Ethiopia: Facebook yafuta ujumbe wa Waziri Mkuu uliowataka wananchi "kuwazika" TPLF

Kumbuka mkuu, serikali ya Abiy ilikanusha mara kwa mara juu ya uwepo wa majeshi kutoka Eritrea kwenye siku za mwanzo za huu mgogoro ila baadae ilikiri uwepo wao baada ya ushahidi wa wazi kujitokeza, je hiki si kiashiria kwamba huu uamuzi wa kuyakaribisha majeshi ya nchi iliyokuwa adui kwa miongo kadhaa kushiriki vita dhidi ya raia wako waasi ni makosa?

Alafu hili suala la hayo majeshi ya Eritrea kuhusishwa na jinai za kibinadamu huko Tigray huoni kama jukumu hili analibeba Abiy mwenyewe aliyewaalika?

Eritrea iliwahi kuwekewa vikwazo vya silaha na jamii ya kimataifa ikishutumiwa juu ya rekodi zake za haki za binadamu na kuunga mkono uasi huko Somalia, ila Abiy aliwaalika kushiriki vita dhidi ya jimbo la Tigray huoni hilo ni kosa?

Halafu mkuu unafikiri shinikizo ndio lilifanya Abiy aondoe jeshi Tigray au serikali haikuwa na uwezo wa kuendelea kulikalia licha ya kuutwaa mji mkuu wa Mekele?......kama ilikuwa ni shinikizo mbona imekuwa ngumu kwa shinikizo hizo kumfanya Abiy kuruhusu misaada ya kibinadamu ipelekwe huko?
 
Vita dhidi ya waasi huwa haina mipaka mzee ndomaana unaona kuna nchi kibao zipo congo, Kenya yupo Somalia na mifano mingine mingine. Hawa TPLF sio tu waasi wa kawaida bali ni magaidi pia na serikali ya Ethiopia inawatambua hivyo.

Eritrea ameingia Ethiopia kwa ruhusa ya Serikali halali kwahiyo sioni shida hapo. Eritrea walishambuliwa pia na TPLF na wameingia Tigray kupambana nao sio kulinda amani so ni kawaida vifo kutokea kwenye mapambano.

Eritrea imechafuliwa na Marekani sababu mshirika wake ni TPLF. Waliwekewa vikwazo vingi tu ukimjulisha na hivyo vya silaha lakini jiulize ni kitu gani ambacho ni tofauti Eritrea inafanya ambacho hakifanyiki nchi nyingine za Afrika hadi wawekewe vikwazo. Abiy hakukosea kutaka maridhiano na Eritrea sababu mambo ya Ndani ya Eritrea hayamuhusu yeye, mfano, North Korea ni mara ngapi wanakutana na South Korea kutaka kumaliza mgogoro wao, Vipi kuhusu Trump alipokutana na North Korea ambao wana vikwazo pia.

Ni shinikizo mzee sio TPLF walimfanya atoke na lilikuwa kosa la ufundi kuondoka labda tuzo ya Nobel ilimlevya. Misaada gani ya kibinadamu ambayo haiendi Tigray? Mara mwisho hao waasi waligoma kuacha kupambana ili magari ya WFP yapite ila baadae walipoa magari yakaruhusiwa. Pili hata kama serikali ingekataa hayo magari kwenda Tigray kwa sababu za kiusalama bado wangekuwa sahihi sababu kuna matukio mengi ya UN kuhusika kwenye uasi dhidi ya serikali iliyopo madarakani mojawapo ni lile la magari ya WFP kutumika kubeba wapiganaji wa ISIS kutoka Uturuki kuingia Syria.
 
Mkuu 'ugaidi' ni neno lenye tafsiri pana kutegemea na wanaolitumia.

Eritrea iliingia Tigray kwa ruhusa ya Abiy (japo alikanusha uwepo wa Eritra huko) kwa kutegemea ingekuwa rahisi kuifyeka Tplf jambo ambalo limeshindikana.

Tplf wanaonekana magaidi na Abiy sababu wanapinga serikali yake ila kwa raia wa Tigray ni wakombozi.

Eritrea hajawahi kuchafuliwa ila serikali yao ndio waliojipaka matope wenyewe kwa rekodi yao mbovu ya haki za binadamu, udiktet na sasa ni uovu wao walioutenda huko Tigray.

Hayo ya UN kusaidia waasi kwenye migogoro ni hisia tu maana hao hao UN ndio watoaji wakubwa wa misaada,fedha na hata hupeleka askari wa kulinda amani au kusimamia mazungumzo ya amani.
 
