Ewe kijana Mpananaji Mpira na Mapenzi visikupotezee Mda wako

Sasa unasimamia kipi katika mada yako!?
 
Sasa unasimamia kipi katika mada yako!?
Bado Messi alijitafuta kwanza kabla ya kumuita Antonella.
Kwanza walianza mahusiano wakiwa na umri mdogo sana, baadaye wakaachana Messi akaenda kutafuta maisha pale Barca, Antonella akasoma mpakaa digrii ya Udaktari akawa na mahusiano na jamaa mmoja hivi. Baada ya Messi kupata maokoto ya kutosha akarudi kumtafuta Antonella, akamuachisha na jamaa, jamaa alilalamika sana, Antonella hakujali, alitaka kuwa na mwanaume bora zaidi yake yule jamaa.

Kujitafuta kwanza , ukipata maokoto plus umaarufu, utapata msichana yeyote unayemtaka.
 
Maisha si kama unavyodhan kila kitu ukikifanya kwa sana kina leta madhara yake point ya msingi ni kusimama katika malengo yako kisha kumuomba Mungu.Mafanikio katika maisha yanasiri nying sana unaweza ukatafuta sana Na usipate huku umejinyima sana.tafuta pesa,wekeza pesa,tumia kidogo,pendeza jali familia yako toa sadaka,toa zaka,saidia wasiojiweza hata kwa kidogo
 
Well said
 
Imagine unajinyima hivyo, hupati good time, unajibanaaa afu mwisho wa siku unakufa unaviacha.
Hata Mola hapendi. Acha tuyaishi maisha.
Mawazo ya kimaskini haya. Umaskini siyo sifa nzuri ni dalili ya laana
 
Upo sahihi lakini kwenye ishu ya mpira nadhani kila mtu ana kitu anachokipenda na kinahitaji muda wake. Kama kijana unaejitambua unapaswa ujue na upangilie ratiba yako kulingana na vipaumbele vyako.

Binafsi napenda sana mpira lakini siwezi vuruga ratiba za michongo ya pesa kisa mpira ambao bila kuwa na hiyo pesa sitoenjoy.
 
Wachache wanaweza hivyo
 
Yapo mamtu yanazunguka na timu Kila ikienda kucheza sehemu yoyote sijui kazi yanafanya saa ngapi, yapo ma mtu yanafunga kazi mapema eti timu Yao inacheza hizi ni akili za kimaskini
 
Jitihada haizidi Kudra
 
Kijana usikubali kufanya mambo ya ujana uzeeni. Kila umri utauishi na hautajirudia.

Katika muda wa kufanya kazi Fanya kazi kwa bidii, jiwekee akiba, jenga makazi ya kudumu, tengeneza mfereji wa kipato usio rahisi kukauka, furahia maisha kadri unavyoweza katika umri sahihi.
 
Mpira kwaTazania ni chanzo cha umaskini na Njaa
 
Huwezi kufanya kazi kwa bidii na huku uko bize na mademu na mpira.

Utaishia kulaumu serikali ya ccm tu
 
Hizi week 3 nimejikuta busy sana na kazi asee nimehisi kupata vidonda vya tumbo maana usiku tumbo linakata nikila linaacha jana nikarudi kushabikia timu yangu ya Yanga na bia zangu nne nahisi nimepona asee let's us live life to the fullest maisha ni mafupi sana,tukiwa tunatafuta maisha tusisahau kuishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…