Ewe mfanyakazi, jitahidi kuwatembelea wenzako ujifunze maendeleo wanayofanya

Well said mkuu,
Ni bora kujiwekeza kwenye shughuli itakayo generate income kuliko kuzika pesa kwenye ujenzi ambao hautaisha mara moja.
 
Kwa kweli kuna ufahari kuitwa baba mwenye nyumba na sio baba mwenye gari.
Nyumba unaweza itumia kukopa ivyo ikatumika kama asset pia
Kujenga kama hali tete ni bora usubirie ujenge ukiwa na cashflow ya uhakika sababu hakuna kitu kibaya kama kutazama mjengo umeishia katikati hata haujafika kwenye rinta, halafu hela ikate.... Babu unaweza tamani kukaba umalizie nyumba hiyo.
 
Kwenye kila msafara wa kenge kumbuka mamba wapo pia

So unapoamua kufungulia kutembelewa au kutembelea jua pia Kuna kujifunza na kufitiniwa.
 
Hakuna cha kujifunza kwa mtu mkuu lamda sema unapambanaje kutimiza malengo yako. Ok unaenda kwa uliyehitimu naye anajumba nzuri na gari nzuri na anaproject fulani amazing unajua nje ya salary anapata kiasi gani. Unajua haya Mambo ni mepesi kama unavyofikiria lakini sio raising hvyo. Nakumbuka miaka kama iliyopita nilkua napata tabu sana kupitia kwa nilihitimu nao chuo lakini badae nkajagundua nakosea sana nikadili na mipango nliyokuwa nmejiwekea, kiukweli nmepiga hatua kubwa sana tena kwa furaha. Mtumishi upo local government kuipata posho yako ya halali mpk usubiri own source ambayo inaweza chukua mpaka miezi sita kuipata alafu unajilinganisha na classment wako yuko central government anamarupurupu kila kukicha na hamna longolongo ndio ujilinganishe naye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…