Tumia tafsiri yoyote ya ugaidi unayoijua niambie kwa vipi kwenye hiyo tafsiri yako TPLF sio magaidi?

Sio kweli kwamba TPLF wanaonekana ni magaidi sababu wanapinga serikali ukweli ni kwamba wametangazwa magaidi sababu wanafanya matendo ya kigaidi. Kama ni kupinga serikali mbona vyama vya upinzani havijatangazwa magaidi.

Kuhusu rekodi mbovu ya Eritrea ya haki za binadamu, Hivi Tanzania ya Magufuli ilikuwa na rekodi nzuri ya haki za binadamu, Rwanda,Burundi, Uganda, Congo ya Mobutu, Cameroon n.k zote hizo zina rekodi nzuri ya haki za binadamu? Je zimbabwe iliwekewa vikwazo na EU na Marekani sababu ya rekodi mbovu ya haki za binadamu au waliwakorofisha wazungu wenzao wa Zimbabwe? EU siyo UN lakini vikwazo vyao vina nguvu karibu sawa tu na UN kwa nchi za Afrika.

Unaposema UN kusaidia waasi ni hisia tu wakati nimekupa mfano unanifanya niishiwe kitu cha sema tena.

"TPLF wanaonekana magaidi na Abiy sababu wanapinga serikali yake ila kwa raia wa Tigray ni wakombozi" hii kauli inasikitisha na kuhuzunisha.
 
Huenda ugaidi wa Tplf ni kumpinga Abiy kwa kutumia mabavu?...vipi kuhusu jinai waliyofanyiwa raia wa Tigray na pande zilizohusika na hii Vita, huo sio ugaidi?.

...Kinachonikera kuhusu Tplf ni kuwa na tamaa ya kurudi madarakani kibabe na kitendo cha msemaji wa huo muungano wao na Ola kuishi Marekani kinatia wasiwasi.
 
kuna matukio mengi ya UN kuhusika kwenye uasi dhidi ya serikali iliyopo madarakani mojawapo ni lile la magari ya WFP kutumika kubeba wapiganaji wa ISIS kutoka Uturuki kuingia Syria.
Yale magari huenda yalitekwa na Isis.
 
Ethiopia na Eritrea sio mahasimu wala hawana dalili zozote za kugombana. Kwanza uhasimu huwa unaisha, leo hii Ujerumani na Uingereza ni marafiki ila miaka ya 1940s walikuwa wanadondosheana mabomu miji mikuu yao. US walikuwa maadui wa Uingereza wakapigana, walikuwa hawana uhasama na Russia mpaka ikawauzia Alaska kwa bei chee ila leo hii mambo ni kinyume.

Eritrea na Ethiopia walipigana na mgogoro wao wakakubaliana umeisha
 
Kwenye vita lazima raia wataathirika tu tunachoangalia ni nani aliyesababisha na nani anayeindeleza na kwa serikali raia sio walengwa. Serikali haifanyi ugaidi kupambana na waasi ni sawa uniambie serikali ya Syria au Iraq inafanya ugaidi kupambana na ISIS( unaona jinsi ambavyo haileti maana).
 
Kwahiyo unachotaka kusema TPDF hawana makosa. Mbona wewe unaona makosa ya Ethiopia na Eritrea peke yake? Vyanzo vyako vya habari ni vipi mkuu.

TPDF na vijana wa Tigray walibaka wanawake na makosa kibao ya kibinadamu ndani ya Eritrea. Unadhani Eritrea ni wapumbavu kutumia gharama, kupoteza wanajeshi na kukaribisha lawama za kimataifa. Eritrea ina uchumi gani wa kuingilia vita isiyoiathiri.

Ripoti ya UN inaonyesha pande zote zimefanya makosa na ukiukwaji wa haki za binadamu.
 
Yale magari huenda yalitekwa na Isis.
Hakuna huo ushahidi alafu mifano ya UN kukiuka haki za binadamu ni mingi tu. UN imehusika kwenye mapinduzi ya Rais wa Haiti anaitwa Jean Aristide, lakini pia UN imehusika na kusababisha kipindupindu Haiti kilichopelekea vifo sio chini ya watu 10000. UN sio wasafi kama unavyofikiri.
 
