Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 2,375
- 4,784
Nywinywinywi Nywaaaaaa!
Chikichiki Pah Pah Paaah!
Hoja hai, haiwi mfu kwa Risasi! Za nini Risasi?
Nashambulia nikitokea upande wa winga wa uchumi. Eee bana wee! Wanazuoni wengi mashuhuru kwenye uwanda wa sayansi ya siasa na uchumi, wamekuwa mara nyingi wakinasibisha jamii huru na zenye haki na maendeleo ya kiuchumi. Nadharia inayowaongoza ni kwamba – jamii huru na yenye haki, ni jamii yenye kujiamini zaidi na kufikiria nje ya boksi bila woga; kitu kinachopelekea wao kujiamini zaidi kwenye utekelezaji wa shughuli za kiuchumi na kuboresha kipato chao.
Nadharia hiyo inathibitika pia zaidi kwa uwazi, unapojaribu kufananisha maendeleo ya kiuchumi na kupaa kwa viwango vya Demokrasia. Mfano mzuri hapa ukiwa ni: Asian Tigers (Nchi za: Singapore, Hong Kong, South Korea na Taiwan, ambazo wana historia wanakuambia zilikuwa kwenye urari sawa wa maendeleo dhidi ya nchi ya ‘Wadanganyika’ mnamo miaka ya 1960’s).
Ni nadharia na fikra hizo hizo zimenituma kufananisha pato ghafi la kichwa kwa mkoa (region per capita) na hali ya kukinukisha iliyotokea siku ya MO29; nimepata matokeo ya kustaajabisha ambayo yanaendana moja kwa moja na tafiti za kidunia (highly significant results).
Ukiachilia madhila yake; MO29 inazidi kutufungua macho kwenye mambo mengi mnoo – mojawapo ikiwa ni hili.
Kwenye huu utafiti ghafi, nimegundua yafuatayo:

- Mikoa iliyokinukisha ina wastani mkubwa wa kipato cha kichwa dhidi ya mikoa ambayo ililala. Hii inaashiria kwamba wananchi wa mikoa iliyokinukisha wanajali sana mapambano yakupigania haki, kwa sababu wanajua kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya haki na maendeleo ya vipato. Symbolically, kuchomwa moto kwa majengo ya mamlaka ya mapato (TRA), TAKUKURU, Mahakama, na Mwendokasi, kunashabihiana moja kwa moja na shughuli za kiuchumi. Sote tunajua hivyo vyombo vinavyowaudhi ‘Wadanganyika’ kila siku na kukwamisha harakati za kupigania vipato vyao.
- Mikoa iliyolala na ambayo hata haikuamka kwenda chooni kukinukisha, ina wastani mdogo kabisa wa pato la kichwa: inaashiria kuwa, ni mikoa ya watu walioridhika na maisha na wavumilivu dhidi ya ukosefu wa haki zote za: kiuchumi, kisiasa, na kijamii, kwenye mikoa yao. Na kwakua sheria kandamizi za mamlaka zinang’ata kama Mbweha mwenye njaa kali wakati wote; wananchi wa hii mikoa wamejikuta kuwa waoga wa kutoka nje ya box, hivyo kukosa chachu ya kupambania fursa za kuboresha vipato vyao. Hii inatuma ujumbe mzito sana kwa wadau wa maendeleo ya kiuchumi: kwamba tukitaka kuinua uchumi wa hii mikoa, ni sharti tuanze na zoezi la kuchechemua ‘mentality’ za wananchi wa hii mikoa, ili watoke katika hali ya kulala -- wanatakiwa wawe aggressive na wenye uwezo wa kutambua haki zao na kuzipambania, come what may. Hii itawaongezea kujiamini pia kwenye kupambania fursa za kiuchumi.
Ufunguo wa Takwimu:
4 Walikinukisha kikanuka vibaya sana! (muharo ulikuwa mwingi sana na ulijaa kindoo!)
3 Walikinukisha kikanuka (muharo ulikuwa robo-tatu ya kindoo!)
2 Walikinukisha kidogo na kujamba sana tuu! (muharo ulikuwa robo kindoo!)
1 Walau waliingia chooni wakajamba sana tuu! (Kindoo hakikuwa na muharo!)
0 Bongo Lala! (Hawakukumbuka kwenda chooni kwakuwa walikuwa wamelala!)
Takwimu
Note: Taarifa ya per capita imetoka kwenye Takwimu za Benki Kuu ya Tanzania za Septemba 2025
Kama kuna mkoa nimeudhulumu naombeni wadau wa hiyo mikoa mnihabarishe, ili niwape masitahili yenu (kama ni Bongo Lala au Bongo Amka basi tuwajue).
Bottom line: Japo mamlaka wanajaribu kudogosha ‘Movement ya MO29’ kwa kuwasingizia wageni, ila kiuhalisia kabisa – ‘MO29 is a localized movement ya Watanganyika halisi walioinuka dhidi ya watawala, kupinga sharia kandamizi za kiuchumi, kidemokrasia, na kijamii.’ Ni masikitiko sana kwa mamlaka kukurupuka na kudogosha hii movement ya kitume na kinabii ambayo itasimuliwa na vizazi! Wapuuzwe wale vitatange waliosema kwamba, "MO29 yalikuwa ni mapinduzi yaliyoshindwa."
Mi nimemaliza kwa leo, nikishambulia kutokea wingi ya uchumi!
Dalali nina habari zako; umepigwa kihalali!
Wenu
MC