Ester Bulaya: Ni bora sisi tuwatumikie mabeberu kuliko kukutumikia wewe!

Ester Bulaya: Ni bora sisi tuwatumikie mabeberu kuliko kukutumikia wewe!

Nazungumzia waliotupa uhuru hawaku wakatili kama hawa wa kwetu! Huko nyuma sijakuongelea. All in all, Slavery was a mode of killing as shooting with a gun, abduction, imprisonment are in today's regimes of the world, africa in particular
Walio tupa uhuru hawakuwa wakatili kama hawa wa kwetu??!!! Unamaanisha waingereza walikuwa watu wazuli sana kwetu sisi sivyo??

Kama walikuwa wema kwanini walikuja kututawala,au wewe ni mmoja wa wale wanao amini kuwa wazungu walikuja kutuletea ustarabu??

Hivi utawatofautisha vipi wazungu hasa hawa waingereza na slavery, na all form of Colonial violence??

Seriously kabisa mkuu unasema Wa Britain hawakuwa wakatili??!!!

Niambie kama ni utani mkuu ila haiwezi kuwa serious hii.
 
Huna elimu ya madhara ya Ukoloni ambayo tunayo mpaka sasa, mojawapo ni watu kufikiri wazungu ni zaidi yetu na wakombozi wetu wakati ni wezi na majambazi wetu. Acha kujitia aibu na kuiaibisha TZ nzima, nenda kaelimike kabla ya kuongea.
 
Kwanza ni uongo hakuna neno linalo koma kutumika pili dunia ya Sasa adui yako kuwa na mawasiliano nae ndio Jambo muhimu zaidi mfano Cuba/USA ,USA/rusia, Egypt/Israel, Qatar/Israel dunia ya Sasa kuwa na mahusiano na adui yako Ni muhimu zaidi lakini sio kushirikiana nae bulaya kajipambanua kuwa ni kweli tunashirikiana nao kahitimisha zile tetesi

Hujamalizia utamu katika jibu lako, kamilisha kwa kujibu nukuu hii katika quote ". Au nitajie nchi 5 tu kwa mtazamo wako wewe ungewaita ni mabeberu" .

Jibu vitu kamili usirukeruke- Nilichokupata ni kwamba ukienda wewe kuomba kwake yeye si beberu, mpinzani akienda kwa huyo huyo ni beberu.

Nilisema neno beberu halina mantiki kama neno Zeru zeru lilivyokataliwa sasa hivi na serikali. Kwa maana hiyo Mwinyi alilikataa neno Beberu na unyonyaji.

Jibu twende pamoja.
 
Bulaya anajisahau sana, hata ukiwa mpinzani kuna makombora ya kurusha
Huko ni kujivua nguo hadharani
Sioni anachojisahau wala kujivua nguo inategemea tu na uwezo wa mtu kuchambua alichooandika
 
Walio tupa uhuru hawakuwa wakatili kama hawa wa kwetu??!!! Unamaanisha waingereza walikuwa watu wazuli sana kwetu sisi sivyo??

Kama walikuwa wema kwanini walikuja kututawala,au wewe ni mmoja wa wale wanao amini kuwa wazungu walikuja kutuletea ustarabu??

Hivi utawatofautisha vipi wazungu hasa hawa waingereza na slavery, na all form of Colonial violence??

Seriously kabisa mkuu unasema Wa Britain hawakuwa wakatili??!!!

Niambie kama ni utani mkuu ila haiwezi kuwa serious hii.

Inabidi umsikilize Prof Lumumba uelewe watawala wetu ni watu wa aina gani? Na kuwa wakati ule tulilazimishwa kwenda ulaya kama watumwa, leo tunkufa baharini tukiwakimbia viongozi wetu kwenda Ulaya- Ni maneno ya msomi Prof Lumumba.

Ukitaka kujua kama leo hii muingereza ni mzuri au mbaya, lete meli 100 zile kubwa, halafu waambie watanzania wanaotaka kutupilia mbali uraia wa Tanzania na kwenda kuishi uingereza wapande hizo meli. Sijui kama kuna meli itarudi Tupu.

