kama vile anampigia kampeni Rais Samia wakati huohuo anasafisha jina lake na kuandaa mtaji wake wa kisiasa wa huko mbeleni.
Mwanasiasa yoyote mkongwe hawezi kuamini maneno ya Makonda kutokana na historia yake na ukweli kwamba anachokiwaza kichwani mwake ni tofauti na matendo yake.
Kufanikiwa kwake kisiasa kumetokana na kuwahadaa watu, kuwadhalilisha wana CCM, wapinzani na viongozi washaafu. Hawezi kushidwa kumfanyia vitendo kama hivyo Raisa Samia hata kama amekula kiapo cha utii kwake. Kwahiyo ni wazi kuwa Makonda anazitumia ziara hizi kujenga taswira kuwa serikali ipo chini yake kwa kutoa maelekezo kwa mawaziri na viongozi waandamizi wa serikali.
Kumruhusu aendelee kufanya hivyo ni kurudia makosa aliyoyafanya Rais Mkapa kwa kumjenga Magufuli kisiasa. Natumaini Rais Samia amewaza kwa undani na kupokea ushauri wa watu wake wa karibu kabla ya kufikia uamuzi huu.
Kama hakufanya hivyo, atajikuta anamuandaa mshindani wake kwenye uchaguzi ujao au anamtengeneza mwanasiasa atayeiingiza nchi kwenye matatizo baada ya kuondoka kwake madarakani. Hapo ndipo dhana ya “Thucydides Trap” itakapodhibitika.
c&p
Thucydides's Trap refers to the natural, inevitable discombobulation that occurs when a rising power threatens to displace a ruling power...[and] when a rising power threatens to displace a ruling power, the resulting structural stress makes a violent clash the rule, not the exception
Tunao memo huu: Mgema akisifiwa, tembo hulitia maji
Baada ya Makonda kupewa nafasi kwenye chama chake, kelele za huruma juu ya CCM na viongozi wake imekuwa kubwa kana kwamba hawajui kwanini Makonda yuko pale.
Amewatoa relini wengi, focus imekuwa kwake kwenye kila tukio lake, na hapo ndio CCM anafanikiwa kwa ulaghai wake kwa wajinga.
Kabisa, kafanikiwa kirahisi sana, wapinzani ndio wamekuwa spika yake ya kila anachofanya.
Siku watakayojua kuwa adui yao mkubwa ni CCM na si wateuliwa ambao leo wapo kesho hawapo watafanikiwa.
Pamoja na maelezo marefu ya kurembaremba na kizungu ndani yake, Bado hujaeleweka mkuu! 😳Kwenye historia ya vita na mahusiano ya kimataifa, kuna nadharia inaitwa “Thucydides Trap” ambayo utumika kuelezea ulazima wa kutokea mgogoro au vita endapo taifa linalochipukia linapotishia kulizidi nguvu na ushawishi taifa lenye nguvu.
Kama wewe ni msomaji wa siasa za Nicollo Machiavelli, utakumbuka kuwa msingi wa nadharia zake ni kuwa kiongozi akihodhi madaraka na mamlaka, hawezi kutengeneza muhimili mwingine wa kisiasa wenye nguvu na ushawishi kama wake. Ndiyo maana marais ushauriwa wasiwateue wagombea wenza au mawaziri wakuu wenye nguvu au ushawishi wa kisiasa kuliko wao.
Bado hatujui sababu za Rais Samia kumteua Makonda lakini tunajua kuwa Makonda alimhadaa Magufuli kiasi kwamba “aliogopa” kumuondoa kwenye nafasi ya mkuu wa mkoa licha ya kukabiliwa na tuhuma nzito. Tulichokiona wiki iliyopita wakati wa ziara za Makonda kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa ni kutumia mbinu zile zile alizozitumia kwa Magufuli kumhadaa Rais Samia; anaonekana kama vile anampigia kampeni Rais Samia wakati huohuo anasafisha jina lake na kuandaa mtaji wake wa kisiasa wa huko mbeleni.
Mwanasiasa yoyote mkongwe hawezi kuamini maneno ya Makonda kutokana na historia yake na ukweli kwamba anachokiwaza kichwani mwake ni tofauti na matendo yake.
Kufanikiwa kwake kisiasa kumetokana na kuwahadaa watu, kuwadhalilisha wana CCM, wapinzani na viongozi washaafu. Hawezi kushidwa kumfanyia vitendo kama hivyo Raisa Samia hata kama amekula kiapo cha utii kwake. Kwahiyo ni wazi kuwa Makonda anazitumia ziara hizi kujenga taswira kuwa serikali ipo chini yake kwa kutoa maelekezo kwa mawaziri na viongozi waandamizi wa serikali.
Kumruhusu aendelee kufanya hivyo ni kurudia makosa aliyoyafanya Rais Mkapa kwa kumjenga Magufuli kisiasa. Natumaini Rais Samia amewaza kwa undani na kupokea ushauri wa watu wake wa karibu kabla ya kufikia uamuzi huu.
Kama hakufanya hivyo, atajikuta anamuandaa mshindani wake kwenye uchaguzi ujao au anamtengeneza mwanasiasa atayeiingiza nchi kwenye matatizo baada ya kuondoka kwake madarakani. Hapo ndipo dhana ya “Thucydides Trap” itakapodhibitika.
c&p
Thucydides's Trap refers to the natural, inevitable discombobulation that occurs when a rising power threatens to displace a ruling power...[and] when a rising power threatens to displace a ruling power, the resulting structural stress makes a violent clash the rule, not the exception
Tunao memo huu: Mgema akisifiwa, tembo hulitia maji
Je, kuna ukiukwaji wa katiba kwa Makonda kutoa maagizo kwa mawaziri na watendaji wengine wa serikali? Nijuavyo kazi ya chama ni kuisimamia serikali na hicho ndicho akifanyacho katibu mwenezi wa CCM. Tukumbuke kipindi Cha kikwete Kinana alitembea maeneo mbalimbali ya Tanzania na kuja na hoja ya mawaziri Mizigo.
Duh!Birds of the same feathers fly together! akili za makonda akiwa nazo mtoto wangu namuua mapema
Kaja na kingine!Huyu kabendera si ndo miongoni mwa waliotunga kitabu cha kumnanga Magu 'the state' nafikri kiliishia kwa wauza vitumbua kwa ajili ya kufungia wateja.
Kimenunulia sana na nakala kuisha. Nimekiagiza UK ndiyo nikakipata! Haikusaidii usema ujinga ukashangiliwa na wajinga wenzio.Huyu kabendera si ndo miongoni mwa waliotunga kitabu cha kumnanga Magu 'the state' nafikri kiliishia kwa wauza vitumbua kwa ajili ya kufungia wateja.