Ewe jobless usijione mnyonge au kukosa furaha, ndugu zako tuko hapa

je chama kina faa na kina umuhimu??


  • Total voters
    139
Katibu wa chama cha majobless (wasio na ajira).


1. Kuongoza na Kuratibu Shughuli za Chama

1.Kusimamia shughuli za kila siku za chama.

1.Kuandaa na kusimamia mikutano ya wanachama.
  • Kuhakikisha chama kinafuata katiba na malengo yake.

2. Utetezi na Ushawishi


  • Kuandaa na kusambaza maoni ya chama kuhusu ajira na uchumi.
  • Kuwasiliana na serikali, sekta binafsi, na mashirika yasiyo ya kiserikali kutafuta fursa za ajira na uwezeshaji.
  • Kuendesha kampeni za uhamasishaji kuhusu haki za wasio na ajira.

3. Kupanga na Kusimamia Miradi


  • Kutafuta na kuratibu fursa za mafunzo ya ujuzi kwa wanachama.
  • Kuanzisha programu za kusaidia wanachama kujiajiri.
  • Kusimamia miradi ya chama kama vile vikundi vya ushirika au biashara za pamoja.

4. Uhusiano na Wanachama


  • Kuhakikisha wanachama wanapata taarifa muhimu kuhusu maendeleo ya chama.
  • Kupokea na kushughulikia maoni na changamoto za wanachama.
  • Kuratibu uandikishaji wa wanachama wapya.

*****5. Usimamizi wa Fedha na Rasilimali


  • Kusimamia mapato na matumizi ya chama kwa uwazi.
  • Kuratibu mbinu za kutafuta fedha kama vile michango, ada za uanachama, na ufadhili.

Asante sana ndugu wajumbe , leo nimepokea majukumu yangu kama katibu naahidi kukitumikia chama kwa moyo mmoja πŸ™
 
Dah nipo apo mwenenu sijui mtanitaje ila Nina miaka 9 mtaani ikifka mwez wa 7 mwaka huu nafkisha 10..
 
Mbona kama chama kipo serious sana πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
je uki mpa mchongo asiye!.
kivipi sasa, michongo inamsaidia kila mtu

mheshimiwa unatakiwa uelewe vyama vingi vinasambaratika kwa kukosa dira

angalia chama kama CHAPUTA, au KATAA NDOA, havina nguvu kwasababu havina tija!

na havina tija kwasababu havina dira

ukiweza kusaidia vijana basi chama chako kitakuwa chama bora
 
Ondoa shaka hilo litafanyiwa kazi kwa uzuri mkuu.
 
mshamba_hachekwi Soma hii uta tuelewa.
 
Wanaandaa mkutano halafu wanaenda kutiaana moyo kwa nini wasitumiane tu sms πŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
tuone utekelezaji sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…