Angelikiwa wewe ungefanyaje yani watu wanajitangazia uhuru wao wanavamia kambi za jeshi. Assume mwanza leo inasema si party ya tz inavamia kambi za jeshi na kushikilia silaha na wewe ni raisi ni hatua gani utachukua?
Kwani imeandikwa wapi kuwa ni lazima uilazimishe mwanZa kuwa sehwmu ya Tanzania labda wamwanza wenyewe wamechoka kuwa watanzania na hawaitaki tena Tanzania ndo maana wakaamua kujitenga
 
Kwani ni lazima mlazimishe watu kuwa kwenye nchi yenu ila binadamu bwana mafisi sana ndo maana mnauwawa kila siku yani kwanini uwalazimishe watu fulani kuwa katika sehemu ya nchi yenu
 
Ungekuwa unajua kwanini Mwalimu Nyerere alivunja uchifu. Na kwanini Mzee Karume alipenda kuwaita Wazanzibari wote ni Washirazi ungeelewa logic ya Abiy.

Hata Marekani hii huwezi fyatuka unataka kujitenga na muungano, Uingereza hii hapa wanaotaka kujitenga wanapingwa, Spain kule jimbo la Cataluna linataka kujitenga na maelfu huwa wanaandamana kushinikiza ila viongozi wake wanakamatwa na sio EU, US wala UN wanawaunga mkono wanaojitenga.

Leo hii anatokea Mwafrika anasema "Tplf wanaonekana magaidi na Abiy sababu wanapinga serikali yake ila kwa raia wa Tigray ni wakombozi"

Abiy analinda katiba ambayo inasema Ethiopia ni moja, wether atafanikiwa au la. Na hakuna sehemu katiba yake inamzuia kuikaribisha Eritrea, na hakuna sheria inayomzuia kutumia jeshi kulinda utengamano wa nchi. Ndio maana katiba ilimpa mamlaka ya kutangaza hali ya hatari. Mambo ya jeshi kutokuwa na nidhamu sio kosa lake, na huwezi mshitaki kwa hilo. Hutokana usikie Simon Sirro kashitakiwa kwa kosa la maaskari wamekimbiza bodaboda mpaka Malawi na kupigwa mawe. Unless huyo kiongozi awe amewaagiza wafanye makosa
 
Me nipate mke tu huko jamani.Ngoja nitafute connection, tena kuna vita ndo aje atulie na mimi huku Tandahimba tuliiii
 
Kwani ni lazima mlazimishe watu kuwa kwenye nchi yenu ila binadamu bwana mafisi sana ndo maana mnauwawa kila siku yani kwanini uwalazimishe watu fulani kuwa katika sehemu ya nchi yenu
Waulize Marekani kwanini walipigana vita ya wenyewe kwa wenyewe wakafa watu zaidi ya 600,000 miaka ya 1800s.

Kwanini serikali inakwambia usijiue, ukikamatwa na jaribio la kujiua unafunguliwa mashtaka. Si ni maisha yako wakuache.
Kwa nini unalazimishwa usomeshe wanao. Kwani serikali imewazaa yenyewe, si ni watoto wako.

Hizo ni sheria. Sheria zipo kwa ajili ya kurekebisha tabia za watu. Kuna watu ni wakeketaji kwenye jamii zao, wanaozesha watoto wadogo, wanaua albino na vikongwe hatuwezi waacha kisa tusiwalazimishe. Kama kufa kupo tu

Ndio hivyo hivyo hatuwezi waacha watu wajitenge. Tanzania pekee ina makabila 126+ kwahiyo tuwe na nchi 126 kutoka Tanzania hii, na Afrika ziwe ngapi, na duniani ziwe ngapi. Si zitakuwa elfu kumi na ngapi, maendeleo unaletaje hapo, corona unapambana nayo vipi, usalama unalindaje
 
Wewe unajipa tabu bule kwa kujishughulisha na maisha ya watu ambao wenyewe hawataki mchango wako sasa mwisho wa siku unaambulia kipigo na fedheha juu
 
Wewe unajipa tabu bule kwa kujishughulisha na maisha ya watu ambao wenyewe hawataki mchango wako sasa mwisho wa siku unaambulia kipigo na fedheha juu
Hata wewe ukitaka kumuoa mwanao lazima tukutandike. Ustaarabu unalazimishwa ndio maana hadi leo dunia imetulia angalau tofauti na enzi za kina Genghis Khan
 
Mkuu Tigray wanapigana ili kumuondoa Abiy madarakani na sio ili wajitenge.
 
Kwani imeandikwa wapi kuwa ni lazima uilazimishe mwanZa kuwa sehwmu ya Tanzania labda wamwanza wenyewe wamechoka kuwa watanzania na hawaitaki tena Tanzania ndo maana wakaamua kujitenga
Kwenye katiba ya nchi ambapo raisi uwa anaapa kuilinda na mojawapo ya kiapo ni kulinda mipaka ya nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…