Ethiopia 2 Vs Egypt 0; Tanzania tuna safari ndefu sana kwenye soka

Ethiopia 2 Vs Egypt 0; Tanzania tuna safari ndefu sana kwenye soka

Kwa wasiofahamu mechi za kufuzu AFCON zinaendelea , na kwa leo mechi kubwa ni Ethiopia dhidi ya Egypt.

Hii mechi ina uhusiano gani na Tanzania?

Ethiopia kama ilivyo Tanzania siyo taifa kubwa kisoka. Lakini katika mechi hii ukiangalia unaona namna wachezaji wanavyojituma pamoja na kukutana na kigogo wa bara la Afrika, Misri.

Misri kama ilivyo Algeria ni kigogo wa soka la Afrika, akiwa ametoka kucheza fainali miezi michache tu iliyopita.

Lakini ukitazama mechi ya leo vijana wa Ki Ethiopia wame dorminate kila idara, Ethiopia wanacheza kwa kujiamini sana.

Tanzania tuna safari ndefu sana kwenye soka la wanaume.
Tunasema kila siku hapa shida ni Simba na Yanga hatueleweki. Itachukua muda sana ila ngoja tuendelee
 
Tanzania siasa ndio inaua mpira, hata kama unataka uongozi kwenye mpira lazima uwe ni mwanachama wa chama fulani ndio baadaye uje ugombee ubunge.

Timu ikionekana imefanya vizuri kidogo eti inakimbilia kwenye bunge ndio ikasifiwe na wabunge wa chama fulani ili ionekane kwamba wao ni sehemu ya mafanikio hayo. Bure kabisa.
 
Back
Top Bottom