Eurocentric & Deterrent Criminal Court: Kama Burundi walijitoa, mpaka sasa Tanzania imenufaikaje na uwepo wa Mahakama inayolenga viongozi wa Afrika?

Kwenye kuadhimisha miaka 75 ya UN kuna tweet nimesoma ambapo nchi mbalimbali 72 zimeunga mkono juhudi na kazi za ICC nimesoma hiyo orodha ya hizo nchi sikuona Tanzania....
Sawa mkuu
 
SISI WENYEWE HATUWEZI kujiongoza kwa kuheshimu taratibu zetu wenyewe.. Angalia al Bashir aliua watu wengi sana kisa tu wana mawazo tofauti...Leo hii anasota jela lakini kwa msaada wa jeshi ila raia wa akwaida hawa angeua vibaya sana.
Mhhh...
 
Njoo kwa Mseven mzee mtu mzima ambae Afrika ingetegemea yeye ndio asaidie wanaongangania Madaraka , lakini anayofanya Uganda nae ni yale yale kutumia majeshi na kukandamiza vibaya kabisa wanaosema tofauti..Haya njoo Burundi na Rwanda Na hata Tz hapo ni yale yale ni laana gani hii???
Doooh...
 
Kule Ivory Coast aliondolewa mtu anaitwa Bagbo kwa kukataa matokeo akapigwa na mkewe wote kwa aibu akaingia Allasane Ouatarra, nae amengangania tayari yaani unasema nani katuroga??? Kila mtu anataka madaraka na akiambiwa jambo anaua haraka sana ..Majeshi ya Afrika yamejaa damu sio za adui damu za watu wenye mawazo tofauti ni aibu na ni laana itaenda na Nyie..WEWE ulieapa kulinda nchi, nchi sio mtu,,usiue raia mwenzio mana hata wewe ni raia una mafunzo tu ya kutumia silaha...
Hii hatari sana mkuu...
 
Ni mpaka pale Majeshi yetu yatakapopata mafunzo sitahiki ya kuacha kuua ndio tutakua huru na hii mahakama kwasasa bora iwepo tu angalau iwatishe...lakini uelewe ukiua hata kwa Mungu ni dhambi achilia mbali hiyo ICC. JIrekebisheni muda ukiisha acha ondoka kwa amani..nchi hizi zipo na wala kujitoa ICC haikusaidii kwani AL bashir si alijitoa je sasa yuko wapi??
Asante kwa mchango wako mkuu
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania;

Kama nchi ndogo za Rwanda na Burundi ambao ni jirani zetu walijitoa kutoka katika taasisi hii inayosemekana inafumbia macho uhalifu unaotendwa na mataifa ya Ulaya (Eurocentric), mpaka sasa Tanzania imenufaikaje na kuwa mwanachama wa mahakama inayoshutumiwa kutumika kama silaha ya kitisho (A Weapon of Deterrence) kwa kuwalenga zaidi viongozi kutoka katika nchi za bara la Afrika?

Was the ICC (International Criminal Court) made for Africa? Should it still be there so as to deter any future political misconducts in the so-called "dark continent"?

View attachment 1620894

Uzinduzi wa mahakama ya kwanza ya jinai ya kimataifa ya aina yake iliyopewa jukumu kubwa la kushtaki, kuhukumu, na kuwaadhibu wale waliohusika na unyanyasaji mbaya sana uilisifiwa sana kama mafanikio makubwa ambayo yangesaidia kuhifadhi na kulinda amani na utulivu wa ulimwenguni kwa ujumla.

Wakati wa hafla ya kutiwa saini kwa Mkataba wa Mahakama (the Rome Statute), katibu mkuu wa wakati huo wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, aliielezea mahakama hiyo kama "zawadi ya matumaini kwa vizazi vijavyo, na hatua kubwa mbele katika mapambano kuelekea upatikanaji wa haki za kibinadamu na utawala wa sheria ”.