Najua sisi ni wazuri wa domo, licha ya macho yetu kuona ukweli.
 
Rasi anatoa eti INSTRUCTIONS watu wasilipwe uko ni kuingilia mamlaka ya bunge. Uganda tumeshuhudia spika mwanamke akimchimbia biti Museveni. Huo ndo utawala wa bunge. Raisi hana mamlaka ya matumiz ya bunge kwa mujibu wa katiba yetu. Ni Tanzania pekee yanapotokea

Sent using Jamii Forums mobile app
Tamko la Rais haliingilii mamlaka ya Bunge. Kazi ya Bunge ni kutunga sheria. Ikiwa Rais atasema cho chote kuhusu utungaji wa sheria, atakuwa ameingilia mamlaka yasiyomhusu. Kama hapendi cho chote kilichopitishwa na Bunge, anachoweza kufanya ni kuiambia wizara husika ipeleke mswada bungeni wa kurekebisha kilichofanywa na Bunge. Kama Bunge likiukataa mswada huo, itakuwa ndiyo mwisho wa habari na Rais hawezi kufanya cho chote. (Sana sana anaweza kuvunja Bunge na kuitisha uchaguzi mpya wa Rais na wabunge).

Baada ya sheria kutungwa, Bunge linakuwa limemaliza kazi yake. Kinachobakia ni kazi ya muhimili mwingine (Mahakama) kutafsiri sheria hiyo, bila kuingiliwa na Bunge lililoitunga hiyo sheria. Cho chote kinachoamuliwa na Mahakama ndiyo mwisho wa habari; hata kama wabunge hawafurahishwi na tafsiri ya Mahakama ya sheria waliyoitunga wao wenyewe. Rais naye haruhusiwi kuiambia au kupendekeza Mahakama iamue hivi au vile kuhusu suala lililopelekwa Mahakamani. Huko ndiko kutenganisha madaraka ya mihimili hiyo mitatu: Serikali (ikiongozwa na Rais); Bunge (likiongozwa na Spika); na Mahakama (yakiongozwa na Jaji Mkuu).

Baada ya Mahakama kufikia uamuzi, inakuwa imemaliza kazi yake. Yaliyobaki ni mambo ya kiutawala ambayo yatatekelezwa na Serikali. Kwa mfano mhalifu amehukumiwa kunyongwa, au kufungwa miaka kadhaa; au kulipa faini kiasi fulani. Mahakama haihusiki katika kutekeleza hayo bali Serikali ndiyo inawajibika kuona kwamba adhabu inatimizwa. Kwa kuwa jukumu hili ni la kiutawala, Rais (kama kiongozi wa Serikali) ana mamlaka ya kuamua kuhusu utekelezaji wa adhabu iliyotolewa na Mahakama. Kwa mfano anaweza kuamua kupunguza adhabu iliyotolewa kutoka kunyongwa kwenda kwenye kifungo cha maisha; au kupunguza miaka ya kufungwa aliyopewa mhalifu, n.k. Hizi ni shughuli za kiutawala na si kuingilia mamlaka ya Mahakama. Rais atakuwa ameingilia mamlaka ya Mahakama pale tu kesi bado iko mahakamani na yeye analeta vyake.

Kutenganisha mamlaka ya mihimili hii mitatu kunaishia katika majukumu tu ya kila muhimili. Mambo ya kiutawala yote yako chini ya Serikali bila kujali muhimili unaohusika. Kwa mfano ulipaji wa mishahara kwa wafanyakazi wa mihimili yote, makazi ya watumishi, vitendea kazi (kwa mfano magari ya mahakimu au wabunge), yote hayo ni mambo ya kiutawala ambayo yanasimamiwa na Serikali. Rais akifanya chochote cha kiutawala kinachohusu muhimili wo wote haingilii mamalaka yasiyomhusu.
 
Inabidi umsikilize Prof Lumumba uelewe watawala wetu ni watu wa aina gani? Na kuwa wakati ule tulilazimishwa kwenda ulaya kama watumwa, leo tunkufa baharini tukiwakimbia viongozi wetu kwenda Ulaya- Ni maneno ya msomi Prof Lumumba.

