Eternal Punishment cannot be understandable by any one

Nani amekwambia Mungu ni mtu? Au umesoma wapi hiyo?
Vitabu vimeandikwa na watu? Ulitaka viandikwe na nani?
Je ujumbe au yaliyomo pia ni maneno ya watu?
Sawa soma na hiki?
Link http://www.islamicbulletin.org/free_downloads/quran/bible_quran_science.pdf

Unategemea utaishi miaka mingapi?
 
Hii dunia ndio Jehanamu tosha.
Tabu, Magonjwa, Njaa, vifo, Vita etc.

Hakuna binadamu yeyote yule anaejua nini kinatokea baada ya kifo.
Wote tuna hisi tu .
 
Hii dunia ndio Jehanamu tosha.
Tabu, Magonjwa, Njaa, vifo, Vita etc.

Hakuna binadamu yeyote yule anaejua nini kinatokea baada ya kifo.
Wote tuna hisi tu .
Kama umejiumba hivi usemavyo ni sawa. Kama unaamini umeumbwa, kwa nini usiamini kile anachokwambia aliyekuumba?

Katika ulimwengu huu kila anayetengeza kifaa, anaandika na user's manual.
Mungu ameleta user guide/user's manual kupitia wajumbe wake. Ukiukataa ujumbe wake ambao unakueleza nini kinakusubiri baada ya kifo, baada ya kifo hutapata second chance.

kama utapata muda angalia video ambazo nimeweka kwenye uzi huu, ziko ambazo wanasayansi wanakubali sasa kuwa ipo " hereafter".
 
Sheria ya Mungu imewekwa Ktk Akili na Moyo wa kila mtu , hivyo kila mtu atahukumiwa kwa kadiri alivyopewa ,
 
Wakuu nashukuru kwa alieanzisha Uzi huu. Umeeleza vizuri kwamba itakuwa ni ajabu ikiwa Mungu atamhukumu mtu adhabu ya milele hata kama hakuzisikia habari zake Huyo Mungu,na ingekuwa hivyo adhabu ya milele isingekuwa ikieleweka. Lakini kwa mujibu Wa Biblia kuna namna ambayo Mungu atawahukumu watu ambao hawakupata nafasi ya kumjua kama ambavyo Mimi na wewe tumepata.(mfano walioishi kabla ya injili kuwafikia na ambao hawana uwezo Wa kuielewa injili(labda wenye ulemavu Wa akili na kadhalika)..naomba ninukuu kutoka katika Biblia..." Warumi 2:12. Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sheria watapotea(watahukumiwa) pasipo sheria,na wote waliokosa ,wenye sheria watahukumiwa kwa sheria.....14. Kwa maana watu Wa mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati,hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. 15.hao waionyesha kazi ya torati iliyoa ndikwa mioyoni mwao,dhamiri yao ikiwashuhudia,na mawazo yao ,yenyewe kwa yenyewe ,yakiwashitaki au kuwatetea;16 katika Siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu,sawa sawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu." kwa maandiko hayo ni dhahiri kwamba Mungu(anayehubiriwa na Ukristo) atauhukumu ulimwengu kwa HAKI. Naamini sasa inaeleweka kama tukichukulia ukristo ndiyo dini pekee ya kweli.
 
Hakika mungu km yupo basi ndio mdhambi mkubwa

Kjn wawatu kaishi maisha ya dhiki,magumu yakaraha..ajui hayo mambo ya dini bado anamtupa kwenye moto mkali wa milele

Kweli iman kitu mbaya
Mkuu huyo mungu unayesema ni mdhambi atakuwa ni yule anayehubiriwa na dini ambazo adhabu ya watu ambao hawakupata nafasi ya kumjua ni Kali kiasi hicho. Lakini Mungu Wa Biblia anatoa maelezo kuhusu hukumu ya watu Wa namna hiyo...na bila shaka utagundua kwamba ni hukumu ya haki. Rejea Warumi 2:12-16 nimeinukuu hapo huu. Bila shaka utaona kuwa Ukristo una majibu yanayoridhisha zaidi kuhusu jambo hili.
 
Hivi kwanini wanazungumziwa wakristo na waislamu tu kuwa ndiyo kila mmoja hudai yupo sahihi? mbona wanaosema kwa kujiamini kabisa kuwa hakuna mungu na wanaoamini mungu lakini hawana dini hawazungumziwi kuwa nao kila mmoja hudai yeye ndiye sahihi?
 
Utata ni upi sasa hebu fafanua vizuri.
 
Hakuna cha moto wala pepo zile ni story tu kama ilivyo kwa hadithi zingine za kale za mazimwi
Lipi lenye kutufanya tuamini au tukubaliane na maneno yako kuwa ulichokisema ndiyo ukweli wenyewe na sio hisia zako tu?
 
Hao wajanja ni akina nani hebu wataje mkuu tuwatambue.
 
Nikisema kitu fulani hakipo, kazi ya kuthibitisha inahamia kwako wewe unaesema yupo.
Kwahiyo haiitaji kuwa uhakika pindi unapotaka kusema kuwa kitu fulani hakipo? halafu kuna watu hawapingi kuwepo kwa mungu lakini pia hawasemi kuwa mungu yupo je,hawa nao itabidi wakubali tu maneno yako kusema hakuna mungu kwa kuwa wewe umesema tu?
 
Je,wewe huo msimamo wako wa kuamini mungu lakini hauamini dini umewezaje kujua kuwa upo sahihi kwa msimamo huo? Na kuna miungu mingi hapa duniani je,mbona hiyo haijakufanya kuacha kuamini imani ya kuwepo kweli mungu kama ulivyoacha na dini?
 
Hakika mungu km yupo basi ndio mdhambi mkubwa

Kjn wawatu kaishi maisha ya dhiki,magumu yakaraha..ajui hayo mambo ya dini bado anamtupa kwenye moto mkali wa milele

Kweli iman kitu mbaya
Unataka kusema hata hapa duniani ukifanya jambo bila ya kujua kuwa kisheria ni kosa je,huwa anasamehewa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…