Kati ya kesi 11 zilizokuwa zinachunguzwa na ICC mwaka huu wa 2020, 10 zinahusisha nchi za Kiafrika. Kati ya hizo 10, tano ni rufaa binafsi za nchi (self-referrals) - yaaani serikali inajielekeza kwa ICC kuchunguza hali fulani ya uhalifu ndani ya eneo lake kwa sababu haiwezi kushtaki wahusika wa uhalifu ambao uko ndani ya mamlaka ya ICC - mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita, na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Mpaka kufikia mwaka 2018, hati zote za kukamatwa na mashtaka yaliyotolewa na ICC ni za Waafrika, pamoja na wakuu wawili wa nchi kwa wakati huo - Omar Hassan al-Bashir wa Sudan na Uhuru Kenyatta wa Kenya.

View attachment 1620896

Uelekeo huu wa kushangaza wa mahakama juu ya Afrika, haswa kesi dhidi ya al-Bashir na Kenyatta kwa wakati ule, ziliwakasirisha sana viongozi wa Afrika, na kusababisha kuibuka kwa lawama juu ya upendeleo wa kibaguzi.

Mnamo Oktoba 2013, Jumuiya ya Nchi za Afrika (AU) iliwataka mataifa ya Afrika kutoshirikiana na ICC, baada ya Baraza la Usalama kukataa kuahirisha kesi dhidi ya viongozi hao wawili (Kenyatta na Al-Bashir).

Waziri Mkuu wa zamani wa Ethiopia Hailemariam Desalegn aliwahi kuishutumu mahakama hiyo kuwa taasisi ya kibaguzi "ikiwawinda" Waafrika wakati Burundi, ambayo ilikuwa nchi ya kwanza kujiondoa uanachama wa ICC, iliikosoa kwa kuwa "chombo cha kisiasa kinachotumiwa na mamlaka [za kigeni] kumwondoa yeyote yule wanayemtaka kutoka madarakani katika bara hili pendwa la Afrika ”.

Kuna baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanadai ya kwamba, tuhuma za upendeleo na ubaguzi wa waziwazi zimetiwa chumvi zaidi. Wanasema ya kwamba, ni wazi kuwa ni sehemu ya ujanja wa wanasiasa na viongozi wanyanyasaji wa bara hili la Afrika ambao walishiriki ukatili mkubwa na wa kutisha na wanatafuta unafuu ya kutotupwa jela.

View attachment 1620902

Je, Tanzania imenufaikaje na kuwa mwanachama wa ICC mpaka sasa ilhali jirani zake Rwanda na Burundi walikwishajitoa zamani sana?

Should the East African Community (EAC) boycott the ICC with the same steady, resolute and unwavering stance?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Safi sana mkuu
 
Ngoja wataalam waje. Kwanini Burundi walijitoa huko ICC?
 
Mkuu naona kuwa si sahihi kutumia na nchi zembe kama Burundi na Rwanda.
 
Ukiwa muhalifu lazima utetemeke na kuigopa mahakama.

Wahalifu mmeanza kubabaika na kumangamanga!

Ohh ati ICC imetusaidia nini!! Ulitaka ikuletee chakula mezani??!

ICC is the court of law responsible to TRY criminals and pose a deterrent effect to any potential future criminal conducts.

Mnakimbia kimbia hovyo!! Tulia hapo muwajibishwe kama mnastahili.
 
Mkuu naona kuwa si sahihi kutumia na nchi zembe kama Burundi na Rwanda.
Huyu jamaa ni haijui mahakama vizuri, Bali propaganda ndio anasikiliza eti ipo kuwaonea viongozi wa Africa
Mbona kuna viongozi kutoka vita ya Bosnia na Serbia (Europe) wamehukumiwa wengi tu? Mbona Kuna cases za Myanmar kuuwa was Rhohingya zinachunguzwa? Mbona

Sikiliza propaganda za na dikteta ambao wanatumia kigezo cha Waafrica vs Wazungu kila Mara dunia inapojaribu kuwaambia waache unyama dhidi ya wananchi wao
 
Back
Top Bottom