Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 32,639
- 42,908
Kumbuka mkuu, serikali ya Abiy ilikanusha mara kwa mara juu ya uwepo wa majeshi kutoka Eritrea kwenye siku za mwanzo za huu mgogoro ila baadae ilikiri uwepo wao baada ya ushahidi wa wazi kujitokeza, je hiki si kiashiria kwamba huu uamuzi wa kuyakaribisha majeshi ya nchi iliyokuwa adui kwa miongo kadhaa kushiriki vita dhidi ya raia wako waasi ni makosa?No sio makosa shida ni vyanzo vya habari unavyosikiliza au kusoma.
Kabla Eritrea hawajaingia Tigray kupambana na hao waasi, TPLF walishambulia mara 17 Eritrea kwa kutumia maroketi waliyoiba kwenye kambi za majeshi ya serikali. Walichofanya TPLF ni uasi kwa seikali kuu ya Ethiopia na ugaidi kwa seikali ya Eritrea.
Eritrea na Ethiopia wana mahusiano mazuri kwahiyo hakukuwa na sababu ya Ethiopia kuwakataza Eritrea kupambana na adui wao wote.
Marekani ina ushirika wa muda mrefu na TPLF ndomaana hata vyombo vyao vya habari vipo biased, havielezi mauaji pamoja na uporaji wa maeneo unaofanywa na TPLF wala chanzo cha mgogoro nini. Ni mara ngapi uliwahi kusikia Mai Kadra massacre ikiripotiwa na BBC au CNN.
Baada tu ya jeshi la serikali kuingia Tigray, Marekani na washirika wake wakaomba serikali ya Ethiopia itoe jeshi lake Tigray kwa sababu hali ya usalama inazidi kuwa mbaya lakini hakujawahi kuwa na kauli nzito juu ya uasi wa TPLF kwa serikali.
Kitu kimoja ninachomlaum Abiy ni uamuzi wake wa kutoa jeshi Tigray baada ya shinikizo huku akiwa hana plan yoyote ya kuwapunguza kasi TPLF.
Mfano wa Kenya na Alshabaab aliotoa jamaa hapo juu upo ukilinganisha na mazingira ya Eritrea na TPLF upo sawa.
Alafu hili suala la hayo majeshi ya Eritrea kuhusishwa na jinai za kibinadamu huko Tigray huoni kama jukumu hili analibeba Abiy mwenyewe aliyewaalika?
Eritrea iliwahi kuwekewa vikwazo vya silaha na jamii ya kimataifa ikishutumiwa juu ya rekodi zake za haki za binadamu na kuunga mkono uasi huko Somalia, ila Abiy aliwaalika kushiriki vita dhidi ya jimbo la Tigray huoni hilo ni kosa?
Halafu mkuu unafikiri shinikizo ndio lilifanya Abiy aondoe jeshi Tigray au serikali haikuwa na uwezo wa kuendelea kulikalia licha ya kuutwaa mji mkuu wa Mekele?......kama ilikuwa ni shinikizo mbona imekuwa ngumu kwa shinikizo hizo kumfanya Abiy kuruhusu misaada ya kibinadamu ipelekwe huko?