Have you proved that he is suspected criminal?
Tunduma wanachama wa chadema pamoja na wagombea wa udiwani walivamiwa wakakamatwa hadi leo wako ndani na wamebambikiwa kesi.
Arusha polisi wamevamia ngome ya uratibu ya CHADEMA na kukamata wote waliokuwa hapo na kutoa taarifa kuwa ni wahamiaji haramu.
Tarime kwa John Heche wamevamia na kuwakamata wote waliokuwa hapo na computer walizokuwa wanatumia hadi leo hakuna maelezo ya kujitosheleza.
Mgombea mwingine Christina Ruge, amepeleka malalamiko tume ameenda kuulizia majibu ya malalamiko yake kavamiwa na polisi kapigwa hadi kulazwa hospital.
Mgombea wa Urais Chadema misafara yake kupigwa mabomu ya machozi kusimama kusalimia wananchi.
Kwa mifano hii michache polisi this time around wamevamia ofisi ya Mgombea wa Chadema Esther Bulaya, kwa utendaji wao kutokana na matukio hayo utakaa uwasubirie? At least alipokimbilia tukio limeonekana.
Masaa 24 yamepita umesikia taarifa yeyote ya polisi sababu ya kumkamata?
Kuwa upande unaonufaika na mfumo huu na kukejeli, kushambulia, kudhihaki wanaokuwa oppressed ni ukosefu wa akili wa kiwango cha juu. Hivi CCM hamuoni kweli? Mnajitoa ufahamu au ni wapumbavu?
In any injustices there is no neutrality, being neutral is siding with the oppressor.
Nyie hata unafiki hamna mnaonyesha jinsi mlivyo, ila kusaliti amani mnaisaliti Tanzania. Na uzalendo siyo kusupport walio madarakani bali maslahi ya nchi. Ila wakati ni mwalimu mzuri mark my words shabikieni udhalimu
“Have you proved that he is suspected criminal?” ...Swali kama hili linaweza tu kuulizwa na mtu ambaye hajui anachoongea. Hajui tofauti ya criminal na suspected criminal na hajui police force inafanyaje kazi zake. Siwezi kukulaumu. Haya ni matokeo ya elimu potofu inayotolewa na viongozi wa Chadema. Hakuna kiongozi makini ambaye muda wote anahubiri shari, disobedience kwa police force. That’s failed leadership of the highest order! Nasema hivyo kwa sababu vyombo vya dola ni 100% portable. Hapa ninamaanisha kuwa watawala wote watapita, lakini vyombo vya dola vitabaki palepale, vinarithiwa kutoka utawala mmoja hadi mwingine.
Ukikuta mtu anatafuta ridhaa ya kushika dola halafu anahubiri huo ujinga, huyo hajitambui na hajawa tayari kwa kazi anayoiomba. Ukimpa hiyo kazi, maana yake jukumu lake la kwanza litakuwa kuwafundisha wafuasi wake kuheshimu na kutii vyombo vya dola. Kama huo sio uwendawazimu ni kitu gani?
No country on earth has a perfect police force. Not one; not even the most democratic, first-world countries! Bad elements kwenye taasisi yoyote, ikiwemo police force, hazikosekani.
Our police force is neither the best nor the worst. Pamoja na kufanya kazi katika mazingira magumu, jeshi limefanya mengi sana mazuri. Kubwa zaidi ni kulinda amani yetu. Bila hii amani tuliyonayo, hata hizi debates tunazofanya hapa zisingewezekana. Ukiwa na negative orientation (focus) huwezi kuona mema yanayofanyika. Ushauri wangu kwa wote wenye mawazo kama yako: Don’t take our peaceful environment for granted. A lot of brave men and women are making sacrifices every day to maintain it!
Ulichoandika ni malalamiko zaidi kuliko hoja za msingi. Hakuna hoja yenye mashiko uliyoitoa kutushawishi kwanini police force haikupaswa kumkamata mtuhumiwa waliyemkamata. Kila police case ni unique. Uhalali wa kukamata mtuhumiwa yeyote hautokani na results za arrests zingine zilizowahi kufanywa na police force. Hatuwezi kusema kuwa, kwa sababu polisi walimkamata X akashitakiwa mahakamani na kupatikana na hatia, basi polisi wakamate kila anayekatiza mbele yao. Vilevile, hatuwezi kusema kuwa, kwa sababu polisi walimkamata X akashitakiwa mahakamani na kukutwa hana hatia, basi polisi wasimkamate mtuhumiwa mwingine yeyote. Hilo halitokei kwenye nchi halisi bali kwenye taifa la kufikirika la Chadema.
Kila mtuhumiwa anazo haki zake za msingi, lakini resisting police arrest is not one of those rights. If anything, resisting a police arrest is one sure way to run into a very serious problem. Elewa vizuri hapa... Police force ni chombo cha mabavu. Wanaruhusiwa kutumia all means necessary, lethal or nonlethal, kukabiliana na mtuhumiwa kaidi. Kwenye nchi nyingi watu wameuawa na wanaendelea kuuawa na polisi kwa kuendekeza ukaidi. Encounter na police ni kitu chepesi sana kwa mtu asiyetaka dramas zisizokuwa na tija yoyote. Kukamatwa na polisi, whether kwa kuonewa au kutokuonewa, sio mwisho wa safari ya haki kutendeka. Watii polisi kisha onesha ujuaji wako mahakamani ili aibu iwe kwao!