Kuna shemeji yangu alikuwa anafanya kazi kwa wahindi kama general manager. Alikuwa anapiga mishe zake kimya kimya kwa kujiongeza so akawa ana make pesa na mkewe ( binamu) alikuwa yupo vizuri kusimamia maisha so wakasonga.
Akajenga nyumba yake fresh akanunua gari akawa amemuachia mkewe ndio anatumia. Siku moja alipopata mtoto wa pili akawaalika wenzake kwa mara ya kwanza hapo kwake, alifanya sherehe mbili, ya kwanza ya shukurani ya kujenga nyumba na makazi mapya na ya pili kumpokea mtoto wa pili.
Kumbuka mara ya kwanza walipokuja kusalimia mtoto wa kwanza alikuwa bado kapanga chumba na sebule. Safari hii wanakuja wanamkuta yupo katika nyumba ya kisasa ya vyumba vitatu tena kubwa na iliyofanyiwa finishing na nje kuna gari ndogo imepaki.
Naona wale wenzake walipoondoka ile hali ya mwenzao kupata mabadiliko mazuri ndani ya muda mfupi iliwanyima amani ya moyo wakaona hapana, lazima huyu arudi katika hali ya zamani kwann atupite hivi.
So wazee wa fitina wakaona wakachonge ngenga kwa mdosi kule ofisini kwao. Aiseee shem wiki moja tu baada ya ugeni ule anashangaa anaitwa na uongozi, na anafika wanamuuliza maswali ya ajabu ajabu ya kumtafuta uchawi.
Huku na kule wakamchana live kuwa ameibia kampuni pesa nyingi sana. Akawaambiwa kama wanaushahidi wamuonyeshe huo wizi. Jamaa wakaanza muuliza kuhusu mali zake, akawaambia kuwa yeye na mkewe wanapambana usiku na mchana na biashara na yeye anajichanga ndio maana kafika hapo.
Mwisho wa siku wahindi wakakosa hoja ila sababu ya hofu wakamtoa kazini akarudi kitaa. Akatingishana nao wakamtoa mpunga wake, akaanza kupiga biashara zake ndogo ndogo. Ilimchukua muda maana hapo katikati alipitia msoto sana kimaisha. Ila baadae akakaa sawa akaendelea na biashara maisha yakakaa sawa.
Siku kadhaa mbele akaja kutana na mojawapo ya madereva aliyekuwapo kazini kwao kwa wahindi na yeye alitolewa mzigoni. Jamaa ndio kumwambia yaliyotokea yote na kumtajia waliomfanyia figisu kwa uongozi kazini kwake.
Shemeji akasikitika sana. Kumbe watu wa karibu aliowaamini na kudhania wanafurahia maisha yake kumbe wamekunja roho zao kwa husuda na wivu. Tena wengine wameshamlilia njaa sana na amewasaidia bila kuwakopesha.
So mleta mada unatakiwa kujua dunia ya sasa na jamii ya sasa haya mambo ya kuleta ukaribu wa kipuuzi mara nyingi huleta hasara nyingi kushinda faida sababu watu kwa sasa maisha yanawabadili akili na kuwa na akili za kindezi sana.