Ewe mwanamke, ukigundua mme wako kapata mtoto huko nje na huna mpango wa kuondoka kaa kimya usimuulize, Ukweli utamuweka huru mwanaume sio wewe

Ewe mwanamke, ukigundua mme wako kapata mtoto huko nje na huna mpango wa kuondoka kaa kimya usimuulize, Ukweli utamuweka huru mwanaume sio wewe

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Hasa kwa wale vinganganizi kutwa nzima kufatilia kama mwanaume ana mtoto nje, ukiupata ukweli ujipange kisaikolojia!! ni heri ukae kimya umwache mme wako kama alivyo wewe kaa kimya tu maisha yaendelee

(1) Mwanzo alikua anawasiliana na huyo Mama wa mtoto kimya kimya,hakutaka ujue, alikua anaogopa kukuudhi, lakini ukishajua basi atampigia na ukimuuliza atakuambia “Nilikua namjulia hali ya mtoto!” Ukikasirika atakununia kuwa humpendi mwanae.

(2) Alikua anahudumia kimya kimya, hata kama pesa kapeleka huko atakopa ili usijue. Ila baada ya kujua, takuambia, msahara nimemlipia mwanangu ada, sina pesa nyingine. Ukilalamika utasikia, “Mwanamke una roho mbaya inamaana hutaki nimsomeshe mwanangu!”

(3) Alikua hajawaambia ndugu zake, au aliwaambia lakini walikua wanamuona mtoto kisiri. Ila ukishajua, atakuambia kabisa natamani nimpeleke mtoto kwa Mama amjue, ukilalamika utasikia “Inamaana hutaki ajuane na ndugu zangu, acha roho mbaya…” hata ndugu watakuchukia kwakua ni damu yao.

(4) Asingeweza kumleta kwako kwakua hamjui, hata kama hapendi mazingira ya huko kwa Mama yake, lakini ukishajua atakuambia nataka kumleta, ukikataa atakuambia “Hapa ni kwangu huwezi kunipangia, una roho mbaya kama nikiwa hao hutaki aje kujuana na ndugu zake nikifa itakuaje!”

(5) Alikua hampost siku yake ya kuzaliwa, akienda kumsalimia anaendakimya kimya. Lakini ukishajua ataenda kumslaimia, siku ya kuzaliwa atampost na huyo Mama mtoto naye atapost kukuumiza roho ukilalamika utasikia “Kwani wewe unakosa nini hapa ndani, mbona unaroho mbaya!”

AKILI KICHWANI, USITUMIE MOYO KUFIKIRI!
 
Halafu hii makala ineandikwa na mwansume

Pole kwa mama mzazi wake

Mtoto wa kiume kuandika mambo yake

Eee.Mungu tunususuru waja wako na hili janga la watoto wa kiume kupenda habari za kike
 
Halafu hii makala ineandikwa na mwansume

Pole kwa mama mzazi wake

Mtoto wa kiume kuandika mambo yake

Eee.Mungu tunususuru waja wako na hili janga la watoto wa kiume kupenda habari za kike
Hilo ni onyo kwa wanawake wenye midomo mirefu kutwa nzima kuchunguza yasiyowahusu, jibu wakilipata wawe tayari kukabiliana na matokeo yake... mtoto akililia wembe mpe!!

Ubongo mtu wangu!!
 
Hilo ni onyo kwa wanawake wenye midomo mirefu kutwa nzima kuchunguza yasiyowahusu, jibu wakilipata wawe tayari kukabiliana na matokeo yake... mtoto akililia wembe mpe!!

Ubongo mtu wangu!!
Waachie wenyewe na wewe acha kuchonga mdomo

Two wrongs don't make a right.

Pambana na hali yako
 
Mtoa mada nimekuelewa sana yaani tangu huu mwaka uanze leo ndio nimeelewa ushauri vizuri.

Ukishajua ana mtoto nje ni mambo mawili unapaswa ufanye: umwambie ukweli na uachane nae.

La pili kama unajua hauwezi kuachana naye ushauri wa mtoa mada ni mzuri sana ni kupiga kimya afanye kwa kujiiba hivo hivo. Amfiche huyo mtoto wake kama bangi.
 
Inahitaji moyo wa chuma kukalia kimya jambo kama Hilo.

Moyo wa chuma haswa!
Ila ukishamuuliza tu unakuwa umempa nafuu kubwa sana na atalala usingizi mzuri akijisemea “bora hata ameshajua”.

Unajua hamna kitu kinamtesa mtu kama kuficha siri ambayo inapaswa isiwe siri? Na pia anakuwa anateseka kila siku akiwaza aanzaje kukwambia ukweli? Na akikwambia ukweli utachukua hatua gani? Hiyo hali ni mateso sana.

Ila ukijua mwenyewe na akijua umejua unakuwa umemrahisishia kazi sana.
 
Wanawake ni waduanzi tu, ata kama unaweza waletee jeshi zima la watoto
 
Halafu hii makala ineandikwa na mwansume

Pole kwa mama mzazi wake

Mtoto wa kiume kuandika mambo yake

Eee.Mungu tunususuru waja wako na hili janga la watoto wa kiume kupenda habari za kike
Kuzungumzia maslahi ya familia ni jambo la kike?
Mungu aepushe hiki kizazi cha mashuga mami
 
Mtoa mada nimekuelewa sana yaani tangu huu mwaka uanze leo ndio nimeelewa ushauri vizuri.

Ukishajua ana mtoto nje ni mambo mawili unapaswa ufanye: umwambie ukweli na uachane nae.

La pili kama unajua hauwezi kuachana naye ushauri wa mtoa mada ni mzuri sana ni kupiga kimya afanye kwa kujiiba hivo hivo. Amfiche huyo mtoto wake kama bangi.
Hapo Kwenye kukaa kimya jamani kugumu. Mi ntakuambia tu, ila ndo asimlete kwangu.
 
Moyo wa chuma haswa!
Ila ukishamuuliza tu unakuwa umempa nafuu kubwa sana na atalala usingizi mzuri akijisemea “bora hata ameshajua”.

Unajua hamna kitu kinamtesa mtu kama kuficha siri ambayo inapaswa isiwe siri? Na pia anakuwa anateseka kila siku akiwaza aanzaje kukwambia ukweli? Na akikwambia ukweli utachukua hatua gani? Hiyo hali ni mateso sana.

Ila ukijua mwenyewe na akijua umejua unakuwa umemrahisishia kazi sana.
Hannah[emoji2935]
 
Hasa kwa wale vinganganizi kutwa nzima kufatilia kama mwanaume ana mtoto nje, ukiupata ukweli ujipange kisaikolojia!! ni heri ukae kimya umwache mme wako kama alivyo wewe kaa kimya tu maisha yaendelee
Ukweli mchungu sana huu!
 
Japo watakupinga ila mtoa mada umeeleza kitu kizuri sana mwenye akili na ajitafakari.

Big up
 
Hapo Kwenye kukaa kimya jamani kugumu. Mi ntakuambia tu, ila ndo asimlete kwangu.

Ndio hamleti ila yeye ataenda. Atapiga naye picha atampost na status na profile pic . Atamchukua weekends atampeleka kwenye michezo ya watoto ata vimba naye huko na mapicha kedekede atauaweka utayaona.

Ila jamani inaumiza. Ndio maana watu wanachukiaga watoto wa nje inahitaji ujasiri sana na Hofu ya Mungu kuwapenda.
 
Back
Top Bottom