Yaani Mawakili wa Serikali ni kujitutumua kama vile nchi hii ni ya kwao. Leo huyo Chakula sijui Chavula kawaambia Mawakili wa Utetezi baada ya kuonesha kuwa huwa wanaruhusiwa kwenda kuonana na wateja wao Magerezani kuwa eti wao wanaingia ndani na hata kukagua mahabusu lakini sio mawakili binafsi. Yaani yote hiyo ni kuonesha tu kuwa wapo juu ya Sheria na kuwaonesha Mawakili wa Utetezi kuwa "inferior". Yaani hawa watu hawa wamejaa roho mbaya ile mbaya wanasahau kuwa kuna maisha baada ya kesi na hata baada ya kustaafu kazi. Kesi hizi hutunzwa kama precedents - wanakomaa sana sana kwa kitu ambacho hakipo. Hapo hamna ugaidi - Chavula na Kidando kumbeni kuwa kila nafsi itaonja mauti na mtaacha tu watoto na wajukuu huku duniani!