kaka, niwatetee kidogo hata kama mimi ni wakili wa kujitegemea. zamani kabla sijaondoka huko kwenye mishahara nilikuwa wakili wa serikali. Mawakili wa Serikali huwa wanatembelea magereza kama moja ya kazi zao kabisa, hata mimi nilitembelea sana. tulikuwa tunawasiliana tu na Mkuu wa gereza kuwa aandae watu wake sisi tunakuja kukagua gereza kesho yake, hivyo wakili wa serikali, Hakimu Mfawidhi, RCO na OC CID Sometimes tunaenda, tukifika pale vifuatavyo huwa vinafanyika:-
1. Mahabusu wanapata nafasi ya kutulalamikia kama jalada linachelewa upelelezi, wakili wa serikali atajibu.
2. kama kuna malalamiko dhidi ya Mahakama, hakimu yupo pale atajibu.
3.kama kuna malalamiko dhidi ya polisi, rco na oc cid wapo pale watajibu. etc.
hii huwa inasaidia sana na mawakili wasipoenda gerezani hadi wanajela huwa wanalalamika, kwasababu mahabusu na wafungwa huwa wanaweza kuleta hata fujo kule. anachosema chavula ni kweli wala hajitutumui, kuna maeneo mengine at least kile mwezi huwa state attorneys hasa hao wafawidhi kama chavula, wanatembelea magereza tena yote yaliyopo kwenye mkoa, sio kama sisi mawakili wakujitegemea ambao tukienda pale tunaonana na mteja wetu tu, mawakili wa serikali wakienda pale wanaonana na inmate wote wa gerezani na wanasomewa risala kabisa, na kutembelea hadi kwenye mabweni kukagua. na siohivyo tu wana wajibu pia wa kutembelea na kukagua vituo vya polisi tena kwa kushtukiza ili kuona watu gani wamekalishwa rumande ya polisi bila jalada kuletwa kwao ili mtu apelekwe mahakamani.
usilolijua ni kama usiku wa giza.