Eti Kwani kuoa ni lazima?

Eti Kwani kuoa ni lazima?

Vijana oeni achaneni na maneno ya kwenye vijiwe vya kahawa,
Ndoa ni tamu.

Msiige watu ambao back ground zao hamuzijui, ndoa ni tamu Tena Ukiwa na pesa ya kubadilisha mboga.

Nyinyi hamkudondoka kama embe , mlizaliwa baada ya makubaliano ya waliooana, kama nyinyi ndiyo wale waliotambulishwa baba zao wakiwa na miaka ishirini, yaani hamkufaidi mapenzi ya baba mna haki ya kuongea mnayoongea,

Au mtu umelelewa na baba huku ukiambiwa mama yako alitaka kukutupa Ukiwa kichanga, au mmelelewa kwenye vituo vya watoto yatima

Ila sisi wengine tunakua tumeogeshwa na baba, tumefundishwa kazi na baba,
Tumeadhibiwa na wazazi wote wawili,
Tumepewa mapenzi ya pande zote mbili,
Kila tunalolifanya Lina baraka ya pande mbili,

Kwanini nisioe, nitazini Hadi lini?

Oeni acheni hizo,.
 
Wewe ulikuwa na bahati mbaya ukaoa chizi na chamoto ukakiona ila hiyo haifanyi ndoa kuwa upuuzi

Ungeoa mtu anayejielewa ukafurahia ndoa Wenda ungekuwa unaipigia promo hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
Alikua ni decent woman..ila nilijiona niko kifungoni nikaona yanini kuishi kama mfunga eti kisa ndoa...nikapita hivi nw na enjoy maisha niko huru kwenda popote kufanya lolote wakati wowote bila maswali wala vikao vya familia.

Ndoa sio ya kila mtu...ukioa/ olewa wewe inatosha.

#MaendeleoHayanaChama
 
Alikua ni decent woman..ila nilijiona niko kifungoni nikaona yanini kuishi kama mfunga eti kisa ndoa...nikapita hivi nw na enjoy maisha niko huru kwenda popote kufanya lolote wakati wowote bila maswali wala vikao vya familia.

Ndoa sio ya kila mtu...ukioa/ olewa wewe inatosha.

#MaendeleoHayanaChama
Sawa mkuu Kila la kheri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio lazima ila kwann mama yako aliolewa
Kailetea Dunia swali gumu
 
Hawa dada zetu naona sijui wamepatwa na Nini ukimpa tu namba yako , anafanya Kazi ya kukuchunguza Kama umeoa au hapana.

Mimi imani yangu inanambia nabidi kusaidia wazazi wangu , masikini, na Yatima tu .

Huu mradi wa Ndoa upo kiupigaji Sana . Bora nisaidie wahitaji kwanza, endapo nipokea wito ntaoa lakini sio kwa kumuonea Mtu Huruma aliyeshindwa kujitunza.

NB tuendelee kutunza Ushuhuda Uzinzi haufi na ni uchafu
Ulazima wa kuoa upo pale unapogombea nafasi fulani ya mamlaka
 
Kabsa kila mtu na akili yake
Anasema akifikisha 50 yrs ndio ataoa. Kisha anatarajia kuona wajukuu zake huku akijinasibu ataishi 90 yrs. Ndio nikamuuliza na mtoto wake akioa after 50yrs ataona wajukuu kaburini? Kumbuka alishasema zinaa haifai.
 
Muulize gates
Kwanini hujasema nimuulize barack obama, badala ya unasema nimuulize gates, ina maana wewe unajifunza kwa waliofeli?

Kila jambo lina faida na hasara zake,ni vile tu tunaamua kukazia fikra faida kuliko hasara za jambo husika

Tukisema tuishi kwa kukazia fikra hasara kuliko faida basi kila kitu hakifai..

hata magari hatutanunua si yanaua watu,ndege pia tusipande maana tutapata ajali..itafikia hatua tutaona kila kitu hakifai..
 
Anasema akifikisha 50 yrs ndio ataoa. Kisha anatarajia kuona wajukuu zake huku akijinasibu ataishi 90 yrs. Ndio nikamuuliza na mtoto wake akioa after 50yrs ataona wajukuu kaburini? Kumbuka alishasema zinaa haifai.
Tell me the difference, ingawa huyu ni mzinzi na huyu ni muasherati. Je, dhambi ya uzinzi ni kubwa kuliko ya uasherati? Kila siku vijana humu tunatoa mada za kuwa mwanaume lazime tuwe na michepuko tena tunaisifia. Kipi kinachokufanya uione ndoa ya muhimu kama kanuni zake huzifuati na huiheshumu.
 
Back
Top Bottom