Ewe Allah! Wape nusra ndugu zetu wa palestina

Ewe Allah! Wape nusra ndugu zetu wa palestina

Abu Ubaidah Commando

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2016
Posts
7,591
Reaction score
6,946
20220808_215751.jpg

Amiin thumma amiin!
 
Cha kushangaza hao Mazayuni wamezungukwa na nchi za Kiarabu pande zote! Lakini kwa miaka nenda, wanaangalia tu kwa macho uonevu wote wanaofanyiwa hao Wapalestina! Tangu wapigwe kwenye vita walivyo kurupuka vya 1956, 1967, na 1973! Wamepoteana kabisa! Hakuna cha Arab League, wala nini!

Yaani ni Iran pekee ndiyo inajitutumua kupitia misaada yake ya siri ya kijeshi kwa Herzibollah ya Lebanon na pia Hamas! Nchi kama Saudi Arabia ndiyo kwanza iko busy kunyonga wananchi wake tu kwa makosa ya kufikirika!

Pasipo kuungana kupambana na Mazayuni, mtaishia tu kutoka machozi kama yale ya samaki. Mwisho wa siku hayo machozi yote yatakwenda na maji.
 
Hiyo sala/jumbe imenikumbusha ubishi wa nabii Eliya na manabii wa Baali (1 Wafalme 18:21-27): Labda Allah aitwe kwa sauti kuu maana ni mungu huyo, Au Allah anamazungumzo, Au Allah amesafiri, Au Allah amelala sharti aamshwe awasaidie wa Palestine
 
Unaacha kuombea ndugu zako waafrica wanaoteseka kwa kukosa huduma nzuri za afya,wanaoteseka kwa kukosa chakula na wanaoteseka kwa maovu yanayosababishwa na vita mbalimbali ndani ya africa.unaenda kujipendekeza kuwaombea watu ambao kwanza hawajawahi kutambua kama wewe ngozi nyeusi ni binadamu kamili au sio.
Unafiki mtupu.
 
Back
Top Bottom