Ewe mfanyakazi, jitahidi kuwatembelea wenzako ujifunze maendeleo wanayofanya

Ewe mfanyakazi, jitahidi kuwatembelea wenzako ujifunze maendeleo wanayofanya

Hapa ndipo umaskini wa watanzania wengi ulipo.Wahindi hawana nyumba wanapanga nyumba za msajili wa majumba na ni matajiri hatari watoto wanasoma kanada nk

Waswahili tunapenda sana kulalia pesa!!! Kazi ya hiyo nyumba nzuri ni nini zaidi ya kulala na kuamka? Hakuna cha kujifunza hapo ujinga mtupu

WAkenya ukimtembelea mgumu sana kukupeleka nyumbani atakuambia twende kwenye biashara yangu na ukifika sio ushangae shangae lazima ununue kitu siuo akupe offer!!! Pale sio sehemu ya utalii !!

Mswahili ukibishana naye kidogo utasikia mimi nina kwangu wewe una nini? Na ukisalimiana naye atakwambia karibu kwangu kumbe lengo lake akuonyeshere hizo pesa alizolaza kwenye matofali badala ya kuwekeza.Anakuonyesha jinsi anavyolalia pesa na kuamka.Jumba hilo mamilioni ya pesa la kulala na kuamka .IDLE CAPITAL invested in beds and siitting rooms!!!

Mleta mada shtuka nyumba nzuri kwa ulimwengui wa sasa sio kitu cha kumbabaishia mtu watu wameshahama huko wamebaki washamba wachache kama wewe
Well said mkuu,
Ni bora kujiwekeza kwenye shughuli itakayo generate income kuliko kuzika pesa kwenye ujenzi ambao hautaisha mara moja.
 
Kwa kweli kuna ufahari kuitwa baba mwenye nyumba na sio baba mwenye gari.
Nyumba unaweza itumia kukopa ivyo ikatumika kama asset pia
Kujenga kama hali tete ni bora usubirie ujenge ukiwa na cashflow ya uhakika sababu hakuna kitu kibaya kama kutazama mjengo umeishia katikati hata haujafika kwenye rinta, halafu hela ikate.... Babu unaweza tamani kukaba umalizie nyumba hiyo.
 
Kwenye kila msafara wa kenge kumbuka mamba wapo pia

So unapoamua kufungulia kutembelewa au kutembelea jua pia Kuna kujifunza na kufitiniwa.
 
Hakuna cha kujifunza kwa mtu mkuu lamda sema unapambanaje kutimiza malengo yako. Ok unaenda kwa uliyehitimu naye anajumba nzuri na gari nzuri na anaproject fulani amazing unajua nje ya salary anapata kiasi gani. Unajua haya Mambo ni mepesi kama unavyofikiria lakini sio raising hvyo. Nakumbuka miaka kama iliyopita nilkua napata tabu sana kupitia kwa nilihitimu nao chuo lakini badae nkajagundua nakosea sana nikadili na mipango nliyokuwa nmejiwekea, kiukweli nmepiga hatua kubwa sana tena kwa furaha. Mtumishi upo local government kuipata posho yako ya halali mpk usubiri own source ambayo inaweza chukua mpaka miezi sita kuipata alafu unajilinganisha na classment wako yuko central government anamarupurupu kila kukicha na hamna longolongo ndio ujilinganishe naye.
 
Back
Top Bottom