Ukitaka kujua kama leo hii muingereza ni mzuri au mbaya, lete meli 100 zile kubwa, halafu waambie watanzania wanaotaka kutupilia mbali uraia wa Tanzania na kwenda kuishi uingereza wapande hizo meli. Sijui kama kuna meli itarudi Tupu.

Najua sisi ni wazuri wa domo, licha ya macho yetu kuona ukweli.
Nimependa andiko lako. Nami nitaingia kwenda Majuu!
 
HUNA POINT KWA NINI RAIS ASIJIBIWE AU KAWA MUNGU
Lazima mwanasiasa aelewe jinsi vile wananchi walivyo na negative attitude against mabeberu,unaposema Ni Bora udeal na mabeberu kuliko rais wako unategemea wananchi watalipokea vipi?.
Hizi nchi zilizokua za kijamaa,mabeberu,makabaila,wanyonyaji,mabepari,wahujumu Ni no go zone,wananchi walikuwa shaped hivyo tangu mwanzo
 
Seriously kabisa mkuu unasema Wa Britain hawakuwa wakatili??!!!
List hapa ukatili wao wenye ushahidi, mfano walimfungulia Nyerere kesi watu wakachanga kumlipia asifungwa etc.
 
Hujamalizia utamu katika jibu lako, kamilisha kwa kujibu nukuu hii katika quote ". Au nitajie nchi 5 tu kwa mtazamo wako wewe ungewaita ni mabeberu" .

Jibu vitu kamili usirukeruke- Nilichokupata ni kwamba ukienda wewe kuomba kwake yeye si beberu, mpinzani akienda kwa huyo huyo ni beberu.

Nilisema neno beberu halina mantiki kama neno Zeru zeru lilivyokataliwa sasa hivi na serikali. Kwa maana hiyo Mwinyi alilikataa neno Beberu na unyonyaji.

Jibu twende pamoja.
Yeyote yule aliewahi kujitwalia nchi zetu nakuzikalia pamoja na kutuuza utumwani na Sasa wanarudi Tena kwa style ya kuwatumia Chadema Ni mabeberu tu uk France German Belgium USA
 
Inabidi umsikilize Prof Lumumba uelewe watawala wetu ni watu wa aina gani? Na kuwa wakati ule tulilazimishwa kwenda ulaya kama watumwa, leo tunkufa baharini tukiwakimbia viongozi wetu kwenda Ulaya- Ni maneno ya msomi Prof Lumumba.

Ukitaka kujua kama leo hii muingereza ni mzuri au mbaya, lete meli 100 zile kubwa, halafu waambie watanzania wanaotaka kutupilia mbali uraia wa Tanzania na kwenda kuishi uingereza wapande hizo meli. Sijui kama kuna meli itarudi Tupu.

Najua sisi ni wazuri wa domo, licha ya macho yetu kuona ukweli.
Hii hadithi yako haivunji tamko la chadema kupitia bulaya
 
Huu ndio ujumbe alio utoa mbunge wa Bunda mh Ester Bulaya kwenye ukurasa wake wa Twitter baada ya hotuba ya Rais.

Nanukuu

"Ni bora sisi tuendelee kuwatumikia mabeberu kuliko kukutumikia wewe"

Hizi ndio kauli za viongozi walio chaguliwa na wananchi na kupewa dhamana ya kuwawakirisha bungeni.

Kama taifa bado tuna safari ndefu sana Mungu atusaidie.!!
Ni maoni yake na wewe unaweza ukawa na yako pia, misho wa siku siasa ni kushindana kwa haya mawazo na wewe unatetea ya kwako ndio yaonekane bora zaidi, sio rahisi kila mmoja akawa na mawazo ya kufana na mwenzake, hii sio kitu ya kukariri mkuu
 
Yeyote yule aliewahi kujitwalia nchi zetu nakuzikalia pamoja na kutuuza utumwani na Sasa wanarudi Tena kwa style ya kuwatumia Chadema Ni mabeberu tu uk France German Belgium USA

Ha ha haaa, hapa umefunguka - Unajua Paris club inatudai pesa ngapi? Sijamtaja Marekani na Ujerumani. Si CHADEMA WALIOKWENDA kukopa bali ni serikali za awamu zote. Kazi kweli kweliiiii
 
Ha ha haaa, hapa umefunguka - Unajua Paris club inatudai pesa ngapi? Sijamtaja Marekani na Ujerumani. Si CHADEMA WALIOKWENDA kukopa bali ni serikali za awamu zote. Kazi kweli kweliiiii
Kudai ni Jambo lingine na kudaiwa ni jambo lingine ndio maana USA kila siku anamuwekea vikwazo china Wana uadui ukomonisti/ubepari Vita vya kibiashara kila siku wanawekeana vikwazo ila umesahau mdai mkubwa wa USA ni china au hujui USA anadaiwa matrilion ya dollar na china turudi huku na habari za chadema kupitia bulaya huu kwa wenzetu ndio huitwa usaliti
 
Bado ni raisi wetu, anasimamia anachoamini na mwanaume yoyote kusimamia msimamo wako ni kitu cha msingi sana...
 
Inabidi umsikilize Prof Lumumba uelewe watawala wetu ni watu wa aina gani? Na kuwa wakati ule tulilazimishwa kwenda ulaya kama watumwa, leo tunkufa baharini tukiwakimbia viongozi wetu kwenda Ulaya- Ni maneno ya msomi Prof Lumumba.

Ukitaka kujua kama leo hii muingereza ni mzuri au mbaya, lete meli 100 zile kubwa, halafu waambie watanzania wanaotaka kutupilia mbali uraia wa Tanzania na kwenda kuishi uingereza wapande hizo meli. Sijui kama kuna meli itarudi Tupu.

Najua sisi ni wazuri wa domo, licha ya macho yetu kuona ukweli.
Kama kumsikiliza Prof Lumumba na kumuelewa hilo kwangu ni jambo la kila siku, sidhani kama kuna siku inapita bila kusikiliza speech zake.

Ubaya wa viongozi wa Africa uko wazi kabisaa hili halina ubishi, wapenda madaraka ni wengi sana, hawana maono yoyote na muelekeo wa bara la Africa.
Na wengi wao wanatumiwa na hao hao wazungu kukandamiza waafrica wenzao kwasababu ya tamaa za matumbo yao, hawajali uafrica wao na hawajui nini tunahitaji sisi kama Africa.

Any civilization that know what they want always reachs their destinations, do we know what we want we as Africans?

Umesema vema watu watakimbilia ulaya ndio watakimbilia huko, Ila unajua ni kwanini watakimbilia Ulaya.?

Is this not because of poverty in Africa? If that is true, it this not because of white's exploitation our resources?

Do you remember the Briton Wood Institution and their restrictions to Africa?
do you remember the Brandit report commission to Africa?
Don't you remember the new colonial project?
How about globalization is this a good thing to Africa.?

Why do always they threaten us by sanctions?

Watu wetu wanakimbila ulaya kwasababu ya umasikini tulio nao na umasikini huu haukusababishwa na viongozi we pekee japo nao ni majipu yaliyo iva, ili unyonyaji tulio fanyiwa na tunao endelea kufanyiwa ndio sababu ya umasikini huu mkuu. na hata akitokea kiongozi mwenye maono mazuri bado tu atapigwa na hao wazungu.
 
Kudai ni Jambo lingine na kudaiwa ni jambo lingine ndio maana USA kila siku anamuwekea vikwazo china Wana uadui ukomonisti/ubepari Vita vya kibiashara kila siku wanawekeana vikwazo ila umesahau mdai mkubwa wa USA ni china au hujui USA anadaiwa matrilion ya dollar na china turudi huku na habari za chadema kupitia bulaya huu kwa wenzetu ndio huitwa usaliti

Somo limeeleweka, hapa tumeelewana. Ulichokiandika ndicho alichokiweka wazi Mwinyi. Maana biashara ni biashara.

Mwinyi alielewa kitu kimoja- Huwezi kuja ukanitukana (aka kuniita beberu) halafu nikakuomba unikopeshe pesa kumlipia mwanangu karo. Over..
 
Back
Top Bottom