Eti Wema mzuri zaidi kumzidi Zari?

Eti Wema mzuri zaidi kumzidi Zari?

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
attachment.php

Kumbe! Imebainika kuwa maneno ‘gold digger ’ katika ulimwengu wa fursa yanamaanisha kuwa ni mtu anayeona fursa na kuzitumia katika ‘ kufaiti’ kupata mafanikio (utajiri ) kwenye maisha.

Zarinah Hassan ‘ Zari The Boss Lady ’
Ndivyo alivyo mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘ Diamond Platnumz ’ , Zarinah Hassan ‘ Zari The Boss Lady ’ ambaye humwambii kitu linapokuja suala la kuona fursa na kuzifanyia kazi

PAMOJA NA HAYO, WEMA MREMBO ZAIDI
Pamoja na sifa hiyo iliyomfanya Zari kuwa mmoja wa mastaa matajiri Afrika Mashariki lakini kwa mujibu wa mashabiki waliomuona ‘ laivu’ usiku wa Ijumaa iliyopita kwenye shoo yake ya Zari All White Party katika Ukumbi wa Mlimani City walisema aliyekuwa mpenzi wa Diamond kabla yake , Wema Isaac Sepetu ni mrembo zaidi kuliko yeye.

Wema Sepetu na Zari The Boss Lady
Likiwa ndani ya mjengo , Ijumaa Wikienda liliwashuhudia wadau wengi ambao walimuona Zari kwa mara ya kwanza wakimshangaa na kudai kuwa yupo tofauti na anavyoonekana.

Kwa mujibu wa mashabiki hao , picha ambazo wamekuwa wakiziona kwenye mitandao ya kijamii zinakuwa zimeeditiwa (kuhaririwa ) na kwamba ukimuona ‘ live ’ huwezi kuamini .

YUPO TOFAUTI NA KWENYE PICHA
“Jamani siamini kama huyu ndiye Zari tunayemuona kila siku kwenye Instagramu maana yupo tofauti sana.

“Kwa waliokuwa wanasema anamzidi Wema wamenoa . Wema ni habari nyingine, ” alisema mmoja wa warembo waliokuwa wakisukumana kumuona Zari.

“Mimi nadhani ni kwa sababu labda amezaa watoto watatu na sasa ana ujauzito wa Diamond wa mtoto wa nne so hawezi kumfikia Wema ambaye bado hajazaa, ” alisema mrembo mwingine akimtetea Zari .

MAKE - UP 100%
“Hamna bwana, kinachombeba Zari ni make - up (vipodozi ) ambavyo anatumia kwa asilimia mia moja lakini Madam (Wema ) hata asipotumia make - up lazima utampenda tu, ” alisema mwingine aliyedaiwa ni Team Wema.

Kuhusu make - up , Ijumaa Wikienda lilizungumza na mmoja wa watu wa Timu ya Diamond ya Wasafi Classic Baby (WCB ) ambaye yupo kitengo cha mapambo ambaye alithibitisha kuwa Zari hufanyiwa make - up kwa muda mrefu hadi mwenyewe akubali kuwa yupo sawa.

Mdau mwingine aliliambia gazeti hili kuwa Zari ni mjasiriamali na ameona kwa Diamond kuna fursa ndiyo maana akakubali kumbebea ujauzito lakini si kweli kwamba ni mrembo kuliko Wema.

“Ameona fursa kwa Diamond . Kwa mfano shoo kama hii (Zari All White Party ) asingeweza kuifanya bila kuwa na ‘ koneksheni’ na Diamond , ” alidai mdau mwingine .

ZARI AMEONA FURSA
Habari zinasema kuwa Zari ameona kuna fursa nyingi Bongo ndiyo maana amekubali kufunga ndoa na Diamond bila kujali kigezo cha umri. Ana umri wa miaka 34 wakati Diamond ni 26.

Akijibu swali juu ya uraia wake wa Uganda na Afrika Kusini na kwamba yeye na Diamond wanatarajia kuishi nchi gani mwanamama huyo alifunguka :

“Tutaishi hapahapa (Bongo ). Kwa utamaduni wetu (Waafrika ) inabidi mwanamke uondoke nyumbani kwenu umfuate mpenzi wako mkaishi wote .

“Watanzania ni watu poa sana , siwezi hata kuwalinganisha ni wakarimu sana . ”

HISTORIA INASEMAJE?
Kuna madai mazito kuwa Zari si mtu wa kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye hana fursa ya kimaendeleo kwani historia inaonesha kwamba wanaume wengi aliowahi kuwa nao walikuwa ni watu wenye nazo.

HAJAWAHI KUWA NA MWANAUME HOEHAE
Baadhi ya wanaume waliowahi kuwa naye wanaosemekana kwamba hawakuwa watu hoehae ni pamoja na aliyekuwa mumewe , Ivan Semwanga ambaye alizaa naye watoto watatu akiwa ni mmoja wa mabilionea nchini Uganda.

Wengine ni Isaac Lugudde ambaye ni staa wa mpira wa kikapu nchini Uganda , mtoto wa mjini nchini Uganda , Farouk Sempala , Jenerali Jeje Odong , wasanii wa muziki, Moze Radio na Weasel , Aziz Azion , Isaiah , Robert Ogwal a .k .a Rasta Rob , Exodus , DJ Shiru , mfanyabiashara mkubwa wa Nigeria na sasa ni zamu ya Diamond
 
Attachments

  • 1430734823669.jpg
    1430734823669.jpg
    104.8 KB · Views: 6,638
We imelda wewe tunajua sana kuwa wema ni boss wako msituletee ushabiki mavi wenu apa mxiuuu kila siku zari zari mbona yeye hana muda na nyie? Ebu acheni uswahili au huyo mpuuzi wenu hana soko mnaona mkimuandika zari ndo mtauza mxiuuu
 
wemaaa.jpgwemasepetuvszarizaladyboss.jpg zari.jpg
Source: GP
Mwenye macho haambiwi ona.....ila zote mi naona zimeeditiwa......hv mtu alitoa kiingilio chake akafanye kompee????
 
Tumechoka na hizi ligi za wema na Zari.Bahati mbaya hawako sawa kiumri hivyo inakua vigumu kuwalinganisha kiujumla.

Umesema kweli mkuu,ila mwenye maadili ya kiafrika asingeacha watt wake yy atafute raha huku bongo
 
Umesema kweli mkuu,ila mwenye maadili ya kiafrika asingeacha watt wake yy atafute raha huku bongo

Ujue kama watoto wake wangekua wana shida halafu mama anakula bata hapo hata mimi ningemlaumu.
Ila wanae wako kwenye gold family wana shida gani? Halafu wameshakua.
Acha afanye yake,huwezi kumkataza mtu kuifuata furaha yake ilipo.
 
We imelda wewe tunajua sana kuwa wema ni boss wako msituletee ushabiki mavi wenu apa mxiuuu kila siku zari zari mbona yeye hana muda na nyie? Ebu acheni uswahili au huyo mpuuzi wenu hana soko mnaona mkimuandika zari ndo mtauza mxiuuu
Binamu mbona Zari nimkubwa sana kwa Wema,yes ni mpuuzi labda na akili yake bado haija changanya lakini Zari unataka kunambia yeye ni Natural beauty yake ile? simchuki Zari wala Simpendi Wema lakini napenda kua fair kwa wote,Wema ana uzuri wake na Zari pia ana uzuri wake...
 
Ujue kama watoto wake wangekua wana shida halafu mama anakula bata hapo hata mimi ningemlaumu.
Ila wanae wako kwenye gold family wana shida gani? Halafu wameshakua.
Acha afanye yake,huwezi kumkataza mtu kuifuata furaha yake ilipo.

Watoto wa siku hizi (hasa wa kishua) wanaishi miezi takribani miwili tu na wazazi, ilyobaki yote shule!
Si hoja sana kuleta hiyo sababu, isitoshe mama yuko kazini!
Si jambo la kijisifu kuishi na watoto muda wote halafu hawana cha kujivunia kutoka kwa mzazi.
 
Yeah,umemaliza yote.
 
We imelda wewe tunajua sana kuwa wema ni boss wako msituletee ushabiki mavi wenu apa mxiuuu kila siku zari zari mbona yeye hana muda na nyie? Ebu acheni uswahili au huyo mpuuzi wenu hana soko mnaona mkimuandika zari ndo mtauza mxiuuu

Hahahaaaa yan global wanasikitisha sana et maoni ya mashabik????? Wangap??? kw utafit upi????? Hv hta sisi tusio vipofu wanatak kutulazmisha tuamin huu ushuz wao????? Poor them!!!!
 
Binamu Mbona yule mwenye Mimba umemficha Insta yule Chausiku na kitumbo kama Fenesi..
 
Back
Top